Mchezaji wa Mpira wa kikapu wa kulipwa nchini Marekani katika ligi ya NBA Hasheem Thabeet ambaye yuko nchini kwa mapumziko mafupi anatarajia kukutana na wachezaaji washule za Sekondari za jiji la Dar es salaam pamoja na wachezaji wengine wa mpira wa Kikapu katika uwanja wa ndani wa Taifa kesho Jumamosi tarehe 08/5/2010 kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi 10:00 jioni.
Shirikisho la Mpira wa kikapu Tanzania (TBF) kwa kutambua umuhimu wa Mchezaji huyu na nia yake katika kuendeleza Mpira wa kikapu kwa Vijana wadogo tumeona ni vyema Hasheem akapata nafasi ya kuongea na wanafunzi hao.
Dhumuni kubwa ni kuongea na Vijana, kuhamasisha michezo mashuleni, kujituma katika masomo na jitiada ya mazoezi pia vijana watapata nafasi ya kuuliza na kuonywesha mambo machache ya kuzingatia.
Katika kufanikish hilo Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) linatoa wito kwa Timu za Mpira wa kikapu katika Shule za Sekondari za jijini Dar es salaam,taasisi binafsi za wachezaji wa Mpira wa kikapu (Kids Basketball Camp) kufika katika Uwanja wa ndani wa Taifa ili kupata nafasi ya kuongea na mchezaji huyo wa kimataifa wa kulipwa ambae amepata mafanikio makubwa.
Mkutano huo unatarajiwa kuudhuriwa na viongozi mbalimbali wa michezo nchini, Viongozi wa TBF walimu wa mpira wa kikapu,pamoja na walimu wa michezo katika Shule za Sekondari na wachezaji husika.
Ziara hiyo ya Hasheem Thabith na wachezaji ni mkakati katika kuelekea katika kukuza na kuibua vipaji vya mchezo wa mpira wa kikapu nchini ikiwa ni sehemu ya mambo ambayo Hasheem ameahidi kuendeleza nchini.
Pamoja na ziara hizo katika jiji la Dar es salaam Hasheem anatarajiwa kufanya Clinic mbalimbali kwa vijana chini ya miaka 15 katika baadhi ya Mikoa mara atakapo rejea tena nchini.
Michael Maluwe
Katibu Mkuu Msaidizi (TBF)

michuzi, mimi nipo ughaibuni kimasomo.ninafanya PhD katika masomo ya afya ya jamii. kila nikisoma blog yaKO naona watu wanajitokeza kuhamasisha jamii kwa kile walichokipata ughaibuni. mimi nimepata mengi, je nawezaje kuhamasisha jamii ya watanzania ktk maswala ya afya pindi ninaporudi huko vakesheni? nijibu
ReplyDeleteChris Bosh alikuwa Staples Center akiangalia waliofuzu na kuingia playoffs wanavyoumana, Hasheem yuko Temeke Uwanja wa Taifa. Ni vizuri, lakini...Ngoja ifike Novemba 2010!!
ReplyDeleteHuku marekani watu ukiwaambia kuna mbongo mwenzangu anachezea NBA huwa wanauliza Hashim who?? Hakuna anaemjua, ila ningekuwa mie ningejijenga kwanza kabla ya kuanza kujionyesha. Eti navyosikia ana mabodyguard na hasemi tena kiswahili hahaha, hashim you are full of yourself.
ReplyDeleteyani katika watu waliobahatika hashim ni mmoja wapo. Mwenzetu kashatafuniwa ni anameza tu. Tatizo kubwa ambalo ni hiyo nyodo na kutokutaka kufanya juhudi kwenye mpira. Yaani ikiisha contract yake anaweza kuwa benchi sababu huku ulaya hakuna cheti kumpelekea bosi na tena ukiwa mweusi na sio mmarekani ndio kabisa unatengwa unaonekana kama wewe umetoka kwenye miti. Kama mnavyoona kwenye TV wanavyoonyesha, ikiwa kama ni wana promote tourism ni utaonyeshwa sehemu nzuri kibao, mlima kili, nk. lakini ikiwa ni wanataka msaada toka kwa wananchi basi wataonyesha vitu kama watoto wenye matumbo makubwa, kamasi zinawatoka na nzi kibao. sio kwamba namtakia baya ndugu yetu ila triki ni kwenda juu na kubaki juu, ila mwenzetu kashaanza kuteleza mara apelekwe mafunzo mara anarudishwa na kuwekwa benchi tu mmmmh hashim kaa jifikirie zaidi.
ReplyDeleteAdumu raisi wetu mpenzi Jakaya Kikwete, adumu.
Tatizo letu waafrica hapo Thabeet kesha ridhika na alichokipata, naona career yake inaishia taratibu hapa marekani kwa kweli nilitamani kumwona akicheza lakini siku timu yake ilipocheza nilichokisikia kwa commentator ni kwamba Thabeet imepelekwa D leage! sasa hivi yupo bongo anachukua likizo badala ya kujinoa kimazoezi na kurudi ulingoni, hakika ninaamini wahenga walisema "Ng'ombe wa masikini hazai na akizaa anazaa tasa" wadau ashakum sio matusi this guy is not serious of what is doing at all, what I can see ni kwamba aangalie forbes.com kisha ona athlets maarufu na kwa miaka mingi NBA sasa hivi ni broke completely pesa yote waliyolipwa kwenye career yao ya NBA kwishnet. Labda uamue kurudi bongo kimoja na hata bongo hela yote itaisha muda sio mrefu kwani hauingizi bali ni unafanya matumizi tu. Hata ushauri unaotaka kuwapa vijana wadogo ni wa aina gani because you are not working hard enough, ukifanya mchezo this is your last contract my brother. You need to get serious with your career huu sio wakati wa kufanya ubishoo ni age ya kuchacharika na kutengeneza hiyo pesa kabla hauja expire!
ReplyDeleteNi ushauri tu you may take or leave it!
Mdau wa damu USA
inatia faraja sana kuona kijana wa kitanzania mwenye mafanikio ughaibuni, lakini bado anakumbuka kuinua vipaji vya wanafunzi nyumbani. huo ndio moyo utakaoendeleza nchi yetu.
ReplyDelete