Marehemu Seif Djibout
Umati mkubwa wa Watanzania katika mazishi ya marehemu Seif Djibout
Waombolezaji mazishini
Baadhi ya waombolezaji

IDADI KUBWA YA WATANZANIA TULIHUDHURIA KUMZIKA MWENZETU KATIKA MAKABURI YA NIKEA PIRAEUS J'NNE 04/05/2010.TULIMSWALIA KATIKA MSIKITI WA ELSALAAM ULIOPO ATHENS.
M/MUNGU AMLAZE MAHALA PEMA PEPONI AMEN.
INNA LILLAH WAINNA ILAIH RAAJIUUN,
MDAU UGIRIKI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 05, 2010

    marehemu akuacha watoto ama MALI ???

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 05, 2010

    Inna lillah wainna illah raajiun...very sad, natamani kweli ndugu wa kijana mwenzetu wapatikane walao wajulishwe habari za msiba...kama kuna aliyewapata atujulishe roho zitulie.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 05, 2010

    Poleni sana wadau Ugiriki....Guys, kuna ndugu zetu wengi sana waliondoka miaka ya 70 na 80 wakipitia Somalia na Djibout, hatujui habari zao...kama kuna waliofariki enzi hizo tunaomba mtuwekee majina yao, maana enzi zile kulikuwa hakuna emails, blogs etc, ni simu za landlines, call boxes na barua tu....Kama kuna mnaowajua walifariki na mnahisi ndugu hawakujua tunaomba majina...ntashukuru sana nikipata habari za mtu nnayemfahamu na sina mawasiliano naye

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 05, 2010

    Nawapa pole watanzania mnaoishi ugiriki kwa msiba huo. mungu ailaze pema roho ya marehemu.
    Hivi mlishindwa kabisa kumpata ndugu yake ili azikwe uku? hata hivyo nawapongeza sana kwa kujaliana. kumbe watanzania mko wengi kweli uko ugiriki, inaonekana ni nchi nzuri isiyo na masheria ya ajabu kwa wageni!!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 05, 2010

    Inauma , inasikitisha ila ndio Amri Udongo alioandikiwa Marehemu kuzikiwa ndio huo.Wengi waishio Ughaibuni hujiandika majina sio yao na hujulikana kwa wenzi wao kwa majina yaso kamili.Je haikuwezekana hata kupitisha habari hizi kwenye magazeti ya Kibongo?au Runinga za Kibongo au hata Radio?Zama zile Radio ilikuwa moja na habari zilisambaa hata vijijini, leo utandawazi namna hii hakuna hata mawasiliano na jamaa zake?Ilifahamika jamaa ni mwenyeji wa kusini na alitokea Keko, hakukuwa na mtu hata wa kubandika picha hizi katika maeneo hayo?Kweli Bongo tambarare!!Tumezidi Ubinafsi na choyo na kulaumu!
    Mdau Ughaibuni

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 05, 2010

    oooh mbona mikono mifukoni tena kwenye mazishi? hawa watakuwa ni wazenj tu!mpaka uwe na rangi kidogo ndio wanakua mstari wa mbele!mungu amsamehe madhambi yake marehemu-amen

    ReplyDelete
  7. Seif N'djamenaMay 05, 2010

    Ndugu Seif Djibout kuzikwa Ugiriki,kama Muislamu wametekeleza Sunna ya Mtume. Katika Uislamu imesisitizwa kuwa ni vyema mtu akazikwa alipofia. Yaani si vyema kusafirisha maiti kwenda kuzikwa mbaali sana na mtu alipofia. Nilipoona picha ya makaburini nikashindwa kuamini kama umati muhamad huo uko huko Ugiriki, yaani ni kama vile Kinondoni makaburini. Mungu adumishe umoja wenu.

    Hakika Mwenyezi Mungu kwake yeye tutarejea. Amin.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 05, 2010

    Inasikitisha sana kwa msiba na inaleta moyo kuona kuwa safari ya mwisho ya Djibout hakuwa peke yake. Greece poleni sana na mwendelee kuwa pamoja. chi zingine tuige mifano hii.Juu ya kutopatikana ndugu: Sie wenyewe tunaamua kukata bogi na kutowasiliana na ndugu zetu bongo. Sababu tofauti, ila majirani hawawezi kumlazimisha mtu ajieleze kijumla, pia hakuna anayetabiri kifo, wote tunategemea tutaishi miaka mingi ijayo.

    Jameni (hasa anony wa 10:51) Kama hatuna la kusema tukae kimya. Chukua Big G tafuna kuliko kutoa "fyongo" Hivi unajua maana ya LOL? Hivi LOL inaunganaje na mazishi and/or matatizo ya uchumi Greese? Nyerere aliwaambia watu walio LOL " mnacheka, mtakufa njaa..."Blackmpingo

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 05, 2010

    Poleni ndugu jamaa na marafiki
    Ankal najua upo bize na WEF, but fanya fanya hii picha na habariza msiba zitokee magazetini, especially magazeti ya udaku coz ndo yanasomeka sana maeneo hayo ya Dar

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 05, 2010

    Ndo matatizo ya kudandia meli na kwenda nchi za watu wakati huna lolote unaandikia mkono wa kishoto ndo haya.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 05, 2010

    Tunajua kuwa kuna wajinga kama wewe....lakini sio lazima kila mtu ajue kuwa wewe ni mjinga....unaweza ukakaa kimya kuficha aibu yako
    Watu wanazungumzia jambo la muhimu wewe ulicho ona ni huyo mtu aliye tia mikono mifukoni tu.....na hapo hapo akawa mzenji....kazi bado tunayo..

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 05, 2010

    Jamani nikitizama sura za hao wazee wanaonenakana ni watu walioenda huko miaka mingi iliyopita. Hivi wamewahi kurudi Tz hawa? Yaani au ndio majina yao na wao yatakuwa Ali Mpemba. Jamani rudini nyumbani siku hizi kuzuri huku

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 05, 2010

    hata ukizikiwa kwenu huwezi fufuka kamwe zaidi hapa kwetu hata hayo makaburi hatuyajali ndo kwanza watu wanafanyia ufirauni wao huko pachafuuu wakati hizo ndio nyumba za milele za wapendwa wetu na sie tuliobaki mie naona ni poa saana tu alivyozikwa huko kwani ishu ni nini? watu kibao wanazikwa nje hata wazungu nao wanazikwa bongo sioni tatizo bora mtu apumzike kwa amani mbona balali aligoma kuzikwa bongo ilhali ana ndugu zake kibao?? hakuna tofauti ukifa ukizikwa popote ni sawa sio ishu

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 05, 2010

    Wanaugiriki poleni kwa Msiba na hongereni kwa ushiriano wenu mlioonyesha.

    Binafsi ningeshukuru kueleweshwa japo kwa kifupi vyanzo vya vifo vya huyu Bwana Seif na yule rafiki yake (Mwenyezi Mungu awapumzishe kwa amani). Autopsy reports zinasemaje? Walipata ugonjwa wa mlipuko, walipigina, au walipatwa na maswahibu gani? Au ilitokea tu kuwa marafiki hawa walikufa kwa kufuatana?

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 05, 2010

    natanguliza kutoa mkono wa pole kwa jamaa wote hapo kwa mmanga"ugiriki" kama tulivyokuwa tunakuita miaka hiyo kwa kumzika huyu mwenzetu alietangulia katika haki.
    mimi binafsi nimefuatilia kwa karibu sana msiba huu na bado nina masikitiko kwa kutopatikana kwa wazee,ndugu au jamaa wa marehemu ili na wao wakapata wasaa wa kumtilia ubani.
    mimi binafsi nimekaa djibouti kiasi cha wiki mbili nikiwa njiani kuelekea kwa mmanga "greece" transit kwa firauni misri ambako nilikutana na vijana wengi sana kama hamis msago wa morogoro,mohamed manara wa dar mdogo wake sunday manara marehemu dimka wa dar pamoja na marehemu charles alberto wa zenj na charles borniface wa dar wengi mnawajua wanakandanda hawa maisha ni tambara bovu kuhangaika ndio wajibu na wakati ukifika wa kurudi kwa muumba basi tena hamna kuaga mungu atujaalie subira na kutupa barka zake katika kutafuta haya maisha.
    nakumbuka katika miaka hiyo tulimzika"gramatikoo" hapo piraeus{pirea}greece ambae alikuwa mwenyeji wa dar na rafiki yangu mkubwa,pia kwa firauni tulimzika marehemu sahib aziz kutoka zanzibar aliyefariki kwa ajali baada ya kuanguka kutoka ghorofa ya tano kwa bahati mbaya wakati wakikumbatiana na rafiki yake kwa furaha ya kuonana kwa mara ya kwanza kwani malik ndio kwanza alikuwa anafika misri akitokea sudan kwa rehema za mungu malik alipona baada ya kukaa hospital zaidi ya miezi mitatu na hivi sasa anaishi england na familia yake na sahib alifariki usiku ule ule.
    hii ndio mitihani ya subhana wa taala.
    kwa udongo tumekuja na kwa udongo tutakitoa.
    maasalaam.
    ex-baharia.{greece}
    ex-mbeba box.{djobouti}
    ex-mbeba zege.{egypt}
    ex-mbeba fagio{sweden}
    sasa nimehamia kwa obama.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 05, 2010

    mwenyeezi mungu aiweke salaama roho ya baharia seif na nawapongeza watanzania kwa kuonyesha upendo kuanzia mwanzo mpkaka mwisho wa msiba ebwana ex baharia uliekaa misri umenigusa sana kwani miaka hiyo ni 84/85 nami nilikuwa mitaa hiyohiyo ya suleiman goa na sharia ramadhan kwakina kida wala kida dunia si kitu nilikuwa sifahamu kama dimka amefariki na mohamed manara tulikuwa nae syria gheto moja umenikumbusha mbali masalaam iwish ningelipata jina lako nami nipo hapa kwa obama juma kisra

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 05, 2010

    duuh kweli maisha ni safari ndefu ex-baharia kweli umeona mengi pole sana yote maisha

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 05, 2010

    Kwanza pole kwa wafiwa na Mola inshallah amuweke pema peponi marehemu. pili shukurani ziwafikie wabongo wote wa ugiriki kwa kumpumzisha mwenzenu katika safari yake ya mwisho ambayo mwanadamu inabidi aipitie . mola ndie atakaye kulipieni kila yaliyo mema . kwa kuchangia tu nilikuwa napenda kumsaidia mdau ex mbeba zege ex baharia anon wa may5 06-59pm kuwa wakati yupo egypt aliyekuwa nae si Charles Boniface ni Charles Kilinda na hiyo ilikuwa milango ya 82-83 na kuhusu Dimka walikuwa wawili mmoja wa K/nyama ambae ndie aliyefariki na mwengine wa Kariakoo ambae yuhai. mdau ex baharia 80s

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 06, 2010

    asante sana mdau kwa kuniwekea sawa kuhusu yule mwanasoka aliyekuwa na hayati charles alberto,ni sawa alikuwa charles kilinda samahani sana kwani miaka mingi na jina lake la pili nilikuwa na mashaka nalo nimefarijika kwa kunisawazisha kwani nina hamu sana ya kukutana na charles kilinda na nilikuwa nyumbani miezi mitano iliyopita lakini sikuwa na uhakika na jina lake kamili.
    pia miaka ndio hiyo hiyo ya early 80s na pale "aguza' kwa kina kida wala kida na wale "mashaolin" wengine.
    maisha safari refu ndugu zanguni nimefarijika kuwasiliana na ex-wabeba zege wa egypt.
    "maelfu salama ya zulu"
    wakituita "ya zulu" wale warabu firauni maana yake "weusi"
    ahsanteni.

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 06, 2010

    salaam bwana JUMA KISRA,miaka zaidi ya ishirini imepita tangu tulipoyatembelea 'MAPYRAMID'nimefarijika kuona safari kwa upande wako haikuishia pale na hivi sasa uko mitaa hii ya obama,mimi kwa jina naitwa "jumapili"na wakati ule kama utakumbuka pale katika ubalozi wetu kulikuwa na luteni kanali ambae ndie alikuwa muambata wa kijeshi mimi ni kijana wake na mara nyingi nilikuwa na mohamed manara,kwa rehema za mwenyezi mungu mwaka 1991 mzee wangu alitangulia katika haki[died}at lugalo hospital wakati huo alikuwa brigedia general na akifanya kazi na major general mboma makao makuu ya jeshi daresalaam.
    namshukuru mdau alienikosoa yule charles wa pili ni charles kilinda nilimkuta alexandria wakati mmoja nilipoenda kuwajulia hali wabeba zege wa ukanda huo katika ghetto lao.
    ahsante.
    ex-sailor.

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 06, 2010

    WE Anon wa May 5, 11:42:00 a.m. na wote mliotoa maneno ya chuki na kejeli wakati wa msiba kama huu(1) mna chuki kali sana (you'll never be happy)(2) mna matatizo ya kisaikilojia , muoneni psychiatrist haraka sana na (3)nyinyi pia mtakufa na wakati wenu ukiwadia...ole wenu!!!!Tubuni, ungameni, tubuni!!! Poleni sana wafiwa na wadau wa Ugiriki.

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 06, 2010

    Dah, dunia ndogo...humu watu tunafahamiana ila tu ndo hivyo hatujui coz hatutaji majina...heshima yako Sunday...ntakutafuta offline

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 06, 2010

    Du miaka hiyo 'mabaharia' wengi waliondoka bongo.Kuna rafiki yetu tulisoma naye sekondari ya Kinondoni na alikuwa akiishi Magomeni kota kwa jina anaitwa Kubo, tangu aondoke hakuna mawasiliano yoyote na hata nguguze hawajui yuko wapi.Kama kuna wadau humu wana habari zake tunaomba tupashane. Kubo aliondoka mwaka 84 barua ya mwisho aliandika akiwa Canada mwaka 84..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...