Home
Unlabelled
hii imekaaje??
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Inaboa kwa kweli, labda TBS au wizara wana jibu sahihi. Cha ajabu hata ukitaka kununua jezi za timu zetu kubwa nchini unakuta lebo ya shirikisho la soka Afrika Kusini! Kamwe siwezi kuvaa jezi ya Yanga ambayo ina lebo ya shirikisho la soka la nchi nyingine, ni upuuzi wa hali ya juu na ni kudekeza uzembe wa watendaji husika! Kwangu mimi haina tofauti sana na kuvaa nguo za lebo ya Tommy Hilfiger, ni mara mia bora nivae iliyoandikwa Zana za Kilimo Mbeya (ZZK).
ReplyDeleteUnajua katika maisha lazima mtu awe na fikra ya kimaendeleo kila siku ya mungu.. Sasa mtanzania akishaona kitu kama hiki anafanyaje?? ANAANZA KULALAMIKA... Badala ya kuanza kulalalmika kwa nini tusifanye kitu kama hichi kuwa motisha kwetu na kutupa nguvu ya kutengeneza bidhaa zetu ili pia nchi za nje wapate bidhaa zinazosema "For Tanzania, By Tanzanians".. Halafu huyo jamaa wa juu hapo hataki watu wavae designer's clothes kabisa ama?? Basi hata magari ya nje tusitumie, tutembee kwa miguu, maana sina uhakika kama TZ inatengeneza baiskeli... Hii ni biashara ya kimataifa bwana.. Isingekuwepo biashara ya kimataifa nani atanunua mazao yetu? Wabongo kucha kulalamika tu, kama umepata bidhaa nzuri si utumie tu.. Shukuru mungu.. Wenzetu Zimbabwe hawana hata mikate..
ReplyDeleteHuyo jamaa wa kwanza hapo juu mimi nakubaliana nae kwa kiasi fulani. Tommy Hilfiger alisema hataki label yake ivaliwe na watu weusi. Nadhani ndio sababu ya kuitaja hiyo label. Hata mimi huwa siivai, ila navaa za ma-designer wengine kama kawa.
ReplyDeletePia nadhani mdau aliyeleta mada amekerwa na "MADE FOR SOUTH AFRICA..." na sio "BY SOUTH AFRICANS"...sielewi ni kwa nini wana-export then, si wakae na bidhaa zao watumie wenyewe, ebo!
Sijaelewa kabisa huyu jamaa sasa analalamika nini hapo. Tena mimi naona inabidi awapongeze ilo duka kwa kumletea kitu quality mpaka jicho lake likapenda akanunua. Nchi yenyewe tumeshaua viwanda vyoote sasa ni soko tuu la China na South Africa. Nenda nyerere Road leo uone, zamani kulikuwa na msululu wa viwanda lakini leo hii ni show room za magari na furniture tuu barabara nzima!! Wewe ilalamikie serikali yako kwa kutosisitiza wawekezaji wa viwanda waje badala yake tunaagiza mpaka sindano na nyembe..
ReplyDeleteWasauzi wana haki ya kuweka lebo yao kama sisi tunavyouza korosho kwao. Suruhisho ni kutengeneza vya kwetu badala ya kulalamikia vya wasauzi.
Sasa tatizo liko wapi? Wao hawajasema iuzwe South Africa tu, bali imetengenezwa na Wa-Afrika Kusini kwa ajili ya Afrika Kusini. sasa hapa Bongo pia wapo Wa-Afrika Kusini watanunua wataenda kwao kutumia. Kumbukeni pia ubalozi wao ni Nchi yaohivyo wanaweza pia kutumia wakiwa humo. Pia yawezekana wana nia nzuri ya kuwasaidia labda mazingira yane ya livyo machafu, tope jingi, vumbi hivyo hayafai kutumika huku kwenu waacheni wauziane wao wenyewe.
ReplyDeleteJamani hawa wamaopinga wanapinga 'MADE FOR SOUTH AFRICA'!!Hawapingi 'MADE BY SOUTH AFRICANs'!!Tusome vyema maoni ya wenzetu na kuwaelewa kabla hatujakashifiana wenyewe kwa wenyewe kwa ajili ya mataifa mengine!!Loo utafikiri duka moja huko S.Africa lingeandikwa 'MADE FOR TANZANIA', makaburu na wazawa wa S.A wasingeshangaa..Ovyoo...!
ReplyDeletenashukuru baadhi yenu kunielewa issue ni kuwa ile bidhaa haitufai huenda hao wa ubalozini wanaoishi hapa. Pack asali andika made for tanzania hata hapo kenya haipiti mpakani.
ReplyDeleteMdau unayesema Tommy Hilfiger alisema nguo zake zisivaliwe na watu weusi, hizo taarifa sio za kweli, Hata mimi nilikuwa napinga kuvaa hizo nguo kwa kuskia habari kutoka redio mbao... ushahidi kwamba hakusema hivyo ni huu hapa anahojiwa na Oprah http://www.youtube.com/watch?v=Nsp_XargGPQ
ReplyDeleteJamaa wameshindwa strategy ya kutafuta nguo zao zivaliwe wakaanza kutengeneza biff na madefigner wa kizungu.