JK akiwa na Mh. Klaus Schwab, mwasisi na mwenyekiti wa World Economic Forum wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 20 wa Uchumi wa Dunia kwa Afrika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar leo.
Na Salim said
RAIS Jakaya Kikwete amesema kuwa ni bora Tanzania kukosa mapato, kuliko kupoteza maisha ya maelfu ya Watanzania wanaokufa kwa ugonjwa wa malaria.

Rais Kikwete aliyasema hayo leo kwenye mkutano wa Uchumi Duniani (WEF), unaowakutanisha washiriki kutoka nchi 85 duniani ambapo pamoja na mambo mingine unajadili namna ya kunyanyua uchumi wa Bara la Afrika hasa baada ya kukumbwa na msukosuko wa uchumi duniani mwaka mmoja uliopita.

Hata hivyo, mkutano huo unakusudia kutoa changamoto na mapendekezo ya njia sahihi ya kupambana na kutokomeza kabisa ugonjwa huo namba moja kwa kusababisha vifo vya kina mama waja wazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano duniani.

Katika kipindi cha maswali na majibu ya papo kwa hapo baina ya washiriki wa mkutano huo, Rais Kikwete alieleza mikakati mbalimbali ya kutokomeza malaria nchini.

Moja ya mikakati hiyo ni kwa serikali kuzifutia ushuru bidhaa zote zinazohusiana na matibabu pamoja na mapambano dhidi ya malaria kuingia nchini, jambo ambalo baadhi ya Watanzania wanadhani huenda likaathiri pato la taifa.

Lakini Rais Kikwete akionekana mwenye furaha baada ya Tanzania kumwagiwa sifa katika mkutano huo kutokana na juhudi zake za kupambana na malaria.

“Lakini kama kuna maelefu ya Watanzania wanapoteza maisha kwa sababu ya malaria na tunaweza kuyaokoa basi ni afadhali tukose mapato, lakini tuokoe maisha ya Watanzania,”alisema Rais Kikwete.

Alisema licha ya mapambano dhidi ya malaria kuanza kwa muda mrefu nchini, lakini serikali yake inaona ndio kwanza yanaanza kutokana na umuhimu na haja kubwa iliyopo ya kutokomeza ugonjwa huo na hatimaye kuokoa maisha ya nguvu kazi ya Watanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 05, 2010

    Na hicho ndicho kilichobakia, kutafakari na kutafuta namna za kukuza uchumi wetu Watanzania na wa nchi nyingine ambazo lengo lake kuu ni kukuza uchumi! Tupo pamoja na Rais wetu katika jitihada zake hizo.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 05, 2010

    Jitihada zinazofanywa na Rais wetu wa Tanzania katika kukuza uchumi zinahitaji pongezi! Hoja zinazozungumzwa ni za msingi?

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 06, 2010

    Watu wanaokufa kwa ajali za barabarani je? Hiyo sio issue???

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 06, 2010

    vyandurua havitibu malaria, mr president think more that. waingereza walipokuwa wanaangamizwa na kipindupindu miaka ya 1800s, waliamua kujenga miondo mbinu wakaangamiza ugonjwa huo. tunatakiwa tuangalie zaidi ya upeo wa kuomba vyandarua, malaria iko uani kwa watanzania. tunaonekana nchi nzima ni bunch of nuckle heads...tunahangaika na malaria 45yrs now. some how ni shame. maadam unanerve ya kuomba misaada waambie hao wazungu wakusadie kujenga city plan.

    ReplyDelete
  5. Hivi wale wanaomkandia JK hawaoni efforts zake hizi? JK kujielekeza kupambana na Malaria ili kuitokomeza kabisa itakuwa ni mafanikio babu kubwa. Pia juhudi kwenye kukifanya kilimo chetu kuwa cha kisasa maana yake ni kuwa asilimia 80 ya Watanzania maisha yao yataboreshwa. Hiyo ndiyo maisha bora kwa kila Mtanzania. No Malaria, No Hunger, Food surplus ya kuuza domestically nad for export. Sasa nyie akina Lipumba na wenzio ambao priorities zenu ziko ndivyo sivyo mnataka JK naye aungane na nyinyi? HONGERA MHESHIMIWA RAIS. We support u sir

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 06, 2010

    Sawa. Lakini kasahau kitu kimoja katika mambo yanayokwamisha uchumi wa Afrika, UONGOZI MBOVU KATIKA NCHI NYINGI ZA AFRIKA. Wasomi kibao walishakimbia nchi zao na wanazalisha huko kulikoendelea. Watu walioko kwenye nyadhifa hutumia vibaya kile kidogo tulicho nacho, ni aibu kwa bara zima.

    ReplyDelete
  7. PETER NALITOLELAMay 06, 2010

    CRYING HISELF IS NOT IMPOSSIBLE IT SHALL NEED INFORMATION WHAT TO COMBAT MARALIA AND AIDS BUT HER EXCELLENTS JAKAYA KIKWETE HIS HIGHNESS PLEASE TELLS THE WORLDS WE ARE DYING ALL OF US SIMPLY BECAUSE NO MEDICINES AND KNOWLEDGE TO AVOID THE DIESEASE OF AIDS AND MARALIA IN THE OTHER HANDS. IF I WILL TELL THE MEETINGS OF READERS I SAID MARALIA IS PERSPECTIVELY DANGER AND AIDS DANGEROUSLY RESPECTIVELY BUT NOW WHAT SHOULD WE DOING THAT IS ANSWER TO GENARATION TO COME VERY TERRIBLE STAFF SO MR PRESIDENT TELL THE SOCIETY AND WORLDS THAT WE A DYING HERE HERE OPENLY NO ASSISTANCE FROM WOLRDS LEADERS OF TOMMOROW AND FUTURE ECONOMY TOO IN JEOPARDY HE KNOW WHAT I AM SAYINGS?

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 06, 2010

    World Economic Forum,
    OOOh yeah. nampongeza Mheshimiwa Rais kwa kufanikisha mkutano huu katika Tanzania kwa mara ya kwanza. Ni vyema ikafahamika pia vyandarua havimalizi malaria. Vinawazuia kwa muda tu wananchi wasiumwe na mbu. solution ni kumaliza mbu kama huko zanzibar walivyofanikiwa.
    Pili kuna magonjwa mengi bado ni tatizo,TB, Ukimwi nk.
    Tatu Mheshimiwa maendeleo ya kiuchumi hayaji kwa maneno tuu. Kuna mambo unahitaji kuyafanyia kazi ili kujenga uchumi Imara na maendeleo (1) kuongeza wigo wa kukusasnya mapato ambayo yameshuka san(2)kujenga nidhamu ya matumizi ya fedha za umma ndani na nje ya serikali-Ofisi yako mwenyewe iwe mfano kwa kuepusha safari zenye misafara mingi isiyo na tija(3)jenga miundombinu bora kwa kutumia rasilimali za ndani-wahisani hawatakuletea maendeleo ya kweli kama wewe mwenyewe hauna jitihada, (4) thamini nguvukazi uliyonayo nchini-wafanyakazi, wakulima, wafanyabiashara na wataalamu wanaokimbia nchi nk.nk na mwisho(5) weka siasa pembeni-na maendeleo mbele...
    Mr. President ni haya tu ndoi yataleta maendeleo kwa TZ yetu,...hatuwezi kukusifia kinafiki ilihali tukijua nchi imekaa kushoto

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...