Augustine Kakubukubu Kakorozya
1941-2009


Ni mwaka Mmoja tangu ututoke Mpendwa baba yetu Mzee Augustine Kakubukubu Kakorozya. Haikuwa rahisi kupokea machungu ya kukukosa wewe kwenye maisha yetu hasa kwa sababu ulikuwa chanzo cha vicheko katika kufurahia maisha yetu, lakini kwa baraka zake muumba, tunaamini uko katika pumziko la milele. Tunakushukuru kwa kutuleta duniani na kutufundisha, upendo, ukarimu, ucheshi, na kumpenda Mungu.

Ingawa hauko nasi kimwili lakini kiroho uko pamoja nasi na utaendelea kuwaka kama nuru katika miyoyo yetu, kwakua bado tunayaona matendo yako katika maisha yetu. Ubunifu wako wa kazi za mikono, akili yako ya udadisi, ucheshi, uadilifu wako, na bidii katika kazi vinaonekana wazi kurithishwa katika maisha ya watoto na wajukuu wako. ASANTE SANA BABA.

Unakumbukwa na Mama Angelina, Kaka yako Marcel Kasigara na familia yake, watoto wako (Adeodatus, Advocatus, Angelo, Simon, Getrude, Bennet, Sophia, Adelina, Ivan na Deus), wakwe zako (Sophia, Patricia na Glory) na wajukuu zako Augustine Junior, Kevin, Caren, Waren, Telvin, Maengela, Valangel Bernice, Gavin, Jocelyne na Sarah-Kathy, Wazazi wenzako na famila zao, Majirani zako Mbeya na Mwanza na marafiki zako.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.

MISA YA KUMUOMBEA MZEE KAKOROZYA ITAFANYIKA, JUMATANO 5/5/10, JUMAMOSI 8/5/10 SAA 12.00 ASUBUHI NA MISA YA KWANZA SIKU YA JUMAPILI SAA 1.00 ASUBUHI, KATIKA KANISA LA KATOLIKI, SINZA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 05, 2010

    Kwa kweli tunamkumbuka sana mzee kakolozya alikua ni mtu mwenye ushirikiano sana hasa katika kijiji chetu cha sae,sisi tulimpenda lakini mwenye enzi alimpenda zaidi.Amen

    Mwana Kijiji Sae Mbeya

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 05, 2010

    Mungu ailaze roho ya mzee kakolozya mahali pema peponi ila nasikikitika mmesahau kumuorodhesha mjukuu mwingine mtoto wa Marehemu Adeodata anaitwa daniel hilo ni angalizo next time mjitahid kuwakumbuka ndugu wa karibu na familia hiyo
    mungu alilaze roho ya marehem pema peponi
    ameni

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 05, 2010

    Poleni sana!

    Kakubukubu Kakorozya ameondoka!

    Lakini mliobakia Mungu awatie nguvu:

    Angelina, Marcel, Adeodatus, Advocatus, Angelo, Simon, Getrude, Bennet, Sophia, Adelina, Ivan, Deus, Sophia, Patricia, Glory, Augustine Junior, Kevin, Caren, Waren, Telvin, Valangel Bernice, Gavin, Jocelyne na Sarah-Kathy!

    ReplyDelete
  4. albert & ireneMay 06, 2010

    TAZAMA ILIVYO VYEMA NDUGU WAKIISHI/KUKAA PAMOJA KWA UPENDO.
    MWENYEZI MUNGU AWATIE NGUVU, AWACHIKE NA KUWALINDA NA AWAONGOZE KATIKA SIKU HII KUU YA KUKUMBUKA MPENDWA MZEE WETU aka MZEE KAKO.
    BWANA AMETOA NA PIA AMETWAA JINA LAKE LIBARIKIWE.
    TUPO PAMOJA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...