Video ya kuwasili kwa mpiganaji Athumani Hamisi toka Sauzi wikiendi hii
Wapiganaji wakisubiri Athumani Hamisi atue
Ankal akiwa na wapiganaji waandamizi. Toka kulia ni Mwenyekiti wa chama cha wapiga picha za habari Mwanzo Millinga, akifuatiwa na Mweka Hazina wake Leah Samike na mwenye maua ni Bi. Mwanakombo Jumaa ambaye ni mpigapicha mwandamizi MAELEZO
Kwa taswira za awali
Kuona Video hiyo na nyingine kibao



Pole sana kaka yetu hamisi.... usikate tamaa na maisha ma researchers wanatafuta kila mbinu kutafuta dawa ya kuwatibu watu waliokuwa katika hali kama yako. Usikate tamaa.
ReplyDeleteHang in there bro, we love you.
Na waliokuja kumpokea wazidi kumpa moyo pia sio tu watokee sababu ya kuwa inquisitive halafu hao hawasikiki tena wala hawaonekani. Hivi ni vitu vitamfanya mgonjwa aumie zaidi. Tushirikiane pamoja kumpa moyo ndugu yetu.
ReplyDeleteBaada ya video hii je mchumba wake kashapatikana au ndio kaishia na yeye?
Je vipi habari za Frano Mtui? kuna yoyote anaejua au kutupa namba yake tumpe moyo? si kwa ubaya ila tulicheza wote saa tuko wadogo.
ReplyDeletenimefurahi kuona anaweza kuinua mikono hiyo itazidi kumpa moyo, ila watu walimzinga sana wangempa nafasi hata angeweza kusema "Habari" ila pale alivyoingia tu wangempigia vigelegele kwa wingi na kungekuwa na watu wangeshika mabango yenye jina lake na kumkaribisha. Picha na video imesaidia sie wa mbali kumwona ila na yeye angefurahi zaidi kama watu wangekuja kumpokea kwa furaha zaidi.
ReplyDeleteThanks michuzi, please keep us updated.
mdau massachussets
hiyo wheelchair itachukua luku yote hapa mwenzetu lazima anatuhitaji kwa hali na mali. na tena hivyo kama hajaoa ndio itamchanganya zaidi.
ReplyDeletelakini naona improvement kubwa sio kama jana zile picha zilinisikitisha zaidi ila leo naona anageuka na kutumia mikono licha ya kwamba ni taratibu.
ama kweli binadamu sisi si kitu, kaka ameniliza mno huyu ila tuzidi tu kumbuombea kwa Mungu aweze kufanya miujiza kwani najua Mungu anaweza kufanya maajabu
ReplyDeleteKWANZA KABISA NAMPA POLE SANA NDUGU YETU HAMISI KWA YALIYOMFIKA
ReplyDeletePILI NAWAPA PONGEZI SANA WANAJAMII WALIOFIKA KWA MOYO WA UPENDO NA HURUMA KUMPOKEA NDUGU YETU
TATU NAMUOMBEA MAISHA MAZURI NA MAFANIKIO MEMA KATIKA MAISHA YAKE
NNE NAPENDA KUWAOMBA WAHUSIKA WAKUU WAJITAHIDI KATIKA KUPAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI
TANO NI KUHUSU HICHO KIJIJI CHETU CHA BAGAMOYO KWA KWELI INASIKITISHA SANA KUONA EAPOTI YA HAPO BAGAMOYO HATA TAA HAZITOSHELEZI KABISA YANI KIZA UTASEMA KIJIJINI
NA IMENISIKITISHA ZAIDI KUONA HATA GARI LA KUBEBEA WAGONJWA HALINA VIFAA MAALUM VYA KUPANDISHIA BASKELI ZA WAGONJWA YANI MPAKA WABEBWE
HUKU UGHAIBUNI HATA TAXI TU ZA KUBEBA WAZEE NA VILEMA AMBAO WANATUMIA BASKELI AU VIGARI KAMA HICHO HAPO ZINAKUWA NA LIFT SPECIAL YA KUPANDISHIA MPAKA NDANI BILA HATA KUSHIKWA SEHEMU
MWISHO NAMALIZIA KWA KUMSHUKURU ANKAL MICHUZI KWA JITIHADA ZAKE ZA KUTUFIKISHIA VIDEO HII NA TAARIFA MBALI MBALI
MUNGU IBARIKI NCHI YETU MUNGU WABARIKI WATU WA NCHI YETU NA WATOKOMEZE MAFISADI WA NCHI YETU.
ANKAL, HII VIDEO NDIYO UMEIREKODI NA FLIP CAMERA YAKO NINI????
ReplyDeletePongezi za kipekee kwa kampuni ambayo Athumani amekuwa akiitumikia kwa kutomtupa baada ya kupata ajali na, naamini, siku zote za maisha yake. Mmekuwa ni mfano mzuri na wa kuigwa, hongereni sana na Mungu awabariki.
ReplyDeletePia mshikamano na upendo wa wapiga picha kwa Athumani ni kitu cha kipekee na kizuri sana. Nimeguswa sana. Marehemu mzee wangu (R.I.P. baba yangu mpendwa) alikuwa na marafiki mia kidogo, na aliwajali na kuwapenda sana. Lakini alipopata tu ajali na kuugua kwa miaka mitatu kabla Mungu hajaamua kumuita tuliona marafiki zake wasiozidi wanne wakija kumjulia hali, tena ndani ya wiki mbili za mwanzo. Baada ya hapo walipotea. Ila mlichokifanya wapiga picha wa Tanzania kiwe mfano kwa jamii nzima, kumjulia hali Athumani mara kwa mara kutampa faraja sana, yeye pamoja na familia yake. Si vibaya mkienda mbali kidogo na kufikiria kuanzisha "Mfuko wa Athumani" ili muwe mnamuwezesha kidogo kidogo, kwani kutoweza kutoa mchango kwa familia yake kiuchumi kunaweza kumuathiri sana kisaikolojia. Mumlinde waungwana.
Pole sana Athumani, amini ni kazi ya Mungu na usiache kumuomba awe upande wako siku zote. Karibu sana nyumbani na ugua pole!
Jamani ee, kuuliza si ujinga...hivi Athumani ni BOXER, MPIGAPICHA ama MWANDISHI?. Naona neno la MPIGANAJI au WAPIGANAJI limetumika katika habari iliyopita pia kumhusu huyu ndugu yetu Athumani.
ReplyDeleteWengine hizi lugha zinatuchanganya, tunapenda habari...na tunafatilia lakini swali langu ni: Kuna ubaya gani kuandika kiswahili cha kueleweka na kila mtu?.
Hao "Wapiganaji" kwenye picha wakimsubiri Athumani hawaoneshi kama wapiganaji.
This is to you Michuzi: Blog yako inasomwa ulimwengu mzima, na watanzania pamoja na wengi wanaozungumza au kujifunza lugha ya kiswahili. Inapotumika slang ya Bongo....sisi wengine tusioishi Bongo tunapata shida kidogo kupata ujumbe sahihi na uliokusudiwa.
Silaumu, natoa mtizamo wangu tu...kwani mawasiliano yana maana gani kama mlengwa hapati ujumbe uliokusudiwa?.