mshambuliaji machachari wa timu Lindi,Ally Mohamed akimtoka beki wa timu ya Ilala,Ahmad Mkweche katika mchezo uliopigwa leo katika uwanja wa Uhuru jijini Dar.Lindi imeshida 3 - 0 dhidi ya Ilala.
Beki wa timu ya Lindi,Mohamed Salum akiondoa hatari iliyokuwa inaelekea langoni kwake mbele mchezaji wa timu ya Ilala,Ahmad Mkweche.Lindi imeshinda kwa kishindo kikubwa kwa idadi ya mabao 3 - 0 dhidi ya timu ya Ilala.
mchezaji wa timu ya Lindi Justin Philipo akitaka kumtoka kiungo wa timu ya Ilala,Hassan Peshco katika mchezo uliochezwa leo uwanja wa Uhuru jijini Dar.
beki wa timu ya Ilala,George Minja akitaka kumtoka mshambuliaji wa timu ya Lindi katika mtanange uliopigwa leo katika uwanja wa Uhuru jiji Dar.
dua ikisomwa baada ya ushindi mnono kupatikana dhidi ya Ilala.
hivi ndivyo ubao wa matokeo unavyoonekana.
Julio akiwa na baadhi ya wachezaji wa timu ya Lindi mara baada ya mpira kumalizika na huku timu ya Lindi ikiondoka kifua mbele dhidi ya Ilala.
mashabiki wa timu ya Lindi wakishangilia ushindi wa timu yao uliopatikana leo katika uwanja wa uhuru jijini Dar.Lindi imeweza kusonga mbele kwa hatua ya fainali ambapo itakipiga na timu ya Singida siku ya jumapili katika uwanja huo huo wa Uhuru.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 27, 2010

    niko mbali na nyumbani kwa sasa ila kwa miaka miwili iliyopita tangu kwa hii michezo kurudi nilikuwa nachukia sana kuona kombe linabaki Dar nimefurahi vijana wa mikoani kwa mliyoyafanya safi sana hongera lindi na singida
    mdau
    Benin

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 28, 2010

    wera wera wamweraaaaaa oyeeeee ,lindi juuu juu zaidi baaaaaaa watajibebaaaa

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 28, 2010

    Hongera Lindi, Hongera Singida!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 28, 2010

    Nimeona mechi mbili za vijana wa Lindi ikiwa ni pamoja na hii ya Ilala, wanacheza vizuri mno. Swali langu ni, kwa jinsi ninavyoifahamu lindi na uchumi wake je vijana hawa wamechukuliwa kutoka mkoani Lindi au ni wa Dar wamepelekwa lindi kwa ajili ya kucheza tu? anayefahamu anisaidie!!

    ReplyDelete
  5. Patrick Tsere (DC wa zamani Ilala)May 28, 2010

    Natuma salamu zangu za dhati za pongezi kwa uongozi wa mkoa wa Lindi kwa ushindi wao dhidi ya Mkoa wa Ilala.Ninaamini mlistahili ushindi huo. Soka la Tanzania Oyee

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 28, 2010

    Aisee naona jana mtaa wa kongo na uhuru ulikuwa mweupe. wamachinga wote walikuwa uwanja wa uhuru,
    Mdau
    Kisiju pwani

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 28, 2010

    wewe anon wa Fri May 28, 08:48:00 AM wacha chochezi hizo! duh jamaa kwa nini unashindwa kuwapa hungera na badala yake unaanza kutaka kuleta uchafuzi wa mashindano yote kwa kuanzisha rumour zisizo kuwa na kichwa wala miguu?

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 28, 2010

    Anon wa tarehe 28 08:48:00 umasikini wa watu unahusiana nini na uchezaji mpira? Kama suala ni utajiri hivi hushangai timu za Amerika ya kusini zinavyowatoa jasho timu za Ulaya? Kama kushinda ni kutokana na utajiri kwenye michuano hiyo ungeona ni timu za Kilimanjaro na Arusha ndio zinashinda au timu ya Temeke maana ndio wilaya inayoongoza kwa utajiri ingawa watu wake masikini.

    Kisha umeshangaa vijana wa Lindi na Singida je wanautajiri gani? Na wao wametolewa kutoka Dar es Salaam pia? Tufike mahali tuache mawazo mgando, kama hauko exposed ni heri kukaa kimya. Hata hivyo Dar imejaa wakuja tele kutoka pembe mbali mbali za TZ si wazaramo peke yake.

    Hongera Lindi, Hongera Singida

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 28, 2010

    Napendekeza Kihwelo aachane na jina na utani la 'Julio' na aanze kujiita Jamhuri Kihwelo 'Mourinho'. Kila nikimsikia Kihwelo akizungumza hunikumbusha kocha wa Kireno mwenye makeke Jose Mourinho, ambaye hasiti kuzungumza kile kilicho moyoni mwake.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 28, 2010

    Nyie TFF kwanini mnafanya wilaya za Temeke, Ilala na Kinondoni kuwa Mikoa? Hebu irudisheni Mzizima tuone kama kombe litaondoka DAR, kama mnataka fair, basi wekeni haya mashindano yawe ya wilaya tu, Mwanza kwa mfano nao wangeleta Sengerema, Mbeya wangeleta Mbozi nk nk, acheni kuipendelea Dar es salaam nyinyi, haya mashindano yanaendeshwa kisiasa zaidi siku hizi, hamna lolote, ndio maana mmetolewa maana nyie wote ni Dar...TUPA KULE!!!!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 28, 2010

    BAAAAAAAAAAA NTU KWAO MWEEEE TUWAPE SIFA ZAO JAMAAAAAA, HIVI HUYU ANYESHANGA LINDI ANAJUWA HISTORIA YA SOKA YA TANZANIA AU ANABWEKA TU, NI MTOTO WA JUZI NINI, KAMA ANA KUMBUKUMBU NZURI NI MKOA KATI YA MIKOA ILIYOKUWA INTAMBA KATIKA SOKO MIAKA HIYO YA 60 HADO 80 MWANZONI ANAWAKUMBUKA AKINA MUHAJI MUKI, KABURU WALIKUJA HATA KUJA KUCHEZEA YANGA NI MKOA ULIOKUWA NA TIMU KALI TATU ZIKIITWA YANGA NA BAADAYE NCHI YETU, SIMBA NA BAADAYE NGUVU MOJA NA BEACH BOYS. WACHEZAJI WOTE WAZURI WA TIMU ZA MTWARA WALIKUWA WANATOKANA NA TIMU HIZI

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 28, 2010

    WADAU MIMI BADO SIELEWI KIGEZO KILICHOTUMIKA KATIKA MICHEZO HII MUHIMU YA MIKOA KWA KUPENDELEA MJI WA DAR. KWANINI MJI WA DAR ES SALAAM UPEWE NAFASI YA WILAYA ZOTE NNE KUWAKILISHA AU HIZO WILAYA SIMEKUWA MIKOA JAMANI. HAYA MAMBO YATAENDELEA MPAKA LINI. HUU NI MFANO MDOGO KABISA UNAONYESHA JINSI MIKOA MINGINE INAVYOTENGWA NA KUKOSA MAENDELEO. HAYA MAMBO JAMANI TUTAACHA YAENDELEE MPAKA LINI???MIMI NAOMBA WADAU TUCHANGIE MADA HII. MAANA TUMECHOKAAA.. HONGERA LINDI NA SINGIDA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...