Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akizungumza na Waandishi wa Habari leo baada ya kukagua maadalizi ya mapokezi ya wageni watakaoshiriki katika Mkutano wa siku tatu World Economic Forum unaotarajiwa kufanyika jijini Dar kuanzia May 5, 2010 kwenye ukumbi wa Mlimani City utakapofanyia mkutano huo. Kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Peniel Lymo na kushoto ni Mkurugenzi wa Afrika wa World Economic Forum, Catherine Tweedie.
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akikagua maandalizi ya mapokezi ya viongozi wakuu wa n chi mbalimbali na washiriki wa Mkutano wa World Economic Forum kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere leo. Mh. Pinda pia alikagua ukumbi wa Mlimani City utakapofanyika mkutano huo. Picha na Mdau Hilary Bujiku wa Ofisi ya Waziri Mkuu


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 02, 2010

    Mikutano kama hii imeleta mabadiliko gani kwa mtanzania wa kawaida? Si yale yale ya semina-elekezi za ngurudto! Poor Africa!!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 03, 2010

    tena jamani naona wazee wengi hapo sioni kama kuna lolote la maana litakuwa jadiliwa kwa maendeleo ya kijana wa kitanzania wamekaa hapo kusubiri posho tu. nahisi ulikuwa muda muafaka wa kuwaachia vijana waweze kuendesha huo mkutano wote na wao wakae wawe wanaangalia kwa kujivunia juu ya watotot wao.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 03, 2010

    annon #2 juu,unafikiri ilo wanalo akilini??wao wanawaza zao tu vijana wanawaona kama maadui zao-threat...
    maana ata me najiuliza ivi vijana tulivojaa bongo na brains zetu mbona logistics za mikutano kama izo ni mteremko tu?adi mataifa wangejivunia ujana wetu lakini ndo ivo...
    2.sasa Dar itakua kituko ilo FOLENI LAKE maana ratiba ya kusafirisha wageni ndo muda wa kwenda na kurudi kazini

    hahhaaaaa na mvua sasa!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 03, 2010

    tena ako kazungu coordinator utakuta katotoooo ila mibaba iyo inafata-fata nyuma tu na mikono nyuma na ---- meno yao!!

    utafikiri damu changa haipo,posho izi?!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 03, 2010

    GRIDLOCK!!!!!!!!!!!!!
    Ati these guys think that by closing 3 roads they can manage the chaos?I hope sasa wattaona uuhimu wa miundo mbinu na mipango mizuri ya jinsi ya ku control traffic. Muda si mrefu leo nimekaa dakika 20 kwenye taa za kijitonyama cos afande anaongoza magari wakati taa zinafanya kazi na yeye anasababisha foleni! we are beyond control!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 03, 2010

    sasa ndio tutaona pale mlimani city kama magari ya waheshimiwa yataguswa ndio ujue wale walinzi wa pale wanashirikiana na vibaka!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 03, 2010

    Anony namba 4. Inawezekana kuwa hako ni katoto lakini bado kakawa na uwezo mkubwa kuliko lundo la wazee wa kiswahili waliokaa pale Jiji wanakula posho.

    Hebu angalia hata vitu vidogo kama kupanda miti stahili ya barabara imebidi kaje katoto katuambie. Hao wazee waliopo pale Jiji miaka nenda rudi mimea waliyoona inafaa ni vile vimaua ka' yaliyopanda ubalozi wa taifa fulani kubwa pale Drive In. Kumbe kila mmea una mahali pake na yale maua hayafai kupandwa barabarani.

    Pabaya zaidi ni kwamba ile miti inahitaji matunzo makubwa sana kwa sababu yamekuwa transplanted yakiwa yamekomaa, na nakuhakikishia kuwa wazee wetu wa Jiji hawataweza kuyatunza pindi mkutano ukiisha.

    ReplyDelete
  8. ObserverMay 03, 2010

    I cant imagine kuwa huu mkutano ndio umefanya kodi zetu ziingie katika gharama kubwa ya kuhamisha miti mikubwa kama ile eti kisa kuna wageni. Yaani naamini gharama iliyotumika pale ni kubwa sana na ninawahakikishia hiyo miti yote itanyauka hata miezi minne haifiki. Akili gani ya kuhamisha miti mizee kabisa kisa ya ugeni wa siku zisizozidi tano ? Hao wageni watakaa hoteli zilizopo katikati ya jiji, kwani toka huko mpk mlimani City je kuna hiyo miti? Let think big Tanzanian. Michuzi hata ukinibania pouwa tu, msg delivered.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...