Marehemu Salim Issa Isihaka alizikwa jana jumatutu katika makaburi ya kiislam mjini Rome.Marehemu alifariki siku ya jumatano tarehe 5/5/2010 huko Napoli, baada ya kuumwa kwa muda mfupi.Msafara wa kwenda mazikoni ulioongozwa na Mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania Italia Mh.Abdulrahaman A.Alli pamoja viongozi wote wa jumuiya makao makuu na matawi yake yote. Ulianza saa kumi na mbili asubuhi kutoka Napoli kuelekea Rome kwa mazishi.Sala na dua kwa marehemu iliongozwa na sheikh Rajab Maulid kutoka jumuiya ya Watanzania tawi la Modena.Mazishi yalihudhuriwa pia na maofisa wa ubalozi wa Tanzania Rome Marehemu ameacha mke na watoto wawili. Mungu amlaze mahala pema. kwa picha zaidi :
Habari za awali


RIP,
ReplyDelete**** Hivi ndg zetu siku hizi mnazika ndani ya jeneza? au ndiyo mambo ya ulaya?
hivi ni kweli Saudia Arabia kuna makaburi ya wakristo?
ReplyDeleteKuuliza si ujinga, Michu usinibanie manake nishauliza maswali mengi unanichunia... hivi huyu Salim ni dini gani? Nauliza hivyo kwa sababu Waislam hawaziki ndani ya sanduku, hapo inakuwaje?
ReplyDeleteWallahi nimestuka mno kuona al marhoum Salim Issa Isihaka akitiwa ndani ya kaburi kwa sanduku. Sielewi waislamu wa Italia wana utaratibu upi tofauti na taratibu za kiislamu.
ReplyDeleteJe inaswihi?
Naomba maulamaa mnisaidie
RIP Bro Salim,
ReplyDeleteWaislam hawazikwi kwenye masanduku lakini haya tunaona ni mambo ya kiulaya, lakini mashehe wapo basi na watufahamishe vizuri maana elimu ni pana mno pengine sisi hatujui vyema. tunaomba kueleweshwa!
mimi ni muislam imeniuma sana kuona anazikwa katika sanduku, na hawa wazungu hizo gloves za nini ? atawaambukiza ugonjwa , yaani ndo maana sipapendi ulaya , bora wangeleta maiti yao tz ikazikwa kwa taratibu za kiislam ,poleni wafiwa
ReplyDeleteALLAH amsamehe madhambi yake na amrehemu,
amin
Jamani hata mimi nimeshangazwa kidogo! au mkiwa ulaya mwazikwa na jeneza? Au alibadili dini akabaki na jina tu? Michuzi samahani labda wamekosea picha ya kuweka
ReplyDeleteKUISHI KWINGI NI KUONA MENGI. WASALAAM
ReplyDelete(1)Kuna Waislamu wengi Ulaya wanazikwa katika masanduku. Cha muhimu ni kuwa (a) Lazima maiti aoshwe, (b) Asaliwe (c) Awe ndani ya sanda (d) Alazwe kuelekea kibla (e)Taratibu za dua zifuatwe. (2) Wewe anon wa 08:25:00, Ndiyo; Riyadh kuna makaburi ya Wakristo. Nilipokuwa mhandisi huko 1998 kuna Mkenya mkristo aliyekuwa fundi Saudia Airlines alimzika mtoto wake huko. Mecca na Madina hakuna makaburi ya watu wasio Waislamu kama vile VATICAN HAKUNA MAKABURI YA WAISLAMU. (3)NAMI NAOMBA NIULIZE:NIMEFUATILIA NA NAULIZA : kwa nini katika blogu hii karibu kila mara kukiwa na habari za msiba ya Mwislamu LAZIMA (99% of the time) watajitokeza watu kutukana, kukejeli na kubeza. Huo si uungwana. Kumbukeni: WHAT GOES AROUND COMES AROUND....... EDDY.
ReplyDeletemmh inashangaza!waislamu hatuziki ktk sanduku,inashangaza kuna watu wamevaa kanzu na kofia hapo wanajiita masheikh wameruhusu hilo!
ReplyDeletenduguze wanaweza kutusaidia ....
poleni wafiwa!
Nitajaribu kufafanua kuhusiana na Sanduku,
ReplyDeleteHuku Ulaya baadhi ya nchi, NI SHERIA KWAO LAZIMA KUZIKWA KWENYE SANDUKU, NA KAMA HUTOZIKA KWENYE SANDUKU NI KOSA LA JINAI, HATA HIVYO WANAJUMUIYA WA KIISLAM WANAJARIBU KADRI YA UWEZO WAO KUIONDOA HII SHERIA, NA MAFANIKIO HAYO YAMEWEZA KUJITOKEZA KWA NCHI KAMA UK, AMBAYO HIVI SASA WANARUHUSU BAADHI YA SEHEMU KUFANYA HIVYO...
Maulamaa watatusaidia katika hili, lakini kwa mtazamo wangu nafikiri alifanyiwa taratibu zote za maziko ya Kiislam na pengine amevalishwa na sanda na katika jeneza amelazwa ubavu mmoja na hilo jeneza limewekwa katika mwanandani na amezikwa kuelekea kibla. Jambo la muhimu hapa ni kuwa amesaliwa sala ya maiti na amezikwa, sababu hata mtu akifia katika meli huko deep sea (nilimsikia baharia mmoja akihojiwa katika TV) hata akiwa muislam maiti yake inazamishwa katika bahari ikiwa imefungwa vitu vizito isielee juu lakini baada ya kuombewa kama kuna waislamu wenzie. Jambo la muhimu tumuombee mola amsamehe madhambi yake.. Ameen
ReplyDeleteina illahi wa ina lilahi rajun.....
ReplyDeletebwana ametoa bwana ametwaa jina la bwana libarikiwe
Jamani msishangae kuwa na jina la Salim, wengi wa ndugu zetu hao walio majuu uislamu wao umebakia kwenye majina tu, wengine wana majina hayo lakini ni waumini wa upande wa pili na wamefanya hivyo bila hata ndugu na jamaa zao kujua.Binafsi nawafahamu wengi tu, wana majina ya kiislamu lakini imani na matendo yao ya kila siku hayaendani na uislamu.
ReplyDeleteJamani kwa uwelewa wangu wa kimazingira, na wala sio wa kidini, pale nje ya London tuliwahi kumzika kijana mwenzetu akiwa ndani ya sanduku, ni kwasababu hatukua na jinsi ndivyo hali ya ki Nchi ilivyo tulazimisha.
ReplyDeleteLakini kwa juhudi za viongozi wa waislam pamoja na jumuia yetu (ZAWA) walianza mkakati wa kufuatilia na kuomba kwa wahusika wanchi na hatimae tukaanza kuona matunda, kwani sehemu mbali mbali tulianza kuzikana bila ya Sanduku. Hivyo vijana wa kiislam wa Italy pamoja na jumuia zao, wanapaswa kufuatilia, pengine watafanikiwa kwa.
masikini muislam mwenzetu sijui kavalishwa na suti !!! yaani nawashangaa ndugu zake walokubali kufanya yote hayo , bora wangechoma moto mwili wake kuliko walivomfanyia ,jamani hebu tuelezeni inakuwaje iwe hivi ? bado sijaelewa au kabadili dini alivokuwa huko ulaya akaamua kubaki na jina lake la zamani ? nisaidieni
ReplyDeleteHi,
ReplyDeleteInawezekana jamaa alibadilisha dini (aliritadi). Vinginevyo kama ni muislam basi kunahitajika ufafanuzi maana yawezakuwa elimu ni pana kweli.
K.O.R.
Michuzi naomba unipe nafasi niwajibu ndugu waliouliza na kushituka kwa kuona ndugu yetu muislamu akizikwa ndani ya sanduku.
ReplyDeleteNaam ni sikitiko kubwa sana kuwa katika nchi zote za ulaya hakuna ruhusa ya kuzika bila ya sanduku. Waislamu wote wanaofariki ulaya na kuzikwa huku wote huzikwa namna hii. kwa hivyo wale waliouliza ni dini gani marehemu alikuwa akifata waondowe shaka yao.
Kusema kweli sheria hii eti nasikia ni kuepuka contamination ya ardhi, sijui kama ni kweli au la ila mimi siamini, kwani nimeshasikia kuwa jews hapa uk wana makaburi yao na wanazika bila ya sanduku.
mdau ulieuliza kama saudi arabia kuna makaburi ya wakristo i hope umeuliza kwa nia ya kuelimisshwa sio kutafuta ugomvi.
ReplyDeleteKwa kukujibu tu, nchi tele hutengenisha makaburi ya waumini wa dini mbali mbali, iwe europe, amerika na hata afrika, hili jambo sio la ajabu na wala halikuanza leo.
ndo mambo ya kiulaya hayo kwani hamjamuona na huyo demu kavaa ushungi mweupe kwani wanawake wa kiisilamu nao wanaendaga kuzika ? ndo majuu ukienda rome fanya kama waroma ni hayo tuu poleni wafiwa
ReplyDeleteHello, namuomba Mwenyezi Mungu aliye mkuu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Amen.(RIP)
ReplyDeleteNdugu zangu, mimi siyo muislam, kwa hiyo nitakayouliza hata kama yataonekana kuwa ya chekechekea saana naomba tuwiane radhi.
Kwa kuwa maherehu hana uwezo wa kuamua azikweje baada ya kufariki dunia, hasa kama amefarikia mbali sana kwao,baharini, angani, kwenye utamaduni na itikadi tofauti kidogo na ile ya kwake, ni kitu gani kinachomzuia marehemu huyo kwenda peponi kwa kuwa walimwengu wameamua kumzika walivyoona wao inafaa?
Mwenyezi mungu anaweza kumwadhibu huyu marehemu kwa sababu tu amezikwa kwenye sanduku? Kama hivyo sivyo, kuna manufaa kuwalaumu hao wazikaji?
Poleni sana waombolezaji, ijapokuwa sikumfahamu marehemu wala jamaa zake!!
Sharia za ulaya hazikubali binadamu azikwe mwili tu. Hata akina jumuiya ya Washia, hawaruhusiwi kujikata visu wakati wa Ashura kama wanavyofanya Iran, na Tanzania. Badala ya kufanya hivyo, wameambiwa kuwa damu ni kitu muhimu sana na wameombwa kupeleka damu Red Cross badala ya kumwaga barabarai na pia kusababisha magonjwa.
ReplyDeleteKama tunataka maisha kama ya wenzetu ulaya, inabidi tuache sheria zetu za kidini nyumbani au kama hatuwezi basi tuishi nchi za kiislamu.
Hii ndo mara yangu ya kwanza kuona muislamu akizikwa ndani ya jeneza.
ReplyDeleteR.I.P BRO
ReplyDeleteNAWASIKITIKIA SANA NINYI MNAOKAA KUJADILI KWANINI KAZIKWA NDANI YA JENEZA,KUFA NI KUFA UZIKWE KWENYE JENEZA,UFUKIWE BILA JENEZA,UZIKWE JENEZA LA MARUMARU AHERA NI AHERA,SO NAWASHAURI WANAOLALAMIKA MWENZAO NDO KESHAZIKWA NDANI YA JENEZA NA HUWEZI JUA LABDA ALITAMKA AKIFA AZIKWE NDANI YA JENEZA?KAZI KWAKO WEWE NA MIMI AMBAO HATUJUI TUKIFA TUTAZIKWAJE,TUTAFAKARI HILO!
ReplyDeleteNdugu Zangu Msihamanike sana katika hili hili ni jambo moja tu kati ya mambo mengi ambayo ndugu zetu wa kiislamu wanapatatabu nayo huku Ulaya, Sababu kubwa ya kuzikwa na sanduku ni sheria za nchi ya Italy ambazo haziruhusu maiti kugusa ardhi ndio maana mnaona wazungu pia wapo hapo, hiyo yote ni katika kuhakikisha kuwa hatolewi kwenye sanduku, kwa kweli uongozi wa jumuiya ya Watanzania Hapa Italy umejitahidi sana katika kuyafanya mazishi yaha yafanyike katika misingi ya kiislamu lakini kwa hili haikuwezekana. "kikubwa hapa kwetu tuliobaki Dunia nikujitahidi kuomba mabadiliko hayo kwa nchi husika, na kumtakia kheri marehemu mola amuondolee adhabu za kaburi na kumuweka mahala pema peponi. Amin"
ReplyDeleteMS (Napoli)
azikwe kwenye sanduku au bila sanduku
ReplyDeleteameshafariki mwenyezi mungu upokea wote wajao na sanduku au bila sanduku kwahiyo acheni upuzi wenu sanduku pale sanduku hapa akili zenu ndogo.
mwenyezi mung amlaze pema peponi. we subiri zamu yko maudongo yanakusubiri bila sanduku shukuru ukizikwa kwenye sanduku utajiju kazi kwako .
mdau ujerumani
nyie waislamu akili zenu ndogo sana
ReplyDeleteuzikwe kwenye sanduku au bila sanduku mwishowe unabkia mifupa hivyo hivyo nendeni shule kidogo. mwenyezi mungu amlaze pema peponi. wenzenu wamefiwa wanuchungu badala yakuwafariji mnaanza kuongea mambo ya sanduku haibu tupu IDIOT IDIOT mpka mwisho wenu
Poleni wafiwa.
ReplyDeleteKweli dunia ni pana, tembea uone. Globu ya Jamii inatufahamisha mengi.
"Ukienda China kutafuta 'ilim' basi usife njaa kwa kukataa kula vyakula ambavyo si halal''
Pia 'Ya Kaisari mpe na ya Mungu Mpe''
Tunamuombea marehemu apumzike pema peponi, amen.
ingekua kuna dini nyengine yoyote inapigwa vita duniani kote kama unavyopigwa vita uislam, dini hiyo isingebaki katika uso wa ardhi
ReplyDeleteUJINGA MTUPU, badala ya kujiuliza kama marehemu aliishi maisha ya kumpendeza Muumba wake tunapoteza muda kwenye jeneza! Imani nyingine, kaaaaazi kweli kweli!
ReplyDeleteAnony 12:01:00 PM, hasira za nini??
ReplyDeleteKama maiti anazikwa ulaya ni lazima sheria zote za maziko ya kiulaya zifatwe penda usipende!! Kama maiti anachomwa moto china ni lazima taratibu zote za kuchoma moto zifuatwe!!! Kama maiti anazikwa uarabuni huna budi kufuata sheria za kisumani!!
What is the difference!?? Hakuna tofauti hapa. Ni mtazamo tu. Kama ikikupendeza acha usumani wako na wewe anza kuzika kiluguru , kizigua, kwani wewe mwarabu??
kuongezea alicho kizumza ndugu yangu eddy....wakati mwengine muislam anaweza kuzikwa kwenye sandaku ikiwa ardhi ya eneo husika ni laini sana....lakini kinacho zikatiwa sana ni mambo manne kuoshwa,kuvishwa sanda,kuswaliwa na kuzikwa.....na kwenye kuzikwa anatakiwa kuzikwa kwenye ardhi na hakuna ardhi itakayo mkataa muisilsm au mkirsto...popote utakapo zikwa utafika mbele ya haki....halafu tuache ushabiki katika masuala ya dini....kwa hiyo kama saudia kusingekuwa na makabu ya wakristo ndio ingekuwaje?
ReplyDeleteKama watu hawapendi hii kitu mimi naona dawa ni kusafirisha tuu kuja nyumbani
ReplyDeleteTuna washukuru sana wa-Taliano kwa kuweka makaburi ya waislam- hili ni jambo la ustaalabu sana ukilinganisha na nchii nyingi za ki-arab ambazo ni wabaguzi wa dini kama nini.
ReplyDelete+
WEWE EDDY HAPO JUU ACHO HIZO HAKUNA MKRISTO ANAYE ZIKWA VATICAN WEWE. VATICAN NI MAKAO MAKUU YA DINI YA WAKATOLIKI. HATA WAKATOLIKI WA KITALIANO HAWAZIKWI VATICANI. HUU NI USTAARABU WA WATALIANO AMBAO HUWEZI KUUPATA KATIKA NCHI ZA KIARABU. NI-ELEWE HAPA SIJA TAJA UISLAM NIMESEMA NCHI ZA KIARABU. UISLAM NA UARABU NI VITU VIWILI TOFAUTI.
ReplyDeleteACHA GHAZABU WEWE. RUDI NYUMBANI TU.
i hope wale wote waliokejeli na kudai kuwa kuzika ndani ya sanduku ni mambo ya kiulaya kadhalika yule alifika hadi kumsingizia maiti kuwa yakuwa huenda ameritadi au yule alosema kuwa maiti imevishwa suti mtashika vichwa vyenu kwa aibu na kujuta kusema mliyoyasema bila ya kwanza kukaa na kutafakari.
ReplyDeleteYaani hamkukaa na kufikiri kwanza ni kiasi gani comments zenu zitakavyowaumiza wafiwa? hivi hamjawahi kufiliwa?
Waislamu wote (sio watanzania)nchi nyingi za ulaya hawana ruhusa kuzika bila ya sanduku. hizi ndio sheria za nchi zao, mgeni utafanya nini?
waislamu wote katika nchi nyingi za ulaya kwa miaka mingi wamekuwa wanafanya kampeni ya kuweza kuruhusiwa kuzika bila ya sanduku, kuna baadhi ya nchi zimekubali na nchi nyengine bado zinasisitiza kuzikwa ndani ya sanduku.
Kuna alietaka kujua maulmaa watasemaje juu ya hili na kama kuna fatwa. fatwa ilishapitishwa toka enzi na dahari kuwa kwa vile mola hakalifishi nafsi kwa jambo usiloliweza imekubalika kuzikwa ndani ya sanduku.
Hata hivyo maiti inavishwa sanda, inalazwa kiubavu na hata huwekewa jiwe/dongo katika kitefutefu kama sheria zinavyosema.
Aliesema kuwa ni bora kujadili kama marehemu aliishi maisha ya kumpendeza mola wake, imani yako ni nini? wewe pegani au? kwa upande mmoja hujakosea lakini kwa upande mwengine ni kuwa hapakuwepo na haja ya kujadili lolote zaidi ya kumuombea dua huko aendako.
Mola amlaze marehemu mahali pema peponi amin.
Kwa kuchangia tu , mtu akizikwa kwa sanda , sanduku , container, na kadhalika yote ni sawa tu . muhimu atakayoulizwa kwa Muumba wake ni mema (AMAAL) gani na mazuri gani ya kumpendeza Mwenyezimungu aliyoyafanya katika uhai wake?. unaweza kuzikwa kwa sanda na ukafika mbele ya haki ikawa kasheshe kwa uliyoyafanya duniani. Mwenyezi Mungu amjaalie Marehemu Salim awe katika kundi la waja wake wema na amsamehe madhambi yake . ameen.
ReplyDeletemdau Pakacha UK