Mwakilishi wa Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Kusini Mohamed Mbiku (kulia) akikabidhi Jezi kwa mmoja wa viongozi wa timu ya Ilala Dr Andrew Mbuguni katika hafla iliyofanyika katika Ofisi ya Chama cha Soka mkoani Mtwara
Mwakilishi wa Mauzo wa TBL Kanda ya Kusini, Mohamed Mbiku (kulia) akikabidhi jezi kwa mmoja wa viongozi wa timu ya mkoa wa Lindi Dr Seif Sinani katika hafla iliofanyika katika Ofisi ya Chamacha Soka mkoa wa Mtwara
Naibu Meya manispaa ya Dodoma Jafari Mwanyemba akimuonyesha traki suti kocha wa timu ya Mazengo worrious Lister Mayala kwa ajili ya maofisa ambao wanashiriki katika michuano ya kili taifa cup mjini Dodoma. Hafla hiyo ilifanyika leo katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Meya wa Manispaa ya Iringa, Amani Mwamwindi akikabidhi jezi kwa Kiongozi wa timu ya Rukwa (Pinda Boys), Elisebius Mbinda, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ilipotoa vifaa vya michezo kwa timu tatu zinazoshiriki michuano ya Kili Taifa Cup katika kituo E cha Iringa, jana kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Iringa. Kushoto ni Msimamzi wa kituo hicho, Eliudi Mvera. Timu nyingine zilizopata vifaa hivyo ambavyo ni pamoja na jezi na mipira ni, Mbeya na Iringa. Picha na Executive SolutionsMICHUANO YA KOMBE LA
TAIFA CUP YAANZA LEO
Na Ripota wetu,
Mtwara
MABINGWA wa michuano ya Kili Taifa Cup timu ya soka ya mkoa wa kisoka wa Ilala leo inashuka uwanjani kuinza safari ya kutetea ubingwa wake kwa kucheza na Mtwara katika mchezo wa ufunguzi utakao fanyika kwenye Uwanja wa Umoja mjini Mtwara.
Akizingumza jana kocha mkuu wa Ilala Jamuhuri Kiwelu alisema kuwa vijana wake wapotayari kwa mchezo huo na watahakikisha wanaendeleza rekodi yao ya kulitwaa kombe hilo kwa mara nyingi zaidi.
Katika hatua nyinge Kiwelu alisema kuwa ataianza michuano hiyo kwa kuwakosa baadhi ya wachezaji wake wa kikosi cha kwanza ambao wapo na timu ya Simba nchini Misri akiwemo mlinda lango Juma Kaseja.
Alisema wachezaji hao watajiunga na timu hiyo katika hatua ya robo fainali ambayo itafanyika jijini Dar es Salaam.
Wakati huhohuo timu ya soka ya mkoa wa Lindi nayo pia itashuka uwanjani kucheza na Ruvuma mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ilala na Mtwara.
Timu zote nne zinazochuana katika kituo cha mtwara jana zilikabidhiwa vifaa na jezi za mechi watakazocheza katika hatua ya awali.
Timu 24 kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara inashiriki michuano hiyo ambayo inaanza kutimua vumbi leo katika vituo sita ikiwa ni pamoja na timu ya vijana chini ya mika 20 (Ngorongoro Heroes).

Who is who? It is hard to tell the difference between the mayor and the captain as they both look about the same (outside the standard brackets of active footbal)...Or it it only me?
ReplyDeletembona habari zote za blog hii hazina maana???????????
ReplyDelete