
TAMASHA HILI LITAFANYIKA KATIKA UKUMBI WA TASUBA UNAOMILIKIWA NA CHUO CHA SANAA KUANZIA SAA NANE NA NUSU ALASIRI HADI SAA NNE USIKU. LENGO LA TAMASHA HILI NI KUTOA NAFASI KWA WASANII MBALIMBALI KUTOKA HAPA NYUMBANI PAMOJA NA KWINGINEKO AFRIKA KUWEZA KUTOA BURUDANI, KUJIFUNZA BAINA YAO NA KUBADILISHANA UZOEFU, PAMOJA NA KUJITANGAZA.
VIKUNDI AMBAVYO TAYARI VIMETHIBITISHA KUSHIRIKI NI PAMOJA NA MOOKOMBA (ZIMBABWE), OMARY OMARY (TANZANIA), MAZS (ZANZIBAR), MAEMBE &THE BAGAMOYO SPIRIT (TANZANIA), JAGWA MUSIC (TANZANIA), JHIKOMAN (TANZANIA), NGOMA ZA ASILI ZA MKOA WA PWANI PAMOJA NA BODY MIND & SOUL (MALAWI).
VIINGILIO KATIKA TAMASHA HILO VITAKUWA NI SHILINGI 500/= WATOTO, SHILINGI 2000/= WAKUBWA NA SHILINGI 5000/= KWA WAGENI WASIO WAKAAZI .
WATOTO CHINI YA UMRI WA MIAKA MITANO WATARUHUSIWA BURE KAMA WATAKUWA PAMOJA NA WAZAZI AU WALEZI WAO....
KARIBUNI WOTE
Kwame Mchauru
Maisha Music
PO Box 105094
PO Box 105094
Dar es Salaam / Tanzania
+255 777 461911
HIvi kumbe Bagamoyo na Zanzibar ni nchi tofauti na Tanzania?
ReplyDelete