Waziri wa Fedha na Uchumi Mh. Mustafa Mkullo akitoa ufafanuzi leo mchana jijini Dar kwa waandishi wa habari juu uchangiaji wa bajeti unaofanywa na wafadhili. Shoto ni Afisa wa fedha za Nje Bi. Matembele. Picha na habari na MAELEZO

Katika maelezo yake Waziri amesema wafadhili hao wamekuwa wakichangia kiasi cha dola za Kimarekani milioni 754 mwaka 2009 - 2010 akasema kwa mwaka wa fedha wa 2010-2011 kiwango cha uchangiaji wao kitapungua mpaka dola za Kimarekani milioni 534 ikiwa ni pungufu ya dola milioni 220 katika bajeti ya Serikali.

Amesema kupungua kwa msaada huo kumetokana na kwamba wafadhili hao walitukopesha fedha wakati wa mtikisiko wa kiuchumi duniani ili deni hilo likatwe katika mgao wa fedha ambazo watatupa katika kipindi cha bajeti cha 2010-2011 ambapo amefafanua kwamba bajeti yote kwa mwaka ni asilimia 40 wakati uchangiaji wa wahisani ni asilimia 12 tu.

Amesema hayo Serikali iliyajua toka mwaka jana mwezi wa Novemba hivyo ilijiweka sawa ili kukabiliana nalo na tayari serikali imejizatiti kwani imeshakubaliana na Benki ya Stanbic ya Tanzania, Afrika Kusini na Uingereza na matawi hayo yote kwa ujumla yamekubali kuikopesha Serikali kiasi hicho cha dolla milioni 220 kwa ajili ya kufidia katika pengo la bajeti ijayo.

Moja ya matatizo yaliyoainishwa na wahisani hao ambayo serikali imetakiwa kuyafanyia kazi ni uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji nchini jambo ambalo limekuwa likikwamisha wawekezaji wengi kuja kuwekeza nchini ikiwemo mambo ya usajiri wa makampuni kuchukua muda mrefu, ucheleweshwaji wa kutoa mizigo bandarini na upatikanaji wa ardhi kwa haraka kwa wawekezaji hao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 22, 2010

    TANZANIA TANZANIA NAKUPENDA KWA MOYO WOTE

    INAMAANA NCHI YETU SIKU HIZI INATUMIA DOLA? KWANINI SERIKALI BADGET YAKE IKO INTERMS OF DOLLARS?

    Na greece walikopa kumeet budget yao siye kwanini tunawafadhili? What will they get in return? Hamna cha bure siku hizi

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 22, 2010

    Ndio maana maisha Tanzania hayalingani kabisa. Watu waserikali wao waneemika kwavile hela zao wajipangia kwa dola na wananchi wa kawaida wao wanaserebuka na hela ya madafu tu...ouch!!!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 22, 2010

    Tuachane na kuwategemea wafadhili. Mbona Kenya na matatizo yao yote wameweza kupunguza sana tegemezi ya aina hii!! Mungu ibariki nchi yetu. Bunge na serikali zipunguze matumizi yao!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 22, 2010

    kama kawaida yao kuwafanya watanzania wajinga. Wahisani wametamka wazi sababu za kutunyima msaada, hatukusanyi kodi wala kuboresha uwekezaji!!!!. Ndugu zangu mlioko nyumbani waonyesheni hao viongozi kuwa mna upeo wa kupambanua mambo siku ya kupiga kura. Mpaka mnyimwe misaada kwa sababu ya kutofanya kile mnacholipwa kufanya?

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 22, 2010

    SHIDA IKO WAPI...TUTAKOPAAA TUTALIPAAA!!!!duniani kote wanajaribu tumeshikilia haitoshi....kwanini mnasemehe makodi ya mamilioni ya shilingi????HUKU TUNAJIENGEZEA MISHAHARA NA MAGARI YA KIFAHARI....KATA BAJETI HIYOOOOO...KAZI KUWA NA VIJIMADA VINGI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...