Mjumbe wa Sekretarieti ya Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, Saidi Yakubu wa Bunge la Tanzania akiwa na mwenyeji wake, Osam Richard katika uwanja wa Mpira wa Mbombela ulioko katika jimbo la Mpumalanga, Sauzi ambao mbali na uwanja huo kutumika kwa ajili ya kombe la dunia, utatumiwa pia na zaidi ya wabunge 500 toka nchi 18 za Afrika ambazo ni wanachama wa chama cha wabunge wa jumuiya ya madola kwa ajili ya mkutano wao wa mwaka. Mdau Saidi Yakubu wa Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola akitoa maelezo kwa wenyeji wa Mkutano wa Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika utakaofanyika Mpumalanga, Sauzi mwezi Julai, kutoka kushoto ni Nd. Richardson, Mkurugenzi wa Utafiti Bunge la Jimbo la Mpumalanga, Nd. Moropa, Katibu wa Bunge hilo na wa kwanza kulia ni Nd. Simon, Katibu wa Kamati ya Ukaguzi wa Fedha za Umma, Bunge la Jimbo la Mpumalanga


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 20, 2010

    A lot of politics but less of an action, It should have been vice versa.

    Bunge la Jumuiya ya madola????? la Dodoma halitoshi?

    Next, Bunge la mkondo wa vyama Tawala kanda ya kusini mwa kaskazini ya Bara la Ulimwengu?? Seriously not a Joke! tupo hapa tutayaona yote haya, once a lot of taxpayers money is in the government coffer, wanakua walevi wa hizo pesa, hawajui wazifanyie nini, zaidi ya kuongea na kuongea na kuongea,

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 20, 2010

    Hivi nini lengo la bunge la umoja wa madola... ?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...