Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein, akisakata Rumba na Bi Elsie Kanza kwenye Tafrija ya kukamilisha mkutano wa Uchumi Duniani iliyofanyika jana wa kuamkia leo katika Viwanja vya Ikulu jijini Dar
,

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 07, 2010

    DUh Elsie umependeza sana....uko wapi siku hizi??Zuma alikutolea macho sana be careful......


    Mojo

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 07, 2010

    Mtu mzima anaselebuka taratiiibu! good time, great.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 07, 2010

    Nashukuru kutupeleka eneo la tukio hapo Mlimani City kuona viongozi wetu wakisakata Rumba Ni furaha kumwona Raisi wetu Mh sana JK akiwa na Mh J Zuma, Raisi wa South Africa ambaye amefagiliwa na chama cha ANC na kile cha wafanyakazi cha COSATU kuupata uraisi. Pia Mh Raila Odinga Makamu kule Kenya na Mh Dr Shein. Kweli walifanya kazi kubwa kama resource pool la viongozi makini wa AFRIKA kutuelimisha tulikotoka na tunakokwenda kiuchumi na Kidemokrasia. Baada ya kazi ngumu na maandalizi marefu wana stahili kuburudika kwa Rumba.

    Asubuhi nimeelimishwa na mada za makamu wa Maraisi Mfano Raila Odinga na Chingarai wa Zimbabwe kuhusu utata au challenge ya safari ya kuelekea demokrasia ya kweli na kujenga uchumi imara. Nchi hizi bado safari zao ngumu. Nashukuru Kenya wamechapisha Katiba yao au Road Map ya Demokrasia pamoja na ushirikishwaji wa wote katika ulaji wa rasilimali za nchi yao. Mzee Mkapa nae katufumbua macho juu ya tegemezi kithiri kwa wazungu.

    Hata hivyo hakuna kizuri kisicho na hasi. Mnajua wengi tumetaabika kuamka asubuhi mapema kuwahi kazini wiki hii. Hata hivyo misururu mirefu haikukosekana. Poleni wajawazito mlokuwa mnaelekea clinic na wale walokuwa wakienda Martenity Ward kujifungua.

    Lilonigusa zaidi ni pale watoto wa shule ya ST Mary ya Muheshimiwa Dr. G.R Kurudi shule J4 baada ya likizo ndefu na kushangazwa kupokea barua inayowajulisha likizo itaendelea wiki nzima hadi Mkutano wa Kiuchumi uishe. Hili lilinipa bumbuwazi. Yaani Watanzania bado hutujawa makini wa kupanga na kutekeleza pamoja na kutafiti njia mbadala hasa wakati wa emergence au adhoc programu. Iweje ujio wa wageni utibue program ya elimu mashuleni. Where is our preparednessplan??. Tumeshindwa kuratibu usafiri na miondo mbinu ya barabara, Mahoteli na Kumbi za mikutano Dar es salaam ziende sambamba na Mkutano wa Maraisi.

    God Bless Tanzania
    Richard Mazingira

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 07, 2010

    Haki ya nani toto mashallah naselebuka nalo urojo wa nini tena unguja.

    Big up nice PC

    MMMMMMMMMMMM

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 07, 2010

    Wewe Annoy wa Fri May 07, 04:07:00 PM, ni watu wachache sana wenye muda wa kusoma hayo yote uliyoyaandika, jaribu kuandika kwa kifupi, au tafuta ukurasa uandike makala yako

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 07, 2010

    Ikulu imegeuka sehemu ya kucheza muziki?Mungu wangu, afadhali Nyerere arudi, Ikulu Ikulu Ikulu, ni mahali pa takatifu, hata kama ni muziki wa watoto hauruhusiwi, labda ilikuwa ni Mlimani City, lakin kama habari inavyoonyesha hapo juu kuwa ni Ikulu, basi nadhan tumefika pabaya sasa!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 07, 2010

    Hizo scarf zilikua zinamaanisha nini? Naona kila mtu anayo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...