Mwamuzi wa akina akipadishwa mabegani na mwezake kwa ajili ya kufunga nyavu ya goli iliyojiachia baada ya mchezaji mmoja wa Moro Kids kupiga shuti kali lililojaa wavuni na kusababisha kuachia kwa nyavu hizo katika Uwanja wa Jamhuri leo. Katika mchezo huo Moro Kids iliifunga Timu ya Taifa ya wanawake Twiga stars bao 8-0.
Mchezaji wa timu ya Twiga Stars , Fatuma Hatibu ( jezi namba 10) akiondosha hatari katika eneo la lango lao wakati wa mchezo baina ya timu hiyo ya timu ya soka ya wanaume wenye umri wa miaka 20 ya Moro Kids, ambapo Twiga Stars ilifungwa mabao 8-0.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya soka la wanawake, ( Twiga Stars) , Charles Boniface Mkwassa, akitoa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa mapumziko katika mchezo wao uliofanyika juzi mjini hapa ambapo timu hiyo ilifungwa mabao 8-0.
Picha na John Nditi wa Globu ya Jamii Mji kasoro Bahari



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 06, 2010

    Fyeka majani!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 06, 2010

    Mkwasa WAPE FIMBO AU MBATA MAANA HUWEZI UKAWAFUNDISHA KWA MIEZI YOOTE HIYO ALAFU WAJE WAFUNGWE NA KATIMU KACHOVU KAMA HAKO

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 07, 2010

    Kocha anaelezea wengine wapo bize kwa kusukana na kutuma msg za mapenzi kwa mabwana zao,wataacha kufungwa? Wengine hapo hawakulala hata kambini wanawaza gemu la usiku.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...