Mpigapicha Mkuu wa Gazeti la Serikali la HABARILEO, mpiganaji Athumani Hamisi ambaye yupo nchini Afrika Kusini kwa matibabu kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, anataraji kurejea nchini siku ya Jumamosi Mei 8, 2010.
Kwa mujibu wa Chama cha Wapigapicha za Habari Tanzania (PPAT), ambapo hadi Machi mwaka huu alikuwa akikitumikia Chama hicho akiwa Mwekahazina Msaidizi, Hamisi atawasili majira ya Saa 12 jioni na Ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini.
Ndugu, Jamaa na marafiki wote wa Athumani Hamisi Msengi wanaombwa kufika katika mapokezi hayo na kumkaribisha tena nyumbani baada ya kuwa mbali kwa kipindi kirefu.
Athumani pamoja na wapigapicha wenzake wawili Anthony Siame na Marehemu Herry Makange walipata ajali ya gari Desemba 12 2008 baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka wakiwa njiani kuelekea Kilwa Masoko Mkoani Lindi kikazi.


Nilipata bahati ya kuonana na Bw Athuman wakati akiwa hospitali Jijini Johannesburg.
ReplyDeleteAmepata nafuu kubwa sana katika matibabu yake na Bw. Athuman alionyesha nia kubwa ya kutaka kurejea katika hali ya awali kabla ya ajali na pia alikuwa na mipango mingi kuhusu maisha yake ya baadaye.
Sintakuwa kijijini Jozi kumwaga lakini namtakia kila la heri katika jitihada zake ka kurejea katika hali ya kawaida. Karibu sana Tanzania Bw Athuman
Mdau
Dk Faustine
Mungu yu mwema! Habari njema! Best Wishes Kaka Athuman!
ReplyDeleteAsante Michuzi kwa taarifa hii.
ReplyDeleteNi faraja kubwa kusikia Mpiganaji Athumani Hamisi anarejea nyumbani. Nilibahatika kumuona akiwa Hospitali Muhimbili na baadaye Afrika Kusini.
Ajali ni ajali, ukisalimika unatakiwa kumshukuru Mungu kwa kuendelea kukujalia zawadi ya Uhai.
Kwa vile mimi ni mmoja wa yaliyonikuta kama yaliyomkuta Athumani, maisha yanaendelea, ila life is not the same again, tunahitaji zaidi marafiki wa kweli kuthibitisha urafiki wao dhati kwa watu kama Athumani Hamisi ili angalau, kuongeza matumaini ya maisha kuwa life still goes on.
Mdau Pascal Mayalla.
Kwa kweli Mungu ni mwema na yapaswa tumshukuru kwa kila jambo. Yote ni mapenzi yake na tumshukuru kwa hilo.
ReplyDeleteKaka Mayalla na Athumani hakika mungu ni mwema. Ndugu jamaa na marafiki bado wapo pamoja nanyi kwa shida na raha.Nazidi kuwaombea ili hali zetu zizidi kuimarika.
Sir Elton John katika wimbo wake alio washirikisha Gladys Nite, Kiki Dee na Steve Wonder Thats what Good friends are for, for bad time and Good time atakuwa nawe wakati wote.
Athumani Karibu sana nyumbani Tanzania.
Amina Mollel
Duh! Pole kaka Athuman. Karibu bongo! Hivi kumbe walipata ajali pamoja na Marehemu Heri Makange ambaye alikuja fariki kwa ajali ya piki2?
ReplyDeleteMungu mkubwa!
Abou-Kibaha.
Karibu Athumani, kuna msemo niliusikia zamani ningependa kukuambia leo, "never give up as long as you have your head above your shoulders."
ReplyDeleteBest wishes.