Mkurugenzi wa Taifa wa Olimpiki Maalumu, Frank Macha (kushoto) akiinua mpira wa Olimpiki utakaotumika kuzindua fainali za Kombe la Dunia 2010 zitakazoanza Juni 11 hadi Julai 11 mwaka huu Afrika Kusini, akiwa na wanaotembeza mpira huo katika nchi kadhaa duniani, Andrew Alis (wa pili kushoto) na Christian Wach. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa DHL, Dlase de Souza. Mpira huo unaotoa ujumbe maalumu wa kuhimiza walemavu kushiriki michezo ya Olimpiki, uliwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam jana ukitokea Arusha, kwa udhamini wa Shirika la Ndege la Precision Air, utakuwepo nchini kwa siku sita, na leo (Mei 4, 2010) utawekwa Uwanja wa Karume, Dar es Salaam kwa ajili ya kushuhudiwa na wananchi.
Mkurugenzi wa Taifa wa Olimpiki Maalumu, Frank Macha (kushoto) akiwa ameshika mpira wa Olimpiki utakaotumika kuzindua fainali za Kombe la Dunia 2010 zitakazoanza Juni 11 hadi Julai 11 mwaka huu Afrika Kusini, baada ya kuwapokea wanaotembeza mpira huo katika nchi kadhaa duniani, Andrew Alis (wa pili kushoto) na Christian Wach.

Mkurugenzi Mtendaji wa DHL, Dlase de Souza nae aliushika mpira huo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. florian rweyemamamuMay 04, 2010

    aisee, siye tutaishia kupata harufu ya pilau, msosi wala wengine.
    Hakuna hata timu moja itakayoshiriki kombe la dunia itakayofanyia mazoezi ( warming up) afrika ya mashariki. Vile vile hakuna hata referee mmoja wala mshika kibendera hatakayetoka afrika mashariki katika wale watakaochezesha kombe la Dunia.

    Kazi kweli kweli.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...