Ankal Asalaam Aleikhum Wallahmatullahi Wabarakatuw
Mie niko hapa umangani kwa muda lakini kiarabu hakipandi. Na hii atiko ya Waziri wetu wa Mambo ya Nje Mh. Bernard Membe akiwa na Waziri wa mambo ya nje wa huku Dr. Mohammed Anward Gargash nimeona nikuletee ili wadau wanaojua kiarabu watafsiri ili nasi kina yakhe tufaidie. Samahani kwa usumbufu
Mdau wa Dubai

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 28, 2010

    KIARABU NI LUGHA RAIS SANA KUJIFUNZA KWA MAANA MANENO MENGI YANAFANANA NA KISWAHILI, JITAHIDI KUJICHANGANYA MITAANI HUTACHUKUWA MUDA UTAJUWA TU

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 28, 2010

    Nenda kwenye Google Translator, halafu uandike hayo maneno ya kwenye gazeti, then uchague from Arabic to either English au Swahili utapata maana yake

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 28, 2010

    NITAKUPA KWA UFUPI TU WA HABARI HIYO

    NI KWAMBA WAZIRI HUYO WA HUKO FALME ZA KIARABU ANAONGELEA KUHUSU KUNUNUA ENEO ZIMA LA KIGAMBONI NA KULIJENGA KISASA NA KUUGEUZA MJI WA MARAHA YANI KUTAKUWA NA MAHOTEL MAKUBWA VIWANJA VYA MICHEZO MBALI MBALI NA MENGI MENGINEYO KUHUSU MARAHA

    SASA HAPO WAZIRI WETU ALIPOKEA MAOMBI HAYO NA KUDAI ATAYAFIKISHA KWA WAKUU WENZIE ILI KUJADIRI SWALA HILO LA KUUZWA KWA KIGAMBONI

    DAH HAWA WATU WANA MIHELA SI MCHEZO

    mdau wa mahakama kuu ya dunia nawakilisha tafsiri fupi ya kiarabu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 28, 2010

    HAPO JUU UMETAFSIRI VISIVYO. USITAKE KUPOTEZA WENZIO. PALE ANASEMA: sisi waarabu tunaona wivu kuona TZ wanataka kuichukua wazungu tu wakati ninyi watanzania ni mali yetu. Sasa tunataka kuja kuwatawala upya. Tumeisha chukua Mbuga za wanyama,kilwa,rufiji tukishamaliza , tutachukua mkoa mingine kadiri ya ratiba yetu, tutanusanusa bagamoyo, halafu tutaenda tunamega kidogo kidogo kulingana na njaa ya wa TZ itakavyokuwa inabana.

    Waziri alikubali katika lugha ya kiarabu cha kubabaisha alijibu: Hiyo ni kweli, mkinionyesha wema, mtapata mpaka bahari ya hindi

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 28, 2010

    wacha ukabwela huo wewe! unataka kumdanganya nani kuwa hujui kilichoandikwa hapo? unataka kutwambia kuwa umangani nzima hapo ulipo hukuweza kumuuliza mtu akutafsirie? Yuko wapi anaekutafsiria kila siku?

    Kwa nini udanganye? unajua issue yenyewe na unataka nasi tuijue, basi si sema tu, hapana haja ya kutufunga kamba.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 28, 2010

    mdau wa May 03:53 umedanganya

    KWA UFUPI. ISHU YOTE HAPO NI KUKUZA MAHUSIANO KATI YA UAE NA TANZANIA HASA KATIKA NYANJA ZA KILIMO NA UTALII. MANENO HAYO NI YA KILA SIKU TUNAYASKIA HAMNA JIPYA LOLOTE HAPO.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 28, 2010

    ahsante mdau sasa hapo ndio ujue CCM itatoka vipi mapema.... JAMANI NAFWA MIE NINA ENEO LANGU HAYO MAENEO SIJUI CCM WATANIMWAGIA UPUPU KWANI WAO HAWASHINDWI BANA... ANY WAY NI MTAZAMO ila mjue watz hapo ndio sehemu ya ccm kuchukua chao mapema, yaani jamaa shavu nhinha mcheck mh. WAZIRI shavu kama mie nadanganya.....

    wela wela tanzania ardhi bay umasikini welcome na tutaendelea kuuza ardhi hadi vizazi vyetu vikose mahali pa kuishi.

    NI MTAZAMO YALIYOMO YAMO

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 28, 2010

    US Blogger anazungumza Kiarabu, anaweza kukusaidia.

    Huyu jamaa anazungumza Kiswahili, KIngereza, Kiarabu, KIhaya, KIfaransa, Kijerumani

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 28, 2010

    Nadhani huyu mchangiaji wa mwisho kaja kufurahisha barza tu maana anachokisema hakihusiani kabisa na stori yenyewe.

    Huyo ni waziri wa nchi za nje wa Imaarat Anwar Muhammad Qarqash akibadilishana mawazo na Waziri Memb katika kujenga mashirikiano kwa nyanja tofauti.

    Pia waziri Membe alimshukuru Waziri Qarqash pmoja na Imarat kwa misaada tofauti iliyotoa kwa ajili ya tz. Pia alimuela jinsi Tzilvyowarahisishia wafabnya biashara kutoka Imarat katika kuwekeza hasa kwenye Utalii na kilimo.

    Pia waliohudhuria ni Balozi Maharage Juma na Balozi Isa Abdullahh Basha -mkurugenzi wa kitengo cha Afrika kwenye wizara ya nje

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 29, 2010

    Eti naskia watani wajadi wamelikoroga Dubai, vibarua vimeota mbawa na si nyasi na sasa mkenya haruhusiwi kuja fanya kazi U.A.E kama hana degree, (hapo nyuma walikuwa wanashuka kwa mkupua ndege moja watu 100 wote wanakuja kazini) hivyo vinafasi nafasi vingi waliokuwa wanapigana vikumbo na maphilipino viko wazi, sasa nauliza serikali yetu hamna mtu au huyo muheshimiwa hapo kwanini hawawaombei waTZ wawe wanapewa vibali kufanya kazi huku sababu sasa hivi hata house girl mTZ kumleta shida lakini MAJIRANI zetu wamejazana kila kona. Sababu ya kuomba waheshimiwa wawaombee ni kuwa naskia Kenya waliombewa na viongozi wa serikali yao. kama hili litafanikiwa si jamani vijana wengi watapata ajira na kusaidia familia zao? nyinyi mnaonaje jamani wadau?

    Sababu ya kulikoroga naskia waliwafanyia mbaya Masheikh wa huku walipokwenda Kenya kutembea waliwatia ndani, waliwaambia wao alqaeda kisha waliwaibia pesa zao hata walipojitambulisha hawakuwasikiliza!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...