Msaada wa materials
Habari za kazi kaka michuzi.Mimi naitwa zamda ni mwanafunzi, nilikuwa naomba nitumie blog yako kuomba msaada wa material au doccuments za biofuels hasa guideline ya biofuel investment maana nimejaribu kuitafuta lakini sijabahatika kuipata,nimepiga simu wizara ya kilimo na wizara ya nishati lakini sikuweza kupata draft yoyote.
Nimeomba draft kwa kuwa Tanzania bado hakuna policy yoyote inayohusika na uwekezaji wa biofuel zaidi ya hiyo guideline hadi hapo watakapokuwa na policy. Ninaomba kwa yoyote ambae anaweza kuwa na hiyo guideline anisaidie ili niweze kukamilisha report yangu ya mwisho.
Nitashuluru sana kwa msaada wenu.Naomba anaependa kunisaidia awasiliane nami kwa email yangu:
Zamda kwanza pole sana kwa shule.
ReplyDeleteMimi naitwa Abdul Ali. Hayo material ninayo. Issue ni jinsi ya kunipata. Anyway mimi ninapatikana Kijitonyama, ukifika pale Break point-Sayansi uliza kwa mzee Ali Mkubwa watakuelekeza kwangu nitakupa hayo material tu aunt.
Tembelea blog yangu na utajifunza kuhusu jatropha (mbono) kama una swali tuwasiliane kupitia mail yangu
ReplyDeleteKaka Abdul mbona unambania dada Zamda...email amekupa sasa si umtumie kwa email mpaka tena aje breakpont..hata kama ni paper work scan utume..utabarikiwa.
ReplyDeleteMMH, WEWE ZAMDA UKIENDA HAPO KIJITONYAMA KWA HUYO ABDALA USIENDE PEKE YAKO, SHAURI YAKO.
ReplyDeleteMmh, misaada mingine inaonyesha dalili za masharti humu. Mhusika katoa anuani pepe kama unataka kumsaidia, wewe unataka akufuate nyumbani sijui Break Point sijui Komakoma.
ReplyDeleteMwalimu Nyerere aliwahi kuwaambia wahisani kuwa tunakubali misaada lakini "with no strings attached", yaani bila masharti. Mimi pia ni Abdul (lakini si huyo wa breakpoint kijitonyama).
ReplyDeleteMwalimu Nyerere aliwahi kuwaambia wahisani kuwa tunakubali misaada lakini "with no strings attached", yaani bila masharti. Mimi pia ni Abdul (lakini si huyo wa breakpoint kijitonyama).
ReplyDeletewee 12:53:00pm nani kasema waislamu hapa??
ReplyDeleteacha jazba wewe!!tumia ubongo
matope
Matope, nadhani hukunielewa kabisa. Nilipomnukuu Mwalimu nilikuwa na maana ya kuwa ukitaka kumsaidia mtu usimpe mahsrti. Huyo dada katoa e-mail yake lakini mdau (ambae ni mwajina wangu, yaani wote tunaitwa Abdu) akaanza kumwelekeza nyumbani kwake. Nina maana mimi pia ni Abdul lakini siye huyo wa kijitonyama, umenielewa sasa??? Sikutaja suala la dini. soma na uelewe kabla ya kukurupuka kwa jazba. Mimi Abdul lakini siye wa break point.
ReplyDelete