Bwana Dunstan Rutageruka wa Sinza
Dar es Salaam anasikitika kutangaza kifo cha Baba yake Mzazi
Mwalimu Novati Simeon Rutageruka (pichani)
kilichotokea katika Hospitali ya Hindu Mandal
Dar es Salaam Jumatano,tarehe 5 Mei 2010.
Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa mtoto wa marehemu, Sinza block D,karibu na Hotel ya Vatican. Habari ziwafikie Mtoto wa Marehemu, Illuminata Rutageruka Maerere akiwa Ofisi za Umoja wa Mataifa Sudan, Mtoto wa Marehemu, Balozi Liberata Rutageruka Mulamula akiwa safarini Marekani, Wana Ukoo wote wa Abalondo popote pale walipo, Wana kijiji wa Musibuka, kitobo,kiziba Bukoba popote pale walipo pamoja na ndugu jamaa na marafiki popote pale walipo
Marehemu, ambaye alizaliwa mwaka 1931, amepata kushika nyadhifa mbalimbali serikalini ambapo alishiriki katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1985 na kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Kagera na pia Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge na Diwani wa Kagera kati ya mwaka 1984-200, ambapo pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Afya na Mazingira na pia mjumbe wa mkuatno mkuu wa CCM.
Marehemu Mzee Rutageruka pia amewahi kuwa kiongozi mahiri wa michezo katika mikoa ya Pwani, Dar es salaam na pia Mwenykiti wa FAT mkoa wa Pwani. Apat kufanya kazi kama Mkurugenzi wa Wilaya za Kinondoni, Dodoma mjini, Karagwe na Biharamulo kati ya 1972 hadi 1983.

Marehemu, ambaye ameacha watoto sita na wajukuuu 17, Anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumapili Mei 9, 2010 kijijini kwake Musibuka, Kusuba, Bukoba.
Ratiba ya mazishi:
Mwili wa Marehemu utafikishwa Kanisa la St. Peters saa tisa mchana kesho Ijumaa kwa misa na heshima za mwisho. Baada ya hapo, mwili utapelekwa nyumbani kwa mtoto wake, Sinza, tayari kwa ajili ya safari ya kwenda Kiziba Bukoba mapema Jumamosi asubuhi.

MOLA AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI
-AMEN

may grandpa rest in peace
ReplyDeletepoleni sana
ReplyDeleteBalozi Mulamula pamoja na wafiwa wote, poleni sana kwa msiba wa Baba; Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi na nyie awatie nguvu na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu cha maombolezi. Tumshukuru Mungu kwa kila jambo. Amen.
ReplyDelete