Mpiganaji Athumani Hamisi akiwasili juzi toka Afrika ya Kusini alikokuwa akitibiwa kwa takriban mwaka mmoja kufuatia ajali ya gari iliyotokea wilayani Rufiji mkoa wa Pwani Septemba 10, 2008 BOFYA HAPA
Na Muhidin Michuzi
Juzi tumempokea mpiganaji mwenzetu Athumani Hamisi ambaye amerejea akiwa amepooza mwili wote kufuatia ajali hiyo. Ilikuwa furaha kumuona tena Athumani ambaye nilibahatika kumtembelea akiwa hospitali Johannesburg. Kubwa nililoliona ndani ya macho yake ni ari yake ya kutaka kuendelea na mapambano, japo amepooza mwili wake wote, ukiacha mikono ambayo anaweza kuitumia, japo kwa shida kidogo. Lakini alipotua tu ilijionesha dhahiri kwamba kichwa kiko salama kwani aliweza kuongea na kumtambua kila mtu. Pia mng'ao wa macho yake ya kuwa na ari ya kupambana na maisha hivyo hivyo alivyo sio tu ulikuwepo, bali ulikuwa mkubwa zaidi.
Azma ya kuandika hii rai ni changamoto iliyopo mbele yetu sisi wapiganaji wenzie Athumani. Je, tutamsaidiaje aweze kutimiza ari yake ya kupambana na maisha katika hali hiyo aliyonayo?
Tayari wadau kadhaa wameshatoa wazo la kumfanya Athumani awe Balozi Maalumu wa Kupambana na Ajali nchini. Kwani kila kukicha imekuwa kama fasheni kusikia na kuona taswira za ajali barabarani kila sehemu ya nchi, huku ndugu zetu wakipoteza maisha na wengine viungo kutokana na ajali hizo zisizoisha. Kubwa zaidi juhudi za kupunguza kama si kukomesha kabisa ajali hizo bado hazijasikika zaidi ya kusikia wito tu kwamba tuwe waangalifu. Je, wito unasaidia nini?
Hivyo naunga mkono wazo la kumfanya mpiganaji Athumani Hamisi kuwa Balozi Maalumu wa Kupambana na Ajali nchini. Natumai, kwa kupitia chama chetu cha wapiga picha za habari a.k.a Press Photographers Association of Tanzania (PPTA), chini ya Mlezi wetu Rais Jakaya Kikwete pamoja na uongozi wa mwenyekiti wetu mpya Mwanzo Millinga na Katibu Mkuu Mroki Mroki, hilo linawezekana kabisa.
Mchakato na uanze mara moja kulifanikisha hilo ili PPTA itoe mchango wake katika kupunguza ama kuondoa kabisa jinamizi la ajali nchini, tukiongozwa na Balozi wetu mteule, Athumani Hamisi.
Zaidi ya rai hii, Globu ya Jamii inatoa wito kwa Serikali, makampuni na watu binafsi kuanza kufikiria namna watakavyoweza kuifanya rai hii iwe kweli. Hapa itahitajika michango ya hali na mali pamoja na kupanga ratiba za uhamasishaji kila mahali na kila mkoa ambako Athumani awe anakwenda kutoa mada akiwa kama Balozi.
Sina wasiwasi kabisa kwamba, akiwa mmoja wa wathirika wa ajali za barabarani, sauti yake itasikika kila mahali na kuwafanya hata wahusika waliolala waamke na kuanza kuchukua hatua za dhati kumtokomeza Jinamizi wa Ajali nchini.
Haya shime Wanachama wa PPTA na Watanzania kwa jumla tuungane kupambana na Jinamizi la ajali badala ya kukaa tu tukiridhika kwamba yote hayo ni KAZI YA MUNGU. Wakati ni kweli hiyo ni kazi ya Mungu na haina makosa, lakini si uwongo kwamba tukiacha kupiga domo na kuanza kuchukua hatua, hili linaweza kabisa kufanikiwa.
Na Mungu huyo huyo, tujiulize, atupe nini tena zaidi??
Tayari katupa mpiganaji Athumani Hamisi ambaye tukimfanya Balozi wa kupambana na ajali za barabarani Mungu, anayependa wanaojituma, inshaallah atatusikiliza tu. Na si vibaya endapo kama tuzo kwa wataofanya juhudi za kutukuka kupunguza ama kuondoa ajali zikawa zinatolewa kwao. Ziitwe Tuzo za Athumani Hamisi kama kielelezo.
Naomba kuwasilisha. Maoni na ushauri unakaribishwa na mjadala uanze ili mchakato uendelee wa kupambana na Jinamizi la ajali nchini...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 11, 2010

    wazo zuri sana wana habari. AJALI ni jinamizi ambalo tukiamua tutalishinda.. tengenezeni utaratibu NIPO tayari. ATHUMANI Mungu ni Mwema na kwake kila JAMBO LINAWEZEKANA JIPE MOYO... TUPO PAMOJA NAWE.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 11, 2010

    hilo nalo neno kaka michuziii

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 11, 2010

    Wazo zuri sana,lakini tunapo amua kupambana na ajari kuna mambo Mengi ya Kuzingatia. pamoja na
    1:Ubora wa Magari-Asilimia kubwa ya magari hasa ya abiria ni mabovu mno na yamekwisha kabisa.
    2:Upatikanaji olela wa leseni.
    3:Rushwa- Madereva hawana uoga,hata wakikamatwa si wanatoa kidogo yanaisha.
    4:Nchi za wenzetu siyo kila mtu anaweza kuwa dereva,tena wa abilia,kwetu ukimuona tu dereva wakipanya na suruali zake tatu tena kazivaa kwa mpigo,utashangaa kwanini huyo mtu anadhamana kubwa hivyo ya kubeba roho za watu.
    5:Barabara zetu pia zina changia,alama hadimu na magari ni mengi kulinganisha na ukubwa wa barabara

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 11, 2010

    Ni wazo zuri, lakini kwanini wazo hili lije baada ya Athumani kupata ajali!! kwa nini huko nyuma bila kusubiri mtu aumie wazo hili lisingekuwepo, na nina imani lingeokoa maisha mengi! wale wote tuliopoteza ndugu zetu kwenye ajali na kukapita kimnya bila wazo hili kuwepo, wale tulio na ndugu zetu vilema kutokana na ajali wapo hawawezi tena kujikimu, kwa nini wasipate chance kama Athumani!! kwa nini hadi mtu alyekuwa maarufu apate janga ndio watu wafunguke macho!! je, ni kwa kumpa maslahi! wangapi wapo majumbani, wamepooza kwa ajali ili hali huko nyuma walikuwa na watu maarufu! tusiende hivyo, swala sio mpaka limpate kiongozi ndio livaliwe njuga, fungueni macho kila wakati janga linapotupata, sio mpaka limpate fulani!
    nana

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 11, 2010

    sorry, wazo zuri. lakini Athumani ni nani? na ni nini kilitokea? je sifa za balozi ni zipi? je anazo?

    asante

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 11, 2010

    pole athumani , michuzi saa zingine sikuelewi , ulivokuwa unasema mpiganaji athumani mimi nilidhani alikuwa bondia, kumbe ni mwandishi wa habari .. sisi wengine hatujaelewa , naomba uwe unajua kwamba si kila mtu anaelewa mpiganaji ni mwandishi wa habari ..

    Ahsante

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 11, 2010

    Mzee Michuzi kweli mshikaji ni shujaa. Bado tunamwombea atapona.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 11, 2010

    Kaka Michuzi,

    Tumepata maelezo ya kutosha, the WILL is there, but we need to sit down first and foremost with Athumani, and talk through about this idea, and carry on from there.

    What do I mean by carry on,

    First and foremost we have the purpose, which is significantly an important part of it,

    Secondly we need a mechanism, of running the idea onto action, e.g establishing a website, just explaining what it is all about, creating a special account for that only purpose, I am sure there are a lot of us who are more than willing to contribute kwa VITA HII, INAMUATHIRI KILA MMOJA KWA NJIA MOJA AU NYENGINE, IT IS A CAUSE WHICH I BELIEVE HAVE A LOT OF INTEREST HERE IN TANZANIA AND ABROAD. na hizi contribution zifanyike kwa njia ya PAYPAL, and other CREDIT CARDS, na kwa wadau wa nyumbani hata kwa njia ya simu kama huduma za MPESA, nk, kwa sababu hili litahitajia pesa kuweza kufanikisha safari za Athumani sehemu mbali mbali kutoa HOTUBA, kuwahamasisha watu, kutengeneza ADD kwenye televisions na RADIO, kutengeneza mabango, na most importantly kumsaidia Athumani katika maisha yake, I am confident this opportunity wont get to worst, There is a lot can be achieved.

    Na kama ulivyosema Michuzi, watu binafsi na makampuni, yako mengi ambayo yako tayari kuchangia kwa njia moja au nyengine, you will be surprised by the response, but first we need to create an ESTABLISHMENT, not a big one, but just an informative WEBSITE, without office but just a patron(Athumani), loading few videos of interviews na msaidizi wa kujitolea, ambao watakua wanakaa every two weeks or a month, and planning a next move, I think from this grass root movement, will eventually grow bigger than you would have imagine, na hii itapolekewa vizuri sana na wanahabari kwa ujumla, in other words PUBLICITY will be there, which is desperately needed.

    Na kuhusiana hii michango, it doesn't need to be a lot of money, but it has to be regular for the time being, ie, there more than willing to contribute $10-$20 every month, and in return they will get an update of the progress that is being made, first teaching peoples of Danger associated with Road USERS, whether that in Schools, Kata, mikutano ya hadhara nk. it simply becomes an investment worthy investing on. A LOT OF LIFES WILL BE SAVED, SURELY!!

    Jengine zaidi, ambalo wengi wataliona kama sivyo, lakini ni muhimu sana kuhusisha vyombo vya kiserikali na mamlaka husika katika mpambano huu, kama ulivyolielezea, kupata mwongozo wa Rais, you never know may be the next budget will be hearing a fund has been set up just to ALLEVIATE ROAD ACCIDENTS, by PROVIDING MUCH NEEDED INFORMATION ON THIS ISSUE TO THE GENERAL PUBLIC. It is a campaign worthy fighting for.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 11, 2010

    Inatia huzuni kila uingiapo blog za Tanzania na kukutana na ajali za magari, watu wanapoteza maisha yao na serikali haionekani kujali. Mengi yanatakiwa yafanyike kupunguza ajali, kwanza barabara hususan zinazounganisha miji mikubwa lazima ziwe na uwezo wa kupitisha gari manne kwa wakati mmoja, mbili zinaenda mbili zinarudi (dual carriage way)na ziwe zimetenganishwa katikati, hii itasaidia ajali za uso kwa uso. Pili barabara ziwe pana na kuwe na sehemu ya gari kusimama bila kuzuia magari mengine (hard shoulders) hii itapunguza ajali zinaso husisha magari yaliyoharibika. Tatu ianzishwe idara mpya itakayo shughulikia mafunzo na utoaji wa leseni kwa kila mtu anaye taka kuwa dereva na leseni zilizotolewa kabla ya hapo zisitishwe. Adhabu ziwe kali kwa mtu atakayeendesha gari bila leseni na atakaye sababisha ajali.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 11, 2010

    KWA UPANDE WANGU HILI SWALA HALINA MJADALA, ATHUMANI UBALOZI UNAMFAA KABISA.
    ILA ISIWE TU MANENO NI PAMOJA NA VITENDO KWA MFANO
    1.WATU WOTE WANAOENDESHA MAGARI WARUDI KTK KOZI ZA USALAMA BARABANI AMBAZO LESENI ZAO ZA SASA ZIFUTWE ZIANZISHWE UPWA NA MTU KUPATA LESENI MPAKA APASI MTIHANI WA USALAMA BARABARANI.
    2.ASKALI WA USALAMA BARABARANI WAKIKAMATWA WANACHUKUWA RUSHWA WAPEWE ADHABU YA KUFUNGWA MIAKA KUMI NA PAMOJA NA KUPOTEZA KAZI
    3.WAANDISHI WA HABARI NYINYI NI KAZI YENU KUHAKIKISHA TRAFIKI HAWAPOKEI RUSHWA.

    CHA KUSIKITISHWA NI HIVI MME WANGU ALIKUWA LIKIZO NCHINI TANZANIA YA WIKI TATU BASI AMERUDI KANISIMULIA NJISI MAMBO ALIYOYAONA HUKO BONGO NI PAMOJA NA TRAFIKI BARABARANI, MIFUKO YAO IMEBADILIKA LANGI KWA AJILI YA KUWEKA PESA YAANI INGEKUWA NI AMRI YAO WAWE NA MIKOBA KAMA WAFANYABIASHARA. KWA MTAZAMO WANGU TRAFIKI WANACHANGIA SANA AJARI ZA BARABARANI IKIWA PAMOJA NA LESENI FEKI.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 11, 2010

    Kamichu ushauri wako ni mzuri sana tena labda hapo watajitokeza watu wa kusaidia kuwapromote watu wetu wenyewe kama manesi na madokta watakao speshialaize kwenye tatizo la uti wa mgongo, sio kama hivi tunaleta watu wa wenzetu ambao kuna wengine watakaoshikwa na matatizo kama haya watashindwa kuajiri nesi wa nje. Hatuna jinsi isipokuwa kukutegemea wewe michuzi sababu uko karibu hata na JK. na pia ingekuwa vizuri ungetoa na picha yake kaka hamisi ya wakati anapigana tuone kwa wale tusiojua alikuwa nani.
    Najua kuna watu watakaoniponda ila jaribu kujifikiria je ungekuwa wewe, au angekuwa ndugu yako au mtu yoyote wa jirani ungejisikiaje? tujumuike kusaidia wenzetu kwa hali na mali.

    NB: kamichu kuna njia yoyote ambayo unaweza kutuachia habari zikae japo siku mbili kabla hazijapotea? kwa sie tuliokuwa ulaya tukija huku tunakuta habari zishaondoka. Pls.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 11, 2010

    kamichuzi kwanini usimuintavyu kaka yetu tusikie kwa maneno yake anaendeleaje? camera unazo, kila kitu so tunakutegemea utuletee habari zaidi.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 11, 2010

    hey huko juuuuuu what is AJARI??? ni AJALI sema L L L L L L L L L L L L L L L L L L L L L L L L L L L L L L L........

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 11, 2010

    Kwa kweli ni wazo zuri kabisa. Kama ambavyo kuna mabalozi wengine wengi, mfano Balozi wa Redds, mabalozi wa nyumba kumi, na kadhalika, nadhani haitokuwa mbaya Ndugu yetu Athumani akiwa Balozi wetu mteule wa ajali, kama yeye mwenyewe yu radhi.

    Ndimi Balozi wa Nyumba Kumi,
    UKonga.

    ReplyDelete
  15. KWANZA KABISA NI KUIONDOA SERIKALI YA CCM MADARAKANI NA KUWEKA VIJANA WACHAPAKAZI WATAOKUWA TAYARI KUSHUGHULIKIA TAKA TAKA ZOTE KWENYE MIFUMO YA JAMII KATIKA NCHI YA TANZANIA. TATIZO NI MFUMO CHAKAVU NA MBOFU MBOFU. BILA YA KUCHAGUA WABUNGE WENYE KUWEKA UTU KWANZA BADALA YA PESA, HIZI AJALI ZITAENDELEA TU HATA NANI AWE BALOZI.

    SASA NI HIVI CCM IMESHINDWA INAKAA KUDANGANYA WATANZANIA AMBAO WANADANGANYIKA KIRAHISI. TUAMKE WOTE KWA PAMOJA NA KUPIGIA KURA YA HAPANA CCM NA WABUNGE WOTE WALIOPOMADARAKANI SASA HIVI KWANI WAMESHINDWA KAZI.

    PIA SHERIA YA NCHI IBADILISHWE, MAWAZIRI WASIWE WABUNGE, BALI WAWE WANAPITISHWA NA BUNGE KUFUATANA NA UZOEFU WAO WA MASUALA HUSIKA KWENYE WIZARA. HAPO UTAONA TUNAPATA WAZIRI WA MIUNDOMBINU ALIKUWA TAYARI KULISHUGHULIKIA TATIZO LA AJALI SI ZA BARABARANI TU HATA USALAMA WA WATUMIAJI WA HIO MIUNDO MBINU CHAKAVU! PAMOJA NA WALE WEZI TRAFFIKI POLISI, WAKAGUZI WA BARABARA NA WAFANYAKAZI WA UWANJA WA NDEGE WANAOKWAPUA MABEGI YA WAGENI. KILA KITU NASIKIA KINANUKA HASA SISIEMU.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 11, 2010

    True hata mimi nakubaliana na wazo lako. na pia huyo anayesema kuwa kwanini awe mtu huyu na sio ndugu zao waliopooza nyumbani...Ni kwasababau watu wanakuwa waangalizi zaidi wakimuona mtu aliyekua anajulikana. Unaona kama gonjwa la ukimwi Magic Jackson-USA ni balozi wa huo ugonjwa pia.

    lakini kama walivyosema hao hapo juu inahitaji kujua ugonjwa uko wapi na kwanini ajali ziwe nyingi hivi na hamna anayesimama katika setikali na kutafuta solution.

    1. Tuchague viongozi wapya wenye uchungu wa ncgi.

    2. Tuangalie lesseni na usajili wa magari TZ zinatolewaje.

    3. Watu wenye leseni wanaelewaje hizo alama za barabara. Iwe lessen zikiwa zimefika muda wa kurenew iwe kuna brush test tena ya kuona mtu anaelewa vipi au macho yake yanaona vipi.

    4. Rushwa..kuwe na undercover people wanaowashika hao matrafic wanaochukua rushwa. lakini hata Obama amesema Africa haitasimama kama haitaweza kuteketeza rushwa....

    Ni mengi sana ya kubadilishwa kwenye sheria zetu za uongozi na utekelezaji...true sioni sababu ya mbunge kuwa waziri...nadhani hiyo sheria ilitungwa ule wakati ambao hamna watu wengi wa kufanya kazi mbunge ataweza kuiwakilisha sehemu yake vipi kama kila siku yupo mjini?

    Na pia mtu akiamua kuwa mbunge basi asijishughulishe na biashara zingine kwavile kutakua na iterest conflicts.

    na hata wakuu wamikoa wasichaguliwe na raisi tena kwa vile watakua wanafanya kazi kumplease raisi na sio kufanya kazi kwa kuwajibika kwa wananchi...mkuu wa mkoa wilaya wote utakuta ni haoa hao kila siku wanahamishwa mikoa hii na kupelekwa kule...Hivi hamna watu wa kufanya kazi vizuri kweli but kushuffle watu? Mtu akiharibu huku anahamishiwa huku...Sheria inabidi ibadilishwe sannnnnnnna tu...
    .

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...