Mwenyekiti wa Semina ya Wabunge wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika
Mashariki inayojadili umuhimu wa kushirikisha wabunge katika utungaji wa
sera za biashara, Mhe. Dr. Raphael Chegeni akimkaribisha mgeni rasmi Naibu
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Mama Masekgoa Masire Mwamba kufungua
rasmi semina hiyo, katikati ni muwezeshaji wa semina hiyo Peter Mathews
toka Geneva, Uswizi
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Mama Masekgoa Masire Mwamba
akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua semina hiyo

Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Mama Masekgoa Masire Mwamba akiwa
na Kaimu Mkuu wa Mkoa, Raymond Mushi pamoja na waratibu wa semina hiyo,
Saidi Yakubu wa Tanzania (kulia) na Shem Baldeosingh toka London (kushoto)

Bunge la Tanzania wiki hii lilikuwa mwenyeji wa wabunge wa
nchi za jumuiya ya Madola kanda ya Afrika katika semina kujadili namna
sera za biashara zinavyoathiri ukuaji wa biashara yenyewe hasa katika
medani ya kimataifa iliyofanyika mjini Arusha.

Biashara ya Kimataifa inatambulika duniani kote kwamba ndio kiungo cha
ufanisi wa uchumi duniani na hivyo sera zinazosimamia biashara hiyo ni
sehemu muhimu zaidi katika kuendeleza mikakati ya uchumi na pia katika
jitihada za kufuta umaskini katika nchi zinazoendelea.

Hata hivyo; Utungaji, Usimamizi na hata uratibu wa wa sera za biashara kwa
kiasi kikubwa umeachwa mikononi mwa watendaji wa Serikali na katika maeneo
mengi ya nchi zinazoendelea hata usimamizi wa Bunge katika kuhakikisha
uchunguzi wa sera na uwajibikaji wa watendaji wake ni mdogo sana.

Hivyo; ili kuwa na uchumi imara na sera muafaka za biashara, nguvu ya
Bunge katika kusimamia utendaji wa Serikali katika utungaji wa sera ni
muhimu.

Ni kwa kuzingatia hilo,Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola duniani
(Commonwealth Parliamentary Association – CPA) kushirikiana na
Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola kiliandaa semina maalum kwa Wabunge wa nchi za Tanzania, Kenya, Uganda na Rwanda ili kuweza kujua nafasi yao na fursa walizonazo katika kuendeleza biashara kwa kuisimamia vyema Serikali
iwe na sera muafaka.

Bunge la Tanzania liliwakilishwa na Mhe. Dr Raphael Chegeni, MB, (CCM)
Mhe. Siraju Kaboyonga,MB (CCM) na Mhe. Maulidah Anna Komu (CHADEMA).

Aidha, Semina hiyo ilifunguliwa rasmi na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya
Madola, Mama Masekgoa Masire Mwamba kutoka Uingereza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 31, 2010

    PICHA YA TATU NAONA HUYU MAMA AMESIMAMA VIZURI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...