Marehemu Hassan Habibu Nyenzi

Familia ya Nyenzi ya Dar es salaam inatoa shukrani za dhati kwa wote waliohusika kwa namna moja au nyingine katika kukamilisha safari ya mdogo wetu mpendwa Hassan Habib Nyenzi aliyetangulia mbele ya haki kufuatia ajali ya gari iliyotokea tarehe 15/5/2010 majira ya saa 1.30 jioni eneo la Mlandizi karibu na daraja la Ruvu, mkoa wa Pwani.
Si rahisi kumshukuru mtu mmoja mmoja na tunaomba hii iwe ni shukrani kwenu nyote. Tunashukuru kwa misaada yenu ya hali na mali katika wakati huo mgumu, hatuna cha kuwalipa zaidi ya kuwaombe kwa Muumba wa Vyote Mwenyezi Mungu awape uzima na afya njema na awazidishie neema na fanaka katika maisha yenu.

Mungu Ailaze mahali pema
peponi roho ya merehemu
-Amina
Salehe Habib Nyenzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. poleni sana ndugu zangu..saleh naomba simu au email adress yako..yangu ni kckuyava@hotmail.com
    ahsante sana MAX KUYAVA U.K

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 23, 2010

    poleni sana wafiwa..inasikitisha sana. His life was cut too short.

    Hizi ajali kila siku zinaleta majonzi mengi sana..

    RIP

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 23, 2010

    Poleni sana wafiwa. Jamani jamani hizi ajali mpaka lini? ni madereva au ni barabara. Tafadhali tusihongane leseni.Mafunzo ni muhimu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...