Ndugu Michuzi,
Nikiwa mmojawapo nayependa kusoma habari katika blog yako nakuomba uweke hii tahadhari kwa wananchi wote kuhusu wizi wa vibaka katika barabara ya Kawawa.

Ni jana tarehe 23.05.10 majira ya saa 3 usiku tulitokea katika sherehe katika ukumbi wa Ilala Boma. Kabla hatujakaribia mataa ya barabarani ya Chang’ombe watoto waliokuwa wamekaa katika kiti cha nyuma walikuwa wanapeana mawasiliano ya simu. Kibaka alijitokeza lakini alikuta kioo kimepandishwa , bila muda alifungua mlango na kumnyanga’nya yule binti ile simu.

Ni jambo la hatari ambalo hatukulielewa kwani magari yalikuwa mengi tena katika foleni. Alitokomea katika kichaka cha majani na miti. Wananchi tuwe macho kufunga milango ya magari mara tuwapo katika safari katika barabara hizi hapa DSM.

Vile vile tunaomba vyombo vya dola kufuatilia maeneo haya hasa nyakati za usiku kwani ndio mwanzo wa kuzalisha majambazi wa kuteka mgari hata kuiba vitu vingine katika magari wakati yanatembea.

Natumaini kama ufuatiliaji utakuwepo hata huyu aliyetuibia simu hii atakamatwa.
Mdau Kinondoni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 24, 2010

    poleni.jamani wizi huu
    maisha yamekua magumu sana kwa watu mitaani so chochote wanafanya,hakuna usalama kabisa these days!!

    sasa wizi la laptops ndo usiseme
    Mwenyezi tusaidie

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 24, 2010

    pole lakini ni uzembe mliofanya , utaacha vp milango wazi ? hasa sehemu ile , UMEJIFUNZA KUTOKANA NA UZEMBE WAKO

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 24, 2010

    Kwa nini uendeshe gari bika ku-lock milango???

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 24, 2010

    wewe Mon May 24, 10:41:00 AM, kuna kosa gani kuendesha gari bila ya kujifungia ndani? yaani ni kosa lake mtu kutojifungia ndani ya gari? why?

    just imagine umejifungia mlango halafu unapata ajali watu watafunguaje milango haraka haraka?

    Infact kwa nini nisiwe na uhuru wa kuendesha gari bila kujifungia ndani? Nyuma kama nina watoto hiyo kweli ni kwa sababu ya usalama wao, na ndio kuna child locks katika gari.

    Lakini wizi huu ungeliweza pia kutokea kwa mtu mzima kama amekaa mbele au nyuma na hajajifungia.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 24, 2010

    Hapo hakuna jinsi hata mki-'lock' milango watavunja vioo na mkiweka nondo/nyavu ktk madirisha mfano wa magari ya deraya(FFU), ndo mtasimamishwa huku 'vibaka' wakiwa na silaha za moto!

    Jawabu ni 'socio-engineering', kuwa nyie wenye nafasi na mlioshikilia uchumi wa nchi kwa njia za uhalali au ki-'EPA' muanze kujua kuwa ktk nchi kuna watu masikini wanaolala na njaa na hawana matumaini ya kuokoka toka wimbi la umasikini.

    Pia wanaona majarida/ mabango ya kibishara/TV yakionyesha waliofanikiwa kimaisha kwa kuwa na simu za mkononi, laptops, magari, majumba ya kifahari n.k n.k

    Hawa masikini hata wakitaka pasipoti wazamie waende nje ya Tanzania kuzipata mbinde/ taaabu, hivyo wameamua watabanana nayi 'matajiri' humo humo Bongo mpaka kieleweke.

    Wenye-nchi mkiona imefikia hapo basi, waacheni vijana watimke waende pande zote za dunia wakatafute 'rizki', maana mmeshindwa kuwapatia ajira, kilimo kwanza, biashara n.k

    Kifupi, fungulieni geti kwa kuwapa vijana pasi za kusafiri kiurahisi wakatafute maisha.

    Mdau
    Rio De Janeiro

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 24, 2010

    Maeneo ya mataa ya chang'ombe, eneo la darajani, kamata na keko yote mpaka njia panda ya kwenda taifa (mafleti) ni vibaka watupu na kila siku mnaambiwa hivyo kupitia michuzi lakini hamkomi sasa tuwasaidiaje? hao ni watoto wa keko kusoma hawataki wao wanachojua ni mazoezi ya ngumi na kunyanyua vyuma ili wajaze vifua waweze kukaba watu vizuri

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 24, 2010

    Unatupotezea wakati na vijipost vyako..........hivyo vitukio vya long wala hukutakiwa kuvipost

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 24, 2010

    Ndo maana natembea na cha moto!!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 24, 2010

    bongo tambarare

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 24, 2010

    dah pole sana, hiyo sehem ni mbaya sana. kuna siku tulikuwa tunasubiri mataa yawake (mataa ya chang'ombe) nilikuwa nikitumia simu huku kioo kiko wazi(ni uzembe) ghafla nikashtukizia mtu hata alipotokea sikujua, akanidaka mkono, bahati nzuri nilikuwa nimeishika simu kwa nguvu kwahiyo akawa anajaribu kuivuta, wakati anaendelea kujaribu, ndugu yangu alikuwa amekaa kiti cha nyuma alichomoza na kumvuta upande wake kwa kumshika shati( kamkunja na kumnyanyua)mataa yakawaka tukaanza kumburuza hadi upande wa pili. hadi tunamwachia sura yake ilikuwa haitamaniki kwa kisago heavy alichopokea kutok akwa ndugu yangu aliokaa nyuma.... ila aliniskitisha sana kwani alikuwa akijitetea kwa kusema maisha magumu jamani, hali ngumu nichunieni.... haya maneno hadi leo nayakumbuka na kila nikikumbuka inanitia uchungu sana.... sasa hapa sijui alaumiwe nani kwakweli??!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 25, 2010

    annon may24 9.27 pm

    unatakiwa wewe uanze hatua kusaidia hawa vijana kivyovyote tu ili wasiendelee kukwida watu njiani..serikali itafanya nini wewe?na life gumu kishenzy out there usipime ndugu

    na mjifunze kufunga lock na mikanda

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...