Michuzi naomba kuuliza.
Je umri wa rais kuongoza unaweza kuchangia mafanikio ya nchi husika?? Hebu tuangalie tofauti za baadhi ya marais wetu Afrika na baadhi ya wale waliopo Ulaya. Nawasilisha mkuu, na mjumbe hauawigi...
DEO MUSHI

BAADHI YA MARAIS WA AFRIKA NA UMRI WALIO NAO
Hosni Mubarak ( Misri) miaka 82
Robert Mugabe ( Zimbabwe ) 86
Hifikepunye Pohamba ( Namibia ) 74
Rupiah Banda ( Zambia ) 73
Mwai Kibaki ( Kenya ) 71Colonel Gaddafi ( Libya ) 68
Jacob Zuma ( Afrika ya Kusini ) 68
Ian Khama ( Botswana ) 57
JK (Tanzania) 59
Wastani: 72.4
______________________________
UGHAIBUNI MAMBO NI HIVI
Barrack Obama (USA) 48
David Cameron (UK) 43
Dimitri Medvedev ( Russia ) 45
Stephen Harper ( Canada ) 51
Kevin Rudd ( Australia ) 53
Nicolas Sarkozy ( France ) 55
Luis Zapatero ( Spain ) 49
Jose Socrates ( Portugal ) 53
Wastani: 49.6
SIKU NJEMA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 24, 2010

    Huyu nae kichwa maji,ndo wastani gani huu??!!! rudi darasani kijana...

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 24, 2010

    ndo maana marais wa afrika uwezo wa kufikiri unapungua

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 24, 2010

    mbona raisi wa Congo hujamuweka?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 24, 2010

    Unataka kusema kuwa Ughaibuni hakuna rais mwenye umri wa miaka 55?yani umetafuta maraisi wazee Africa na vijana Ughaibuni.tabia mbaya hiyo

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 24, 2010

    I must say, Hosn Mubarak and Robert Mugabe look quite young for their age ..

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 24, 2010

    Swala siyo umri, bali kupambana na changamoto za vipindi mbalimbali cheki umri wa marais ambao nchi zao kiuchumi zimeendelea:

    George Bush senior 69 USA
    Ronald Reagan 77 USA
    Winston Churchill 77 UK
    Mahathir bin Moh'd 88 Malaysia
    Surharto 77 Indonesia
    Chiang Kai-Shek 88 Taiwan

    Hapo wastani unauona mwenyewe, hivyo uongozi siyo suala la umri bali visheni ya kuongoza nchi ipige hatua kubwa ya kimaendeleo kijamii, kiuchumi na kitamaduni.

    Mdau
    Shimoni Kariakoo

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 24, 2010

    Hakuna uhusiano wowote wa umri na utendaji wa kazi za ma-rais mahala popote duniani,na hamna hata research moja inayooshaonyesha hivyo, after all the president is doing nothing as he or she has loads of watalaamu katika maeneo yote. Rais ni kama chief katika kijiji mambo yote anatendewa na kuelekeza hata kama akiwa kichwa/genius, na zama si za mbali sana nchi za ulaya kama USA, UK na URUSI walikuwa wanapendelea sana viongozi wazee wakisema wana uzoefu si wa kazi ya urais bali wa maisha na wemeona mengi. Tatizo ni viongozi wenyewe binafsi wa bara la Afrika na priority zao, wengi wamechukuwa for granted kuwa sisi ni wajinga hatujuwi kitu. Marais wengi wa Africa, whatever age no matter what, what they priotise is their own benefits not those of the populace, and they do so simply because in Africa we dont have checks and balances, if we have, then they dont work properly and they have no concrete legal backing. Ndo maana WANAIBA na kuboronga madaraka na tunawatazama tu. Huwezi KUIBA na kuboronga madaraka Ulaya ukatazamwa tu. Mifano tumeiona USA Richard Nixon alivuliwa madaraka kwa WATERGATE KASHIFA, MA-SENATA kibao wanakula mvua 100 kwa makosa ya rushwa na wizi. Vyombo vya habari viko huru kuelezea hali halisi bila ya uoga na kuwaachia wananchi wenyewe waamua wakati wa uchaguzi mkuu. These things will never happen in Africa, unless we change our mind set.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 24, 2010

    Kama post yako ina maana yeyote, basi tofauti ya maendeleo kati ya Tanzania (59) na Ufaransa (55) ni ndogo sana! Na tukitaka kupata maendeleo chachap tumchague Ridhiwani Kikwete?

    "U-Raisi si kubeba Zege" Malekela.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 24, 2010

    Mi naona tukitaka maendeleo chapchap tumchague Kanumba the great na PM awe Ray Kigosi.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 24, 2010

    Mwai Kibaki wa Kenya alizaliwa Novemba 15, 1931, Kwa hiyo umri wake ni miaka 78, siyo 71.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 25, 2010

    Point of correction, David Cameron siyo rais bali ni waziri mkuu wa United Kingdom.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 25, 2010

    Huu ndio mjadala ambao unapaswa uwe kwenye magazeti kila siku kukumbusha wananchi hasa afrika kuwa wanapaswa kuwa mbali. Uhusiano kati ya umri na utendaji ni muhimu vilivyo, kwana umri unaonyesha mafanikio, huko kwa wenzetu kugombea lazima uonyesha mafanikio yako binafsi na sio mchovu unaetegemea kuponea ikulu, hili ni muhimu kwani hawana njaa wanaonyesha ni kitu gani wanataka kuwafanyi wananchi na siyo kitu gani atapata kutoka kwa wananchi. Pili huyu mtu umri umekwenda na labda alianza kukishililia kiti hicho tangu kijana mpaka uzee na hatimaye mauti kumkuta madarakani, atapata wapi changamoto kama uendeshaji wake ni ule ule miaka nenda rudi? Kuneemeshana wakati wengi wanaumia, mbona hata raisi aki-retire bado anapeta saana tena bila majukumu, analindwa na kupata zaidi ya maofisa serikalini. Wenzetu wanafikiri kuancha jina na kuonyesha umaarufu kwa kuwapa waliowengi. chukulia Obama hakuwa na shida kabla ya madaraka, aliondoka anahitaji kubeba nini ambacho alikuwa hana kabla? Inaishuhudia historia na kuacha historia ya aina yake, angalia kwetu ..... Ulaji tuuu maulimi nje nje. Tunajiuliza lini tutafika - wapi tunakokwenda?

    ReplyDelete
  13. Al MusomaMay 25, 2010

    Kuna mtu aliwahi kuniambia kuwa mtu anakuwa mzee pale anapokuwa mkubwa kuliko Rais au Waziri mkuu. Kwa maana hiyo nitakuwa kijana kwa muda mrefu - wadumu viongozi wetu...

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 25, 2010

    Neno "rais" asili yake ni wapi??? Mi nahisi kuwa ni neno/jina la kutoholewa, ila sijui linakotokea haswaaaa???? Tafu wamatumbi.

    ReplyDelete
  15. kweli,
    tunajua Ronald Reagan miaka yake ya mwishoni ya urais Alzheimers full chaja, watu wakawa wanazani ana act tu kupiga mbonji kwenye mikutano kumbe mwenzao tayari full moon, Nancy ndo alikua raisi ndo alikua anashinda nae oval office kumbembeleza kutia masign.Nancy alikua hachezi mbali,. This is true story.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 25, 2010

    Wacha zako:-

    Jean-Claude Duvalier became president of Haiti at age 19.

    Joseph Kabila, was 29 when became president.

    El Hadj Omar Bongo Ondimba (born Albert-Bernard Bongo on 30 December 1935) became President of Gabon in 1967, He was just 31 .

    Andry Rajoelina, 35, President of Madagascar.

    Yahya Abdul-Azziz Jemus Junkung Diliu Jammeh, President of Gambia he is 44

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 25, 2010

    Topic hii ndo yenyeweeee...Inaonyesha ni jinsi gani umri ulivyo na effect katika kutoa maamuzi haswaaa...that being said ndo maana Nchi za Africa tunakufa masikini..Maraisi wetu ni wazee sana wanatakiwa ku retire sio kuongoza. when u r that old your thinking capacity can be not so good!! thanks

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 25, 2010

    Anon May 24, 09:35,

    What a good way of putting it! Ha ha haaa. You have hit the point home!! It is not about the age!!

    Anon May 24, 08:47,
    Nondozzz..

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 25, 2010

    hii sample haina maana. Katafuta maraisi wazee wa africa, akacompare na vijana wa duniani! mbona hapo kuna mabara mawili against one. Kama unapima then pima bara zima ama kipimo chako ni maraisi wa weupe na weusi? Mbona wa India hayupo, North Korea, Malaysia, Cuba, Chile etc. Ama hao huwajui????hii haina maana yeyote

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 25, 2010

    Africa ni jadi yetu kuongozwa na wazee. Tuwape wazee heshima inayostahili, kuna msemo unasema 'what an old man sees while sitting,a young man can not see even when he is on the top of the tallest tree'.

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 25, 2010

    Anon May 25,

    I am impressed that you are knowledgeable in such issues as Alzheimers..

    First Lady Nancy must have been very conversant with her Agenda..

    Bye just now..

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 25, 2010

    Kweli kabisa uwezo wa kuongoza haupo kwenye umri, ni uwezo wa kufikiri, kufanya maamuzi ya busara, na kuwa na discipline kwenye kazi zako. Kwanza sipati picha kungekuwa na viongozi wa 30s na 40s tu, ingekuwa vurugu tu... na vi miss vyetu vingekoma... Na hao wanaopiga kelele kuhusu wabunge wenye umri mkubwa ni wehu... angalieni viongozi kama akina ted kennedy walikuwa kwenye senate mpaka umri gani? Na kama kuna kijana ambae ni raia na anataka kugombea ubunge/urais/udiwani, si agombee! mbona mnapiga domo tu? hasa nyie wa jamii forum... Kama nyie ni watu wazima wenye akili timamu na ni vijana wenye nguzu zenu kwa nini mnataka short cut? mnadhani hao mnaowaita viongozi wazee walibebwa? wali struggle mpaka kufika hapo walipo...nyie mnataka mpachikwa tu... hizo tabia ni za kichangu za kutaka mambo kiulaini bila jasho... Ushauri wa bure...FUATA NDOTO ZAKO AND WORK HARD TO MAKE THOSE DREAMS COME TRUE... la kama hamuwezi...kaa kimya! Na hiyo tabia ya kudharau wazee itawatokea puani siku moja!

    ReplyDelete
  23. tatizo la nyie vijana wa Africa mkipewa urais mnaongeza wake tu kwikwikwi

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 25, 2010

    Waziri Mkuu wa sasa Italy, Silvio Belsconi sasa ana miaka 74, Italy uchumi umetulia na pia hata timu yake binafsi Inter Milan pia imefanya mambo makubwa. Bado Magazeti yake binafsi na vituo vyake binafsi vya TV/Radio huko Italy pia vinapeta vizuri.

    Sisi uchumi na timu za mpira 'kichwa cha mwendawazimu'- nimenukuu.

    ReplyDelete
  25. Correction kwa Anon 11:27:00! Silvio Berlusconi anamiliki timu ya AC Milan na sio Inter Milan! Mwenye Inter Milan ni Massimo Moratti! Careful kabla hujatoa data kama hizi kwa wadau!

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 25, 2010

    hakuna kitu hapa wewee!!

    iko siku tutafika tukiacha kunyemelea utajiri pindi unapopata kazi tu...hii tabia inaanzia nyumbani pale life linapotupiga,so linaendelea adi uko mbeleni

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 25, 2010

    72.4-49.6=22.8
    NO WONDER AFRICA TUKO NYUMA KIMAENDELEO KWA MIAKA 20 NYUMA.

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 25, 2010

    Wacha ushamba wewe. Berlusconi timu yake ni AC Milan sio Inter Milan. Zinduka

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 25, 2010

    UPUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUZI MTUPU!!!!!!!!!!


    Ni nani kakwambia kuwa ubongo unazeeka?

    Ubongo ni sawa na msuli; usipoutumia, utavia!

    Wakati mwingine ugonjwa wa fahamu ndio unaouathiri.

    Hebu soma haya yafuatayo. Ni elimu tosha kabisa:

    SOURCE: npr.org/templates/story/story.php?storyId=126115275

    (NPR = National Public Radio - USA)

    April 20, 2010

    Though people can become more forgetful in middle age, research suggests that they're at the top of their game in other areas, such as vocabulary and reasoning.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...