Kaka hebu tuijadili kwa nguvu zote mada ya hii
hapa chini na tuipigie kelele kweli kweli


JUZI MAJIRA YA SAA SABA USIKU RAFIKI YANGU ALIKUA ANA RUDI NYUMBANI KWAKE KUPITIA NJIA YA KAWE CHINI. BAADA YA KUVUKA KIDOGO DARAJA LA KAWE (MAKAO MAKUU YA JESHI LA KUJENGA TAIFA) GHAFLA AKAKUTANA NA MAGOGO YAMEPANGWA BARABARANI KUZIBA NJIA NA ALIPOJARIBU KUPUNGUZA MWENDO ALIWAONA WATU WAKIJA TOKA NYUMA YAKE WAKIIBUKIA VICHAKANI, UAMUZI ALIOUCHUKUA NI KUPARAMIA YALE MAGOGO UKIZINGATIA GARI YAKE SIO KUBWA YALIHARIBU MIGGU YOTE YA MBELE NA BAMBER LAKINI ALIKIMBIZA HADI POLISI KAWE NDIPO ALIPOJIHISI YUPO SALAMA LAKINI GARI MBELE KOTE HAIFAI

CHA KUJIULIZA, HII SIO MARA YA KWANZA KWA UJAMBAZI HUO KUTOKEA MAENEO YALE NA KUNA KIPINDI KULIKUA NA ULINZI WA PAMOJA KATIKA ULTIMATE SECURITY , POLISI NA JKT LAKINI NADHANI ULINZI HUO HAUPO TENA

NAWASHAURI WAKAZI WANAOTUMIA NJIA HIYO NI BORA UZUNGUKE LUGALO NI SALAMA ZAIDI KULIKONI NJIA HIYO HASA WAKATI WA USIKU MKUBWA. NASIKITIKA KWAMBA VITENDO HIVYO VINAFANYIKA MITA CHACHE TOKA MAKAO MAKUU YA JKT???

MDAU, KAWE

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 11, 2010

    tanzania tanzaniaaaa sikupendi kwa moyo woteeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 11, 2010

    Noma sana. Hii ni kazi ya polisi, kulinda usalama wa raia. Sintoshangaa kama tunasubiri wawekezaji kutoka ng'ambo...au misaada ya wazungu kuimarisha huduma za kipolisi.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 11, 2010

    Kuichukia Tanzania ni sawa na ku-hate the game...which is wrong, ni hao viongozi ndio wamechemsha kabisaaaa, kazi kula kodi zetu tu bila ya kuinufaisha nchi.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 11, 2010

    Wewe uliesema unaichukia Tanzania hufikilii vizuri. Hukuhuko ulipo kama ni USA au nchi ingine kuna matukio kibao ya mauaji ya silaha. Wewe subiri ukifa utachangiwa uje kuzikwa hukuhuku bongo...

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 11, 2010

    HII ISSUE NAKUMBUKA TULISHAWAHI KUIZUNGUMZIA SIKU ZA NYUMA HUKO. INASIKITISHA SANA HATA HUO ULINZI UNAOWEKWA PALE HUWA NI KAMA ZIMA MOTO TUU. AIBU KUBWA NI KWAMBA MAKAO MAKUU YA JKT YAKO PALEPALE MPAKA HIVI SASA NAAMINI LABDA HAO ASKARI WA JKT NDIO WANAOFANYA HUO UJAMBAZI!.. INAWEZEKANAJE KWELI HAPOHAPO JESHINI UJAMBAZI UKAWA UNATENDEKA NA WAO WANAJIFANYA HAWANA HABARI. LAZIMA JKT PALE KUTAKUWA NA WATU WANANUFAIKA NA HUO UJAMBAZI. JKT WANAWEZA HATA TUU KUWEKA MATAA YAKAWA YANAMULIKA PALE DARAJANI NA MAZINGIRA YAKE HAO MAJAMBAZI HAWAWEZI KAA PALE, LAKINI HAWAFANYI KITU CHOCHOTE KUZUIA UHARIFU HUU. HII NCHI MPAKA SIKU MOJA AVAMIWE WAZIRI NDIO UTASIKIA HATUA ZINACHULIWA RAIA WA KAWAIDA ANAONEKANA HANA THAMANI. NI AIBU SANA KWA JKT MLALAKUWA MAMBO KAMA HAYA KULALAMIKIWA KILA SIKU.

    NI AIBU KWA POLISI WANASHINDWA KUZUIA UHARIFU HUU..
    NI AIBU KWA JKT KWA KURUHUSU UHARIFU BARAZANI KWAO..

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 12, 2010

    USIONE AJABU HAPO WANASHIRIKIANA NA HAO JKT WALIOPO ZAMU ZA ULINZI, KWANI HAINGII AKILI MWIZI KUFANYA HIVYO NA USIONE AJABU NI JKT WENYEWE. HUU NI MWAKA WA UCHAGUZI TUTUMIE BUSARA ZETU KUCHAGUWA VIONGOZU BORA.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 12, 2010

    mi nakubaliana na anony wa 09:57, kama vipi polisi nayo ibinafsishwe

    ReplyDelete
  8. matanzaniaMay 12, 2010

    Hii shughuli wanafanya wenyewe jkt zama za kufichaficha mambo watz lazima tuziache na polisi baadhi wanajua ndiyo maana muda huo hakuna patrol inapita mitaa ile.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 12, 2010

    chakusikitisha zaidi barabara anayoshauri mdau (lugalo) ndio ile inayojaa malori mabovu yanayobeba cement toka kiwanda cha wazo, yanansababisha ajali kila siku.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 12, 2010

    Wewe mchangiaji wa kwanza unayeichukia Tanzania: mimi mara ya kwanza kumuona mtu akipigwa risasi mbele ya macho yangu ilikuwa ni 1992 huko Queens NY USA. Kuna Mtanzania rafiki yangu alipigwa na skinheads UK mpaka akapooza nusu ya mwili (paralysis). Kaa hukohuko ule makombo ya wazungu wewe as a second class citizen (house nigger "lapdog"). Kurudi kwenye mada yetu: (1) Usiku funga milango yote (lock) na pandisha vyoo; (2)Ukifika njia panda kama hakuna magari usisimame (3) Fanya mazoezi ya "reverse" katika sehemu nyembamba ili siku utakapokuta njia imefungwa uweze ku-reverse gari haraka. Mbinu hizi nilijifunzia Kenya ambako vitendo kama hivyo ni kitu vya kawaida. Eddy.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 12, 2010

    Inatosha kusema kuwa ni aibu kubwa sana mahali kama jkt mlalakuwa kufanyika vitendo vya ujambazi. ni aibu, hivi tusemeje ili tueleweke? inawezekena vipi makao makuu ya jeshi ndipo pakawa sehemu ya ujambazi? mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama upo kweli?

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 12, 2010

    we punguani hapo juu sio kila anayekufa nje ya nchi aje kuzikwa bongo na sio kila anayekufa nje ya nchi anachangiwa wengine sio walala hoi kama wewe kalagabahoooo

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 12, 2010

    mr mdau kama ulishuhudia mtu kapigwa risasi mbele ya macho yako kimpango wako hata bongo watu wanauliwa na risasai na mbaya zaidi huko rushwa imestawi kama maua kaeni na dhiki zenu naishi vizuriii kama ulipokuwa huku hukutoka akili yako ilikuwa imedumaa sirudi huko ng'oooo kwani shida nnini? unaongelea ishu ya 92 we ndo pimbi kweli njoo new york ule raha kama ulibaguliwa ulikuwa umekaa kifalafala huna lolote bongo kuna dhiki sana nani hajui ? hata kama unayo hela pa kuzitumia ni shida pia naona umadenge umekuganda mukichwa GOOOOD BLESSS AMERICAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA!!!!!!

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 12, 2010

    Anyony wa Tarehe Wed May 12, 10:47:00 AM unayejiita Eddy. Ushauri wako ni wa kijiweni sana! Ina maana hao majambazi ni wajinga kiasi gani wazibe barabara halafu wao wasiwe nyuma yako kabla hata hujaamua kujapiga revasi? Kama unataka umia zaidi tumia hizo mbinu zako. Hapa tunazungumzia kuzuia haya mambo wewe unaleta kujua kwamba wewe ni mjanja sana wa kukwepa majambazi. Huo ni ubinafsi tuu unakusumbua. Eti mazoezi ya rivasi.. kwani dereva gani hajui rivasi? Unazungumzia kufunga vioo.. kwani wao wana hasara gani kuvunja hivyo vioo? Unafikiri wataogopa kuvunja?
    Acha hizo.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 12, 2010

    Maisha magumu jamani wacha watu wajitafutie riziki zao kwa namna yoyote ile mbona Zombe aliitafutia mkate wake namna kama hizo? Karamagi, Lo.., Mramba, Liumba/ msishangae sana jamani kibaya ni kuotewa tu lakini maadam mmepewa tahadhari basi poa ichukueni kama tahadhari.Lakini suala la kwisha hivi vitendo tusahau kwa sasa. Hali ni mbaya

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...