TOKA MWAKA 2000 MPAKA MWAKA 2003 MSANII ALIKUA ANACHUKUA SHILINGI 100/= KWA KILA TAPE MOJA AMBAYO ILIUZWA 1,200/= MWAKA 2004 MPAKA SASA MSANII ANAPOKEA SHILINGI 200/=, KATIKA TAPE INAYOUZWA SHILINGI 1,500/=, JE KWA NINI BIDHAA YA MZIKI HUWA HAIPANDI BEI KAMA BIDHAA ZINGINE? NADILIKI KUIFANANISHA BIDHAA YA MZIKI KAMA BIASHARA YA MUUZA GENGE,NDIZI,MIWA, MAHINDI NA N.K. KIUKWELI IT'S TOUCHING.
-DUDUBAYA
KWA UJUMBE HUU NA MAMBO MENGINE KIBAO




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 20, 2010

    WAULIZE CCM.AU WEWE HUJACHANGIA?NILIFIKIRI NINYI WASANII MNA MAPESA MENGI HADI KUCHANGIA CCM,KUMBE.....TEH TEH TEH

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 20, 2010

    Bei ya muziki haiwezi kupanda na inflation kwa sababu inategemea sana demand na supply. Wakati uchumi unakwenda vizuri, watu wanapokuwa na pesa za ziada kwa ajili ya burudani watanunua sana kanda za muziki na hivyo demand yake kuwa kubwa na bei kupanda. Wakati uchumi umekwenda mrama demand ya burudani hupungua na hivyo bei ya muziki pia kushuka.

    Vile vile kukiwa na wanamuziki wengi wanaopiga muziki wa aina moja, basi kunakuwa na kanda nyingi sokoni kiasi kuwa bei ya muziki huo inapungua. Kumekuwa na bongofalva nyingi sana kati ya mwaka 2002 hadi leo. Inaelekea mwaka 2004 hakukuwa na wanamuziki wengi sana kama ilivyo leo, au wanamuziki wa wakati huo walikuwa hawatunzi muziki kwa haraka haraka kama leo. Vile vile kuwepo kwa burudani nyingine kama kanda za movie kunapunguza demand ya muziki na hivyo kudororesha bei yake.

    Kupungua kwa bei ya muziki siyo tatizo la Tanzania tu, bali ni la dunia nzima ambapo kwa marekani mauoz yalipungua to dola 24 kwa cd moja hadi dola 4 kwa CD moja. Wanamuziki wa Marekani hawategemei sana mauzo ya kanda bali hutumia zaidi concert tours kujitengezea mapato yao

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 21, 2010

    Mdau wa Mwanzo Point nzuri kweli ule wizi mtupu.... wa CCM.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 21, 2010

    CHA MSINGI HAPO NI HALI YA UCHUMI WA NCHI NDIYO INACHANGIA DEMAND YA VITU NA BEI ZAKE. NINAPOSEMAHALI YA UCHUMI WA NCHI INAMAANA PANA SANA. KWA MFANO MTU HAWEZI KUNUNUWA CD YA MUZIKI KAMA HANA RADIO INYOPIGA HIYO CD NA HII HUTOKANA NA HALI HALISI YA UCHUMI SI WATU WENGI WENYE UWEZO WA KUWA NA VITU KAA HIVYO SO DEMAND ITAKUWA NDOGO NA KAMA SUPPLY IMEKUWA KUBWA SANA YA MUZIKI WA LEO SO BEI ITAKUJA CHINI KWA VILE WANAO-DEMAND NI WACHACHE KWA VILE HAWANA UWEZO WA KUNUNUWA VYOMBO VYA KUSIKLIZA MUZIKI HUO. PIA TECHNOLOGIA ILIVYOKUWA INAWEZEKANA WATU WENGI WANAWEZA KUPATA BURE MIZIKI YENU KWA BILA YA KULIPA PESA. LINGINE NI LABOUR POWER EMBODIED KWENYE KAZI ZENU HAINA SI YA ZAIDI YA HIYO PESA MUNAYOUZIA CD. NA HII PIA NI SWALA LA HATUA GANI NCHI IMEFIKIA MAENDELEO YAKE KIUCHUMI KIASI KWAMBA INA UWEZO WA KUWAJAZA WATU MAPESA MFUKONI NA KUJENGA PURCHASING POWER, NDO MAANA TUNAONA COKE TANZANIA NI SHS 300 KWA CHUPA WAKATI KWA MFANO UNITED KINGDOM PENGINE NI POUND MOJA. KAMA UTAZILINGANISHA PESA HIZI KWA PESA MOJA NI KWAMBA BEI YA SODA UK NI SHS ZAIDI YA 2000 NA TZ NI SHS 300 HAPA UNAJIULIZA KWA NINI WAKATI SODA NI MOJA ILEILE. NI VITU VINI HAPA VINAFANYIWA MAHESABU YA KITAALAMU, KWA MFANO KIBARUA WA KUTENGEZA HIYO SODA KATIKA NCHI ZOTE MBILI ALILIPWA KASI GANI, UMEME ULILIPIWA KIASI GANI KWA SODA, MASHINE GHARAMA ZAKE KWA SODA, KODI ZA NCHI HUSIKA, DEMAND AND SUPPLY, GDP NA VIT KAMA HIVYO. LAKINI KWA MIAKA HII KUUZA CD BADO 1500 NI DEZO

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 21, 2010

    Concerts ndizo zinalipa na private shows. MAREHEMU MICHAEL ANGECHUKUWA POUND MILLIONI 50 KWA SHOWS ZAKE UK KAMA ASINGEKUFA. LIONEL RICHIE HUWA ANAIMBA KWENYE PARTY ZA WATU BINAFSI ANACHKUWAGA DOLA 500,000.00 PENGINE KWA MASAA MAWILI TU.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 21, 2010

    mimi nimechangia, wewe je?

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 21, 2010

    DUDU BAYA,ur very lucky kipato kimepanda kutoka tsh100-200 thats 100% rise.....nilikuwa nanunua cds £15-20 miaka 5-7 iliopita leo hii cd haizidi £10,hela ngumu ndugu na cd ni leisure haiwezi kupanda kama bidhaa nyingine.
    kingine ni kuwa hii ni free market kwanini usi-negotiate vizuri na whoever anaeku-offer tsh200/cd akupe tsh1000/cd.JIBU UNALO.

    ReplyDelete
  8. Kaka TrioMay 21, 2010

    msimdanganye mwenzio wenu. Hiyo ingine ni ni faida ya distribution chanels yani walee wasambazaji, na gharama zingine za uandaaji ya muziki wako na kukumeneji wewe kwa maana huwezi kujimeneji wewemwenyewe na kuzifanya hizo shughuli zote za kuandaa muziki na hadi usambazaji.

    Si unaona hata huko USA kwene iTune unanunua muzika kwa bei ya senti kadhaa za dolari unafikiri mwanamuziki anapata kiasi gani?

    Kwa maneno mangine ndio mana unaona wanamuziki wangine wako independent ili angalau wapate mgao mkubwa kuliko ule ambao wangeupata endapo wangekuwa wamejiandikisha kwene lebo fulani au manejiment fulani

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 21, 2010

    Hi ndugu yangu Godfrey Tumaini au Dudubaya, Mimi nakubaliana moja kwa moja na maoni ya mdau wa pili. Kutokana na uchumi dhaifu wa-Tanzania wengi hawana pesa za ziada. Kwa walio wengi pesa zote zinaishia katika kodi, chakula, elimu na bili nyingine kibao. Isitoshe wengi hubaki na madeni kila mwisho wa mwezi. Kwa mantiki hiyo kwa walio wengi burudani kama muziki na mengineyo huwa sio kipaumbele. Mimi nadhani muda umefika kwa wasani wenyewe kuamua upande wa kwenda. Kama tatizo ni kuchacha kwa sababu ya ukosefu wa kipato kutokana na mauzo ya kanda then kuna njia nyingi za kuendelea kupiga muziki huku unaishi maisha mazuri au ya kuridhisha. kwa mfano wasani wanaweza kutumia pesa wanazopata kutoka katika matamsha kwa uangalifu kama kufungua biashara, kujenga nyumba za kupangisha nk. Wengine wanaweza kwenda shule na kupata ujuzi mwingine mbali na muziki, then baadae wakafanya muziki kama hoby huku wanapata mshahara kazini. Swala la umasikini Tanzania halitakwisha karibuni hivyo bei za kanda na CD zinaweza zisipande kwa miaka mingi ijayo. Ni busara kuanza kuangalia vyanzo vingine vya pesa.

    Paul Mbenna (Mr Paul)

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 21, 2010

    mtoa maoni wa pili umeelezea vizuri sana! maana hata siye wengine tuliokuwa hatuelewikwa nn thamani ya muziki hushuka kila siku! umetuelewesha kiufasaha! pia nadhan umejaaliwa busara,nakupa BIG UP ya nguvu kaka/dada.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 21, 2010

    tatizo ni kuwa na wasanii njaa wengi (bongo fleva) na kutokuwa na tungo za maana zaidi ya kuimba pipi pipiiii na malavi davi yasiyo na sababu. Kwa kweli mtu ufikiria sana kununua kanda za fleva, maana utakuta tape yenye nyimbo sita ni moja tu kidogo ina maana zingine zote zinajazia tape. Sasa eti mtu una elfu mbili ununue tape yenye nyimbo moja ya kuvutia, si bora ukaazime kwa rafiki yako aliyeliwa mapema. Na huko tunakokwenda sidhani kama fleva itakuwa na soko, na ndiyo maana kila kukicha unaona mapromota TZ wanaleta wapopo (nigerians) kuja kuimba vitu tusivyojua. Sie tunaona ujiko nigerians wanakuja TZ kumbe wenzenu (promoters) wanaua biashara yenu kwa kuwaona hamfai kibiashara.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 21, 2010

    bwana dudu mziki wako haujengi unatakiwa uwe msanii anaye elimisha jamii sio kusemana na kupigana jukwaani na mr Nice NA KUMUUA MWENZAKO KI USANII, ila pesa unazipenda. Hauna uwezo wa kuimba ila uliwazarau hata waliokushauri mia mbili kama haitoshi ACHA.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 21, 2010

    Dudu mimi nakubaliana na msemo hapo juu nazani inabidi ujitahidi kutoa nyimbo inayo elimisha jamii na iwe na mvuto utapata ongezeko kwa kazi zako.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 21, 2010

    Tanzania toka zamani wanamuziki wengi huwa wanajihusisha na fani hii kwa sababu ya mapenzi yao ya muziki na sio kujitajirisha, na ndio wengi utaona walikuwa na kazi zao nyengine na muziki ni burudani. sasa kama wewe unataka muziki iwe ndio means pekee ya kukupatia chakula basi ondoka tanzania.

    Tatizo tanzania ni soko zima la muziki, unadhani ni wangapi wanaojali kununua cd originals? kila mtu anakopi tu! unadhani ukipandisha bei ya cd ndio wanunuzi watazidi au watapungua?

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 21, 2010

    Mfumo mzima wa biashara ya muziki ni wa kutatansha sana dunia nzima. kwa ufupi mwanamuziki alie serious anakuwa na promota alie serious, anaemfanyia PR kali kwa kila cd/album anayotowa. Ni PR ndie anaemshauri muimbaji ni namna gani awe ana behave na nini wapenzi wa muziki wanachotaka kusikia na hivyo kumshauri awe anakizungumzia. PR ndio anae identify the market na kuongoza zoezi zima la targeting the market. PR huwa halali kwa kuandaa appearance na interviews za mteja wake katika vyombo vya habari na kuhakikisha anapata publicity katika sehemu mbali mbali.

    Pia tour and live performance ndio muhimu zaidi ndio zinazoingiza pesa. Muimbaji halipwi kwa kila cd ila hulipwa kwa percentage ya mauzo yote toka cd, concert, public appearances na marchandise.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 21, 2010

    jamani mnazungumza sana,Je??COSOTA
    mbona haisemi kitu??mmeazisha hiyo COSOTA ili isaidie kutetea haki za wasanii,na hatuoni kazi yoyote ya maana ya hiyo cosota,tunaomba ivunjwe na viongozi wake wawe wasanii wenye uchungu wa kusota katika fani hii,huyu bwana anayejiita mwanasheria Mr Mkinga ndiyo dikteta mkuu katika cosota,tunaombaa aondolewe haraka iwezekanavyo na hizo sheria zake za india azipeleke kwake,yeye siyo msanii yaani haelewi kabisa mambo ya sanaa.Huu wote ndio tunaita uozo
    wa systems nyingi hapa bongo.
    msanii mwenye usongo na cosota.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 21, 2010

    kwa hiyo hii ndo sababu hiliyo kufanya uache muziki na kuwa mganga wa kienyeji !! na kweli mganga wa kienyeji kwa mwaka naingiza shilingi kuliko msani wa bongo flavour!!! hata hivyo wewe dudu baya una force fan mimi sionagi unacho himbaga !!

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 21, 2010

    wewe unataka pesa hiongezeke je na nyie wa sanii mme ongezeka nini ki usanii !! kam midundo ni hile hile mna copiana kila mwana.huyu akiimba mbagala kesho mwingine hataimba kimara !! hamna mbinu mpiya vijana !! mnataka kuruka ruka tu jukwaani then mtunzwe!! mtabaki kuota !!!muoneni mwenzenu sean kingston na ubonge wake anavyo sweat jukwaani !! fanya kazi nzuri na mlipwe vizuri !! sasa nyie kabla ya hata ku perform mmeshaleo dengu!!

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 22, 2010

    Je,huyo mdau aliyeandika juu ya cosota mbona hamumuungi mkono?huu ni ukweli kabisa cosota ni uozo mtupu ,siku hizi ukippeleka kazi zako za kisanii kwenye kusaini mikataba au kuuza kazi zako unaambiwa pitia cosota,huko cosota ndiyo balaa tupu huyo dikteta Mkinga hapatikani ofisini hata mwezi mzima,sioni maana hata ya kuwa na ofisi kama hii ambayo inaliapiwa kodi kubwa,pia ubabaishaji na maswali ya kijinga
    cha muhimu ni kweli awekwe msanii
    mwenye uchungu na fani hii,iwe muigizaji,mcheza ngoma,mwanamuziki
    nk.nadhani wizara husika pia ifuatilie jambo hili kwa karibu na wasanii tusikae kimya kulea mafisadi kama huyu bwaana Mkimga.
    msanii Dar.

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 24, 2010

    MSANII DUDUBAYA, AMEJARIBU KUELEZEA NI NAMNA GANI WASANII WA AINA YOYOTE ILE WANAVYOUMIA KUTOKANA KAZI ZAO. KUUMIA HUKU NI KUTOKANA NA KIPATO KIDOGO WANACHOAMBULIA. NADHANI INGEKUWA VYEMA BADALA YA KUMSHAMBULIA MSANII MKAUONA UKWELI KWAMBA, KATI YA SH 1500, MSANII ANAPATA 100. HII 1400, INAENDA WAPI!!!!!!!!!!!!!!!. KWA TAARIFA YENU INAENDA KWA WATU WA KATI AMBAO WANAHESABIKA.
    NA HAPA HOJA HAPA SIYO HAWA WATU WA KATI, NI SERIKALI NDIYO HASWA INAYOAMBIWA AU KULALAMIKIWA NA HUYU MSANII. SERIKALI HAIONI UMUHIMU WA ENTERTAINMENT INDUSTRY KAMA INAWEZA KUCHANGIA KUONGEZA AJIRA KWA WANAINCHI WAKE. KAMA INGEONA UMUHIMU BASI INGESIMAMIA KWA KUTUMIA NGUVU ZAKE ZOTE ILI KUWAFAIDISHA VIJANA WAKE, NA PIA KUJIPATIA KODI KAMA ZILIVYO BIDHAA NYINGINE. INASIKITISHA SANA, KUNA KIKUNDI CHA WAJANJA NDICHO KINACHIMILIKI SHUGHULI HII, WANA MAPRODUCER WAO, WANA WASANII WAO (AU WANAOKUBALIANA NAO) BAHATI MBAYA RADIO NA TV NAZO ZINAINGIA KWENYE MTEGO HUO (WENYE TV WANAACHIA VIJANA WAO WAENDESHE VIPINDI, HAWA WANATUMIKIA KIKUNDI HICHI), INASIKITISHA HATA TV YA TAIFA TBC, NAYO INAFALL KULEKULE. HAIWASAIDII HAWA WAJASIRIAMALI KABISA (WASANII) ANGALIA VIPINDI VYAO. MIMI HUWA HAIINGINII AKILINI KABISA!! HAKUNA EFFORT YA KU-I-COVER NCHI YOTE, NI DAR ES SALAAM TUU.
    SASA KWA LOGIC HII NI WAPI WASAMBAZAJI HAWA WATAWEZA KUBADILIKA. SIKU ZOTE NIMEKUWA NIKISEMA TBC IACHE KUSHINDANA NA CLOUDS AU ITV ETC, IT SHOULD STAND ON ITS OWN, GUIDED WITH PRINCIPLES ZA KUWAHUDUMIA WATANZANIA, NA KUTEKELEZA ILANI ZA CHAMA KILICHOPO MADARAKANI: KWA SASA NI KUONGEZA AJIRA (MAMILIONI YA JK) SIONI UEKELEZAJI WAKE.
    WAPO KINA DUDUBAYA WENGI NYUMA YAKE. KUHUSU AINA ZA KAZI ZA WASANII WETU, HIYO PIA INATHITISHWA NA HOJA HAPO JUU, HICHO KIKUNDI NDICHO KINACHOWALISHA WATANZANIA AINA YA MUZIKI. WA HOVYO, LAKINI KILA TV NA RADIO ZINAPIGA IKIWEMO YA TAIFA. NI AIBU KUBWA. ONA KILI AWARD ILIYOPITA. THE SAME GROUP INFLUENCED EVERYTHING. KUNA NINI PALE. NI DAR TUPU, WAPI MIKOANI, WAPO WENGI WAZURI NA PRODUCTION NZURI. LAKINI UTAPITA WAPI WEWE KAMA SIYO MWENZAO?
    NI SERIKALI NDIYO INAYOWEZA KUBALI HALI HII. HAWA KINA COSOTA NA BARAZA LA SANAA NI USANII NA WALA HAWANA MENO KWA SABABU WANALISHWA NA KUNDI HILI. OTHERWISE NI USANII NA AIBU TUPU.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...