Mgeni rasmi Balozi Mwanaidi Maajar, Mbunge wa Ilala Mh. Hassan Zungu (wa pili kushoto waliokaa), Mbunge wa Muleba Kusini Mh. Wilson Masilingi (wa tatu shoto wakiokaa) na uongozi wa Jumuiya ya watanzania UK (TA) baada ya kuwasimika mwishoni mwa wiki huko Reading
Balozi Mwanaidi Maajar, Mh. Wilson Masilingi, Mh. Hassan Zungu, Ali Kiba na uongozi wa Jumuiya

Mbunge wa Muleba Kusini Mh. Wilson Masilingi akitoa nasaha zake
Prodyuza wa filamu ya Lovely Gamble Frank Eyembe akifurahia cheti alichopata kutokana na mchango wake na wa Urban Pulse anayoiongoza katika kufanikisha mambo kibao ya Jumuiya
Mdau Ben Maira akipokea cheti cha utambuzi wa mchango wake
Diwani wa Reading Mh. Richard Willis akijipatia msosi wa nguvu wa Kiafrika
Mwenyekiti wa TA Reading Mh. Banduka akiongea
Warehouse palipendeza
Balozi maajar akinadi msuli wa kimasai kuchangia TA Reading
Ali Kiba naye alikuwepo shereheni
Msanii anayekuja juu kwa kasi Francis 'Sauti ya Bongo' akitumbuiza
Msanii Damuz wa kambi ya Urban Pulse akimwaga mistari

Na Ally Muhidin wa
TZ-ONE.blogspot.com
Jumuiya ya Watanzania nchini Uingereza wikiendi ilopita iliwakabidhi rasmi madaraka viongozi wa chama hicho katika ukumbi wa The Warehouse jijini Reading. Viongozi wa jumuiya ya TA walichaguliwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwezi wa nne jijini London, Uingereza.

Jumuiya hiyo iliwaalika viongozi mbalimbali wa kitaifa na vyama visivyo vya kiserikali kuhudhulia halfa hiyo, mgeni rasmi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Bi. Mwanaidi Maajar. Katika sherehe za Jumiya hiyo huko Reading, Mh. Balozi aliandamana na Mh. Wilson Masilingi , Mbunge wa Muleba Kusini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya nje na Ulinzi, Mh. Masilingi aliambatana na Mh. Hassan Zungu, Mbunge wa Ilala , lakini pia Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge mambo ya nje na Ulinzi.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Uingereza, Dr John Lusingu, alianza kwa kumshukuru Mh. Balozi Maajar kwa kudumisha umoja na ushirikiano ambao umetokea
kupendwa Uingereza, vilevile kusaidia jumuiya pamoja na Watanzania kwa kuwakutanisha na viongozi wa serikali na vyama toka nyumbani Tanzania wanapofika hapa Uingereza katika ziara zao, kuanzia Raisi Jakaya Kikwete, Makamu wa Raisi, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Wazari Membe na viongozi wengine wa kiserikali.
Mwenyekiti, pia alitumia fursa ya ugeni huo kuikumbusha serikali kwa kupitia waheshimiwa hao kwamba Jumuiya ya Watanzania iliyopo hivi sasa ni tofauti sana na zile za miaka iliopita, kwani kwa sasa wana umoja, upendo, na ushirikiano wa hali ya juu na sasa wako tayari kuliko siku zote kushiriki kikamilifu katika kuchangia ujenzi wa Taifa kwa kupitia huduma zao, mawazo yao, kwa hali na mali.
Dr. Lusingo aliowaomba viongozi wengine wa serikali kuipa msingi imara njozi ya Raisi kuhusu diaspora ili isiishie katika majukwaa bali kuwe na tofauti zinazotambulika kutokana na mchango wa watanzania ughaibuni wingereza.
Kabla ya kuanza hotuba yake Mh. Balozi,
aliwaalika Mh. Zungu kuamkia Watanzania. Mh. Zungu alifurahi sana kuwa katika shuguli ya Kitanzania katika ukumbi uliofurika, na kupendezshwa na rangi za bendera ya taifa la Tanzania, aliwakumbusha Watanzania, kufanya kila linalowezekana kuwa na nguvu ya pamoja kuliendeleza taifa lao na kudumisha yale mambo ambayo Balozi Majaar ameyaanzisha.
Naye Mh Masilingi aliwafurahisha Watanzania, pale alipowaambia kuwa hata kama kuna sababu zilizowafanya baadhi yao kutafuta uraia wa nchi zingine, utaifa wao bado ni hazina kubwa na wajivunie utaifa wao wanaopokuja nyumbani kwani ndio kwao na hakuna Mtanzania alie na muda wa kuchunguza mambo yanayohusu uraia wao wa nchi nyingine kama hauhatarishi usalama wa Taifa.
Kuhusu hoja ya Uraia pacha . Mh.Masilingi alikiri kuongolewa baada ya kuwa na mjadala kidogo kuhusu swala hilo na baadhi ya waTanzania, isipokuwa alioonya kuwa ni vema mawazo toka pande zote za Mjadala yapokelewe kwa makini.
Naye Balozi Maajar, alimshukuru Uongozi wa TA kwa mchanganuo wake kuhusiana na jinsi Jumuiya ilivyobadilika katika muda wake hapa Uingereza, Mama Maajar huku akikatizwa mara kwa mara katika hotuba ya na wimbo Mama, Mama, Mamaa, Mama Huyo !ambao umejitokeza kuwa maarufu kama ishara ya kuuafiki umahiri wa uongozi wake na mapenzi ya Watanzania Uingereza. Aliendelea kuwakumbusha Watanzania huko Reading kuwa yote yaliwezekana kwa sababu ya ushirikiano wao. Aliwaomba Watanzania waendeleze mshikamano huo na ubalozi na hata atapokuja balozi mwingine.
Mh. Maajar aliwashukuru Mh. Masilingi na Mh. Zungu kwa kukubali kwao kujumuika na Watanzanai Reading licha ya uchovu wa safari kwani walifika asubuhi ya jumatatu. Baadaye Mh Balozi Maaja aliongoza mnada wa kuchangia mfuko wa Jumuiya hiyo Reading hii ilikuwa baada ya shuguli hiyo kusuasua. Balozi alifanikiwa kuchangisha kiasi cha fedha kisichopungua paund £300 za kingereza, na dola $50 za Kimarekani kutoka kwenye leso ya kimaasai ya pauni £20.
Katika hafla hiyo Mdau wa Urban Pulse Frank Eyembe aliahidi kuwa siku ya uzinduzi wa tamthilia ya Lovely Gamble, atachangia asilimia tano ya mapato kwa Jumuiya Watanzania Reading.
Naye Sporah show alichangia pauni £5o , Mh. Zungu Dola $100, na Mh.Masilingi Pauni $50. Mwandishi wetu Ally Muhdin wa Blog ya TZ-ONE alipowahoji wanachama wa jumuiya hiyo walisema wafurahishwa na mchango mkubwa alioutoa Balozi Maajar katika kufanikisha sherehe hizo na kuweza kuwaletea viongozi wa Kiserikali kuja kujumuika nao.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Davis (mzee ngomuo)hongera bwana.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 05, 2010

    Shelehe kweri inaonekana irifana, vyakura na hata halambee hazikuwa nyuma, japo ni kidogo lakini si haba. Kweri Mama Barozi inaerekea wewe ni mtu wa watu, maana hata wageni waarikwa hawakutaka kukosa kuhudhulia japo kwa dhalula. Ira tu nadhani hapo awari mrisema kuwa ware wagombea wa uwazili mkuu wa Uingeleza wangekuwepo na badara yake amekuja diwani,,,, rakini si haba maana naye kawawakirisha wenzake, kama ambavyo haikuwa laisi kwa kila Mtanzania arieko Uingeleza kuhudhulia kuagwa kwako. Tunakutakia safali njema Malekani. Wasalaam.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 05, 2010

    Naona Mheshimiwa Diwani wa Mji wa Kusoma kaja kuomba kura za mwisho mwisho..

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 05, 2010

    Wabongo wa UK tatizo lao kubwa ni kujisahau,Europe ni pakuchuma na wekeza kwenu Nyumbani,bado tu hamujajifunza toka kwa wenzenu wakenya,watu wapo radhi kuendelea kusafisha choo ili mradi tu anaishi majuu,na wewe Ally kiba rudisha majeshi Bongo kabla hujaambukizwa hilo gonjwa la Ulimbukeni
    Mdau wa Istanbul

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 05, 2010

    kelele zote za watu wa READING WANACHANGA LAKI SITA TU KWENYE HARAMBEE MBELE YA BALOZI?.LAKI SITA NDIO POUND MIA TATU.UKITOA PEZA ZA MHESHIMIWA ZUNGU NA MASILINGI BASI WAMECHANGA HAO WATU WA READING KAMA LAKI TATU NA NUSU AMBAYO SAWA NA POUNDS MIA NA HAMSINI.HII NI AIBU.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 05, 2010

    Ankal please you are now grown up, Haya mabo ya kina Ali Kiba kila siku kutuwekea tumechoka hivi hakuna kitu kingine cha maaana unachoweza kuweka ? Na hizi jumuia uchwara za UK kila siku tunazisikia. Come on acha hizo !!

    ReplyDelete
  7. PETER NALITOLELAMay 05, 2010

    IM VERY EXACTLY STONISHED THAT EVERY ENGLISH AMBASSADOR DIDNT STAY ENGLAND IN PROPER MANNER LIKE THIS MOM WHOM IS IN GOING TO AMERICAN OVER SEAS. I WISH HIM ALL THE BEST WISHES BY THE WAYS SHE SHOULD COME UP TO HIS HOME I CALL THEM HOME LONDON BECAUSE AFTER STAY LONDON QUIET SOMETIMES IS HOME. I AM VERY PLEASED HER JOB TO THE USA IS PURE CUMBERSOME HELP HIM GOD. MR. PRESIDENT HER DOING THE GOOD JOB IN THIS RESHAFFLE OF AMBASSADORS.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 05, 2010

    we mdau wa pili hapo juu ni mtu mzima ovyo shule yako nusu uliyosoma na kufeli bado haiwezi kukusaidia na huwezi kuwa kiongozi hata kwenye familia yako sababu unafanya mambo ya kijinga hata mtoto saa nyingine hawezi kufanya upuuzi kama wako kuandika makusudi ili kukera watu grow up na urudi shule kuiweka sawa hiyo medula oblangata yako ovyoooo!!!!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 05, 2010

    Naungana na Naritorera kwa hiro,,,,

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 05, 2010

    Nimefurahia sana mchango wa huyo anonymous wa pili!!!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 05, 2010

    Mdau wa Wed 05, 11.32 Unaishi England? Ah! Uandishi wa huo ujumbe ... sijui ni makusudi au ni vipi.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 05, 2010

    Michuzi najua na hii pia utaibania . hau sio umoja wa Watanzania wa UK . huo ni umoja wa Ex Tanzanian ( waliowahi kuwa WaTanzania ) waishio UK kwani asilimia kubwa hapo wameshaukana uraia wa Tanzania , wengine wameshapata uraia wakiingereza na wengine bado wamejiripua Kisomali, Kirwanda na Kirundi najua utabania lakini ukweli unabaki ulivyo. plz usiwe unabania comments za maana utadhani mtu ambae hukuishi aggrey.
    mdau Pakacha .

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...