Mwalimu Maua Rashidi wa Shule ya Msingi Uhuru Wasichana ya jijini Dar es salaam akiwaandaa baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo kushiriki michezo mbalimbali leo shuleni hapo wakati wa kampeni ya kutokomeza Malaria nchini yenye lengo la kuwajengea uwezo na uelewa wanafunzi wa shule hiyo kupitia michezo.
Mwanamuziki mkongwe wa Afrika Kusini Yvonne Chaka Chaka(kushoto) ambaye pia ni Balozi wa Kimataifa katika Mapambano dhini ya Malaria Duniani akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kampeni ya kutokomeza Malaria Duniani yenye kauli mbiu “Tuungane Kutokomeza Malaria” leo katika shule ya Msingi Uhuru Wasichana jijini Dar es salaam.Pamoja na na mambo mengine balozi na mwanamuziki huyo amehimiza ushiriki wa jamii nzima hasa wanafunzi kupitia shule zao kupewa elimu kuhusu Malaria kupitia michezo mbalimbali, Kulia ni Bi. Anna McCartney-Melstad Mshauri wa “Voices for Malaria Free Future II – Tanzania kutoka Chuo cha Afya ya Jamii Bloomberg.

Meneja Mkuu wa Kiwanda cha kutengeneza nguo cha mkoani Arusha cha A to Z ambacho pia kinatengeneza vyandarua akijibu baadhi ya maswali kutoka kwa waandishi wa habari kwa kushirikiana na Bi. Yvone Chakachaka namna kampuni ya A to Z inavyoshiriki katika kampeni ya kutokomeza Malaria kwa kutengeneza vyandarua bora na vyenye viwango leo wakati wa kampeni ya kutokomeza Malaria kupitia michezo kwa shule za Msingi iliyofanyika shule ya Uhuru Wasichana jijini Dar es salaam. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 03, 2010

    ha ha ha malaria toka mwaka 1965 tunapambana nayo ha ha ha better give up fighting it and start to defend against it.

    au tuwaachie wachina wapigane nayo manaake si hatuwezi kitu bwanaa.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 04, 2010

    Uliye-comment wa kwanza huna akili,ndio nyie nyie kila kitu lazima ubishe

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 04, 2010

    Huyo Dada aliyevalia mawani ya steav wonder imekuwaje tena? kazi kweli na hisi kama sio mahali pake any way yupo mzungu hapo labda dada anataka muzungu amuone yupo babu kubwa kimaendeleo

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 04, 2010

    kuna hili tangazo la malaria linalotolewa katika luninga zetu,hivi kile kiinglishi nani anakielewa?maana malaria inatusumbua sie wa hali ya chini na kiinglish zero kabisa!!

    yani ni tangazo ambalo wazungu gani sijui uko wanaliongelea na unajua kiinglish chao sie kapa

    badilisheni lile tangazo

    na dawa ya malaria sio NETI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...