fundi mitambo akiweka mambo sawa kwenye kifaa cha kisasa cha kuoneshea sinema katika viwanja vya nje usiku wa kuamkia leo kabla ya gemu la brazil na korea kaskazini. Kampuni ya AfriCinema imekuwa ya kwanza kuleta mtambo huu wa kisasa ambao unafaa sana kwa kuonesha sinema za mafunzo ama kampeni sehemu yoyote ili nchini kwani una umeme wa kujitegemea wa jenereta. kazi kwenu mapromota na waendesha kampeni za mafunzo na biashara
Kitambaa maalumu cha kuoneshea sinema nje ambacho ni kikubwa kuliko vyote nchini na huonesha picha kwa ubora wa hali ya juu. kitambaa hiki chenye urefu na upana wa futi 30 husimikwa kwa kujazwa upepo.

Maendeleo ndiyo furaha yetu.
ReplyDeletewe toka hapo unatuziba bwana.
ReplyDeleteHawa jamaa hatimaye wameanza, nimewakisia tangu mwaka jana, hongereni!
ReplyDelete