Ticha Fred Alfred Rwechungura kazini

Siku hizi kuna wanafunzi, wanataaluma na watafiti wengi kutokana na hali ya umasikini unaozikumba nchi zetu na hasa vyuo vikuu vyetu, wanakosa au hawapati vyenzo muhimu za kusoma kama vile vitabu na majarida mbalimbali na kuwafanya wakomae katika nyanza zile wanazo somea.

Kwa kugundua hilo, mdau Fred Alfred Rwechungura ambaye ni mwalimu katika chuo kikuu cha Mzumbe, Morogoro, katika idara ya Uchumi, na mbaye ni mtaalam katika masuala ya uchumi miradi, hivi sasa akimalizia kula nondozzzz yake ya PhD yangu ya Uchumi katika chuo kikuu cha Bradford Universityy nchini Uingereza, ameamua kuanzisha Libeneke kwa ajili ya watu kama hao yaani wanafunzi wa vyuo vikuu na watafiti mbalimbali kutoka mashirika au serikalini maadamu awe anashughulika na masuala ya utafiti na masuala mengine yahusuyo uchumi na miradi kwa ujumla.

Libeneke lake linakwenda kwa jina la
www.fredalfred.blogspot.com.

Ticha Rwechungura kaiambia Globu ya Jamii leo kuwa Libeneke lake litafanya kazi kama blog yoyote ile, ambapo watu wataweza kutuma michango yao mbali mbali inayo husina na masuala ya kitaaluma na utafiti. Vile vile wadau wataweza kutuma masuala mbalimbali yanayo watatiza katika masuala ya uchumi, miradi ( kama kupanga, kuanzisha na kusimamia/kuendesha miradi) na suala lolote linalo husu utafiti katika hatua (level) yoyote ile. Kwa sasa mdau akiingia na asipate kile anachokitafuta asikate tamaa. Anaweza kutuma ujumbe wa kitu gani alikuwa anakitafuta au alitaka asaidiwe.

Ticha huyu anaahidi kuwa hii itakuwa ni njia au furusa moja wapo ya kuwafanya watanzania, wanataaluma na watafiti mbali mbali kufaidika na TEKNOHAMA, akiitaja kuwa kwa njia hii elimu inaweza kuwafikia watu wengi na kwa wakati mmoja na kwa kila mtu mahali alipo bila kuingia gharama sana, mbali na kukaa madarasani na kumsikiliza mwalimu.

Wanataaluma, watafiti na watanzania wote kwa ujumla, mtatuzi wa matatizo yaliyokuwa yanakukabiri amefika kwenye ncha ya vidole vyako, mtumie naye atakusaidia kufika ulikotarajia kufika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 10, 2010

    Hongera sana mdau kujiunga katika libeneke la kublog. Tuendelee kuwa pamoja.
    Zemarcopolo...

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 10, 2010

    inapendeza, tutakutembela tu mdau.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 10, 2010

    jamani kama mnaanzisha kitu muwe sirias sasa cheki ankali najuhudi zoote za kutuwekea apo tunafungua link kupe hakuanna kitu sasa mnaongeza nafasi bwana ya matukio mengine .......kaka fred sijui jiandae kwanza poa tuuuu ata kama tabaniwa kurushiwa hii koment yangu lakin mimi ujumbe nimefikisha tayari ......inatia aibu tunafungua blog kwa shauku kubwa inasema The blog you were looking for was not found. returnnto blogger......ok tuonane muda mwingine

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 10, 2010

    Naamini kuwa april mosi imeshapita, sasa kwa nini mtu mzima na elimu yake yote aliyonayo ameamua kutufanya wajinga na kutudanganya hapa? kwa nini lakini mtu wa elimu kama yako unatupa matumaini yasio ya kweli na kutupotezea muda wetu? hujui kama wengine tunalipa kupata hii huduma ya internet?

    link hii www.fredalfred.blogspot.com ukiifuata unakuta kuwa haiexist.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 10, 2010

    Ankal ni vizuri Huyu bwana akawa serious na anachokifanya na pia anachokiandika!!! Ni vizuri ajue anaandika nini!! Kwanza anaposema kwa watafiti hajawa wazi ni huduma gani ya kitafiti ambayo watafiti wanaweza kuipata ktk blog Yale na ni kwa watafiti wa maeneo gani? Je ni natural science researchers, social science researchers, engineers au kina nani. Anataka kutuambia kuwa mtafiti wa mambo ya miti na misitu, au mtafiti wa mambo ya baharini na viumbe maji, au mtafiti wa mifugo, au mtafiti wa uchumi wa kihesabu na kitakwimu(econometrics) nakadhalika wote watapata huduma wanauotaka kwa maenea yao ya utafiti??? Mi naona anakurupuka tu na kudhani ni rahisi!! Pili hasema ni huduma zipi sasa atatoa je za kiushauri, je ni huduma za kuwapatia takwimu(data) watazohita kwa tafiti zao, je ni huduma ya literatures kwa studies zao, nk au ni nini? Na Kama ni hivyo basi atawezaje kuhudumia Nyanja zote za utafiti namaanisha kwa mfano Mimi nafanya natural experiments labda ktk soil sciences mwingine anafanya something ktk maisha ya majini mwengine yeye ni mtafiti ktk psychology, socialogy, political science, mathematical medelling sasa anawahudumiaje watu wa maeneo hayo mbalimbali??? Ni Kama hajui anatutangazia nini!!! PILI, hii uchumi miradi ni nini?? Hakuna field Kama hiyo Katina uchumi tusidanganyane bwana!! Project economics?? Anaweza kutuambia aliisomea wapi hiyo degree ya uchumi ambapo alispecialize katika project economics??? Hiyo degree inaitwa project management na huo sio uchumi!! Huwa kuna regional economics, labor economics, international econ, emperical econ, financial econ, environmental econ, agricultural econ, and the like, sasa hii ya project economics ni Kali na ni mpya kwanza haipo!!!! Halafu michuzi samahani Mimi Huyu bwana nafahamu degree yake ya kwanza ni BSc Forestry kutoka Sua, masters ni ya Project Management kutoka Brsdford Uk, ni ajabu kusikia yeye ni mtaalam wa mambo ya uchumi!! si kweli. Anyway samahani bwNa michuzi Kama nimekukosea wewe au huyu bwana lakini nafahamu kuwa Phd anayoifanya sio ya uchumi!!!

    ReplyDelete
  6. Thats gud thing congrats

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...