Mfanyabiashara mashuhuri na mkereketwa wa siku nyingi wa klabu ya Yanga Davies Mosha ameahidi kuleta mabadiliko makubwa kwenye klabu hicho cha Jangwani endapo kama atachaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wake.
Akiongea na Globu ya Jamii, Mosha amesema iko haja ya kuwepo kwa uongozi utaopeleka maendeleo kwenye klabu, na kuendeleza yale mazuri yote yaliyoanzishwa na uongozi uliopita. Vile vile amesisitiza haja ya kuendesha klabu kwa njia zaa kisasa ikiwa ni pamoja na kubuni na kuimarisha vitega uchumi mbalimbali ambavyo vimekuwa havifanyiwi kazi.
Amemsifia sana mfadhili mkuu wa Yanga, Bw. Yusuf Manji, kwa jitihada zake za kuiendeleza klabu hiyo na kuongezea kuwa mkakati wake mkubwa utakuwa ni kuhakikisha kwama uwanja wa Kaunda unakuwa wa kisasa na wenye kutumika muda wote.
Kubwa jingine analopania kutekeleza ni kuhakikisha wanachama wote wanajiunga pamoja na kuleta maendeleo na pia kuhamasisha upatikanaji wa wanachama wapya ili klabu iendelee kuwa na nguvu zaidi
KILA LA KHERI KAKA DAVIES MOSHA KIUKWELI UMETUPA FARAJA SANA KWA KUJITOKEZA KUGOMBEA KUIONGOZA TIMU ULIYOIPENDA TOKA UKIWA SHULE SIKU ZOTE TUMEKUA TUKIPIGA KELELE KWAMBA WADAU WENYE VISION WAJITOKEZE KUIONGOZA YANGA,YANGA YA SASA INAHITAJI WATU WAPYA WENYE MAWAZO MAPYA,WEWE UMEIFANYIA MENGI YANGA UKIWA NJE SASA TUNAKUOMBEA UINGIE NDANI ILI UWE NA WIGO MPANA ZAIDI WA KUTOA MCHANGO WAKO,KARIBU YANGA KAKA
ReplyDeleteSafi sana,haya ndio mambo tunayotaka kusikia,yanga inahitaji watu kama nyie,sijapiga kura siku nyingi kuchagua viongozi wa yanga,lakini safari nitajitokeza kutumia haki yangu ya kidemokrasia,ila chondechonde kaka ukiingia katika uongozi jiweke kando na watu wanaoitwa MAKOMANDOO,ambao kifukwe yeye hupenda kuwaita eti TAUSI WA IKULU,utapoteza umaarufu wako ndani ya YANGA mapema.
ReplyDeletemakubwa gani kwa mpira upi labda sanaa
ReplyDeleteDavies Mosha + Yusuf Manji=Yanga Company Limited. Kila kheri Yanga, hawa jamaa najua wanakoipeleka Yanga. Historia ni mwalimu wa kweli..
ReplyDeleteWE ANON UNAYESEMA YUSUF MANJI + DAVIS MOSHA=YANGA COMPANY LTD,ACHA WIVU WA KIKE,UNADHANI HIZI TIMU ZITAENDELEA BILA KUENDESHWA KIBIASHARA?HEBU ITAZAME AZAM ILIYOANZISHWA MIAKA 3 ILIYOPITA THEN FANANISHA MAENDELEO YAKE NA HIZI TIMU ZINAZOITWA KONGWE....MPIRA WA SASA NI LAZIMA UITE WATU WAWEKEZE,ACHA MAWAZO MPAUKO THINK POSITIVE ALWAYZ
ReplyDeleteHongera Mpiganaji Davies Mosha,naona Watani zetu Simba wameshaanza kuweweseka humu ndani,wanakujua jinsi ulivyokuwa unawalaza mapema na MORO UNITED yako enzi ziiiile,sasa wanajua dozi zile utazihamishia YANGA,na wataipata safari hii hakutakua na mamluki watakaojipenyeza uongozini Yanga.
ReplyDeleteNakuunga mkono Davies kwa hilo la kuhamasisha upatikanaji wa wanachama wapya,haiingii akilini eti klabu kubwa kama yanga yenye mtandao wa mashabiki uliosambaa mpaka vijijini kuliko hata vyama vya siasa eti kusikia kati ya mamilioni ya wapenzi wake hao eti ina wanachama wasiozidi 1500!shame!kwa hiyo ukiingia madarakani usilewe madaraka,itekeleze ahadi hii wengi nikiwamo mimi nitakupigia kura kwa ahadi hii tu kwa kuwa sikufahamu sawasawa ila umenigusa kwa hilo,mengine tutajuana mbele ya safari
ReplyDeleteLOYD NCHUNGA+DAVIS MOSHA+YUSUF MANJI-IMANI MADEGA=YANGA MAENDELEO
ReplyDeleteBaba Elisa hebu acha fujo.....
ReplyDeletelooo hii mtu ina hela chafu sana huyu ataleta maendeleo hana dhiki kabsaaa, tumpe kura ya ndiyoooooooooooooooooooooooooooo
ReplyDeleteFrom Kenya,
ReplyDeleteYour dedication to duty will help fulfill the goals and aspirations of the Club. This will definitely go a long way towards raising the young messi's of Yanga. All the best to you! LISA footballers of Kenya support you, Big up to you kaka!
huyu jamaa ni kijana mwenye pesa sana na ana mapenzi ya kweli kwa yanga! yaani Davis hata haitaji kupinga kampeni, yanga tunamhitaji sana. sasa ni wakati wetu wanachama kuamka na kuchagua watu wanaofaa sio wapiga kelele
ReplyDeleteHongera Davis Mosha tupo pamoja na wewe