Mdau Constantine Thobias na mai waifu wake Nelly Sembuli wakipozi baada ya kumeremeta katika 'Mlima Kilimanjaro' uliopo katika eneo la Export Processing Zones (EPZ) lililopo Ubungo External jijini Dar wikiendi ilopita. Bw. Harusi anafanya kazi Parapanda na Bi. Harusi yuko katika kampuni ya Uzibora Maharusi wakipozi na familia
Maharusi wakiteremka wakati familia ikiwa kileleni 'Kibo'

Mandhari ya mfano wa mlima kilimanjaro uliojengwa ndani ya eneo la EPZ
Panapendeza
Bustani mwanana ya EPZ ambayo pamoja na mfano wa mlima kilimanjaro pamekuwa kivutio kikubwa kwa wadau ambao kwa sasa wanaruhusiwa kwenda kupiga picha za sherehe mbalimbali kwa mchango mdogo wa shilingi 10,000/- jambo ambalo limesifiwa na wengi kwani angalau kuna mbadala wa sehemu ya kupigia picha ukiondoa kwenye fukwe za bahari








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 30, 2010

    kwa wastani sehemu kama hizi zingekuwa nyingi hapo bongo maana kweli muonekano wa kwenye picha hii kweli panapendeza

    na hii ni biashara kubwa hapa uchinani maana wanasehemu kama hizo kibao yao.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 30, 2010

    jamani ni pabaya.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 30, 2010

    Hahahaha ama kweli hii ni Tanzania hapo ndio kituo ambacho kimegharimu mamilioni ya pesa kwa ajili ya kukuza mauzo nje..kimekuwa studio ya maharusi..where are we going..na hisi hii ndio iliyomfanya JK amwambie Dr Meru thinking does not need money..Kesho kwenye bajeti ya wizara ya Viwanda bishara na Masoko inabidi taasisi hiyo itoe taarifa ya mafanikio ni harusi kadhaa zimepiga picha ktka eneo hilo badala ya what Tanzania has managed to export.Mimi haya mambo yananiumiza zana kaka michuzi...Usinibanie tafadhali

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 30, 2010

    I really likethis. Huyu aliyeanzisha hii kitu nampa mkuu na mkono...Wow! this is so nice. Unajua kuna wengi hata Moshi hawajafika na hata kuuona huo mlima hawajauona. Na kwenye magazei au sehemu zetu nyingi wala hatuutangazi kama ukienda Kenye na kuona picha mjini zinaonyesha huo mlima...


    Love it

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 01, 2010

    Nashauri hapo mahali pasitumike kupiga picha za harusi. Ni kweli panapendeza katika kuweka kumbukumbu lakini sidhani kama ilikuwa ni lengo la walio patengeneza kuwa patakuwa kituo cha watu kwenda kupigia picha za harusi. Tufunguke mawazo jamani. Itakuwa kila jumamosi ni bugudha tupu pale tarumbeta, ngoma wakati ni sehemu yenye umuhimu wake kiuchumi.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 01, 2010

    Aibu ..hapandio pa kupigia picha jamani? Watu wameona hivi utaona sasa watakavyokuwa wanajaa pale jumamosi kuwekeana zamu za kupiga picha za harusi.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 01, 2010

    Ni pazuri, let those wanapiga picha waendelee kufaidi vya nchi yao. Kilimanjaro washindwe kwenda, hata hapo External napo wasiende. Angeenda mzungu kupiga picha pale mngesema, tehe tehe tehe wathungu wanapapenda, wameenda wabongo mnachonga. Sasa mbona hamkuchonga mlipoona wakuu mbalimbali walipotembela hapo na kupiga picha. Au nitofautishiekati ya mtu kutembelea hapo na mtu kupigia picha. Wabongo acheni hizo, kizuri chochote cha nchi tutumie ilimradi tu hatukidhuru. Ukitaka pasitumike kupigia picha basi hata na viongozi wa nchi nao wasiende kupagia picha.
    Ila sioni mantiki ya katazo hilo, acha watanzania wafurahie utalii wa ndani, acheni ushamba

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 01, 2010

    Mkimaliza kupiga picha tujulisheni, sie wakenya na waganda tunatafuta maeneo kama hayo, kwa udi na uvumba ili tuje kufanya bishara hapo za kufa mtu!! Sawa?? Msije kukasirika lakini eh, maana inaonekan wazi kwamba 'kwenye miti......hakuna wajenzi" kweli au uongo????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...