Ombi la Chama Kuchangia
Uchaguzi Mkuu wa CCM Oktoba 2010
Ndugu Mzalendo,
Kwa heshima na taadhima ya dhati tunayo furaha ya kukuarifu kuwa, Mwenyekiti wa CCM taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amewaomba wanachama wote wa CCM na wasio kuwa wanachama lakini wenye mapenzi mema na Tanzania ,kukichangia chama katika uchaguzi mkuu ujao baadae Oktoba mwaka huu.
Halmashauri kuu ya CCM United Kingdom katika kikao chake cha Mei -1- 2010, kiliunda kamati maalum ya kusimamia na kutekeleza ombi la agizo hilo.
Kwa hivyo basi ,kwa uzalendo wako kwa taifa lako Tanzania na watu wake,tunaomba mchango wako kwa kiasi chochote utakachojaliwa nacho na tunakuahidi kuwa mchango wako utawasilishwa moja kwa moja Makao makuu ya Chama Dodoma wakati wa mkutano mkuu wa chama ambapo viongozi wakuu wa CCM United Kingdom watahudhuria na kuwasilisha mchango wako huko.
Shime wana Ndugu, Mzalendo tushikamane katika kutekeleza ombi hilo la Mwenyekiti wa chama taifa kizalendo ili tuonyeshe kuwa kweli tupo imara kutoa mchango kwa taifa letu.Tunaomba mchango wako uwe umeifikia kamati kabla ya mwisho wa mwezi wa sita, ili michango yote ya wapenda CCM iwasilishwe Dodoma katikati ya mwezi Julai.
Unaweza kuwasilisha mchango wako moja kwa moja katika Akaunti ya CCM UK ambayo ni;
Benki: Lloyds TSB (UK)
Branch: Market Place, Reading
Jina la Akaunti: Chama Cha Mapinduzi
Akaunti Namba: 0587300
Sort Code: 30-96-96;
IBAN NUMBER: GB75 LOYD 309696 9600 5873 00
*Tafadhali andika jina lako kama reference ili tuweze kukuandika katika orodha ya watu waliojitolea ambayo itapelekwa Makao Makuu Dodoma.
“MTU KWAO:Watanzania tuna jukumu la kuijenga Tanzania popote pale tulipo”
Imetolewa na Wanakamati;
Hassan Hafidh – Mwenyekiti wa Kamati - 07536497772
Lilian Barongo - 07525175337
Mariam Mungula - 07770910901
Tunatanguliza Shukrani za dhati.
Ndugu Mzalendo,
Kwa heshima na taadhima ya dhati tunayo furaha ya kukuarifu kuwa, Mwenyekiti wa CCM taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amewaomba wanachama wote wa CCM na wasio kuwa wanachama lakini wenye mapenzi mema na Tanzania ,kukichangia chama katika uchaguzi mkuu ujao baadae Oktoba mwaka huu.
Halmashauri kuu ya CCM United Kingdom katika kikao chake cha Mei -1- 2010, kiliunda kamati maalum ya kusimamia na kutekeleza ombi la agizo hilo.
Kwa hivyo basi ,kwa uzalendo wako kwa taifa lako Tanzania na watu wake,tunaomba mchango wako kwa kiasi chochote utakachojaliwa nacho na tunakuahidi kuwa mchango wako utawasilishwa moja kwa moja Makao makuu ya Chama Dodoma wakati wa mkutano mkuu wa chama ambapo viongozi wakuu wa CCM United Kingdom watahudhuria na kuwasilisha mchango wako huko.
Shime wana Ndugu, Mzalendo tushikamane katika kutekeleza ombi hilo la Mwenyekiti wa chama taifa kizalendo ili tuonyeshe kuwa kweli tupo imara kutoa mchango kwa taifa letu.Tunaomba mchango wako uwe umeifikia kamati kabla ya mwisho wa mwezi wa sita, ili michango yote ya wapenda CCM iwasilishwe Dodoma katikati ya mwezi Julai.
Unaweza kuwasilisha mchango wako moja kwa moja katika Akaunti ya CCM UK ambayo ni;
Benki: Lloyds TSB (UK)
Branch: Market Place, Reading
Jina la Akaunti: Chama Cha Mapinduzi
Akaunti Namba: 0587300
Sort Code: 30-96-96;
IBAN NUMBER: GB75 LOYD 309696 9600 5873 00
*Tafadhali andika jina lako kama reference ili tuweze kukuandika katika orodha ya watu waliojitolea ambayo itapelekwa Makao Makuu Dodoma.
“MTU KWAO:Watanzania tuna jukumu la kuijenga Tanzania popote pale tulipo”
Imetolewa na Wanakamati;
Hassan Hafidh – Mwenyekiti wa Kamati - 07536497772
Lilian Barongo - 07525175337
Mariam Mungula - 07770910901
Tunatanguliza Shukrani za dhati.
Jamani nyie CCM wenzangu, mnatutia aibu ya kuombaomba kama Matonya. Tumekuwa hatujulikani tukishiba wala tukiwa na njaa.
ReplyDeleteMbona sijawahi kusikia wana-CCM katika nchi nyingine wakitembeza mabakuli namna hii, TUSEME NA NJAA ZETU.
Swali, hivi shughuli za kisiasa zinaruhusiwa ukiwa ugenini hata kwa vyama vingine? Hapa nina maana mbili; Tanzania inaruhusu na nchi hizo hasa UK zinaruhusu?
ReplyDeletemhhhhh halmashauri kuu ya CCM - UK....ipende inji yako......tuitikie wito wa mwenyekiti wa CHAMA kuonyesha uzalendo kwa inji TANZANIA.....kazi kweli kweli!! ndugu zetu wa UK muwe mnasoma soma hata habari za nyumbani muweze kuwajua wazalendo..haya yana mwisho haya alisema ngoswe.....
ReplyDeleteHIVI NYIE WATANZANIA WA MNAOISHI UK HALAFU MNAFANYA SIASA ZA CCM MMEKOSA VITU VYA MAANA VYA KUFANYA? KAMA MNATAKA KUFANYA SIASA RUDINI TANZANIA KULE.
ReplyDeleteBora pesa yangu nimpe Ombaomba akanywee pombe kuliko niichangie CCM, Hell to the NO.
ReplyDeleteMmekosa kazi!
ReplyDeleteMdau Bradford
Baada ya umaskini wote mnaotutia na kulea mafisadi wenu bado tuwachangie????
ReplyDeleteKopeni kwa Manji na Lowasa. Leave Tanzanians alone
Juu ya nini nichangie CCM?
ReplyDeleteWatanzania wenzangu mnaoishi nje mnajua fikakuwa nchi yetu ni masikini ya kila kitu nashangaa mnataka kuchangia chama baada ya kuchangia maendeleo ya nchi yenu kwa mfano kama mnaangalia habari za nyumbani kupitia Tv kuna shule mkoa wa Tanga wanafunzi asilimia 95 wanaenda shule bila hata marapa pia chakula wanapa mlo mmoja au siku inapita msione nyie huko mnakula vizuri wenzenu huku mambo magumu afadhali ya jana. kama kweli mnamapenzi mema na nchi yetu basi wasaidie ndugu zenu wanaotabika huku Tanzania kuliko mtoe pesa ziende kwa watu wenye vitambi mtelezo.Msinichukie hayo ni mawazo tu.
ReplyDeleteHivi ni lini sisi watanzania tutaamka na kuwa na mawazo jengevu na yenye mwelekeo wa kujiinua?sasa kama nyinyi muliokuwepo Abroad munaendelea kuwa na mawazo sawa na mwanakijiji wa Bongo,na sisi huku tufanye nyinyi.
ReplyDeleteAchaneni na mambo ya siasa,tupeni mwanga katika biashara,elimu,afya,teknolojia na maendeleo kwa ujumla,jifunzeni kutoka kwa jamii nyingine za waafrika huko Uk
mdau Tanga
kachukueni za EPA tena.
ReplyDeleteNilivyokuwa nasema Watanzania UK wapewe ushauri nasaha hamkunielewa.
ReplyDeleteNdiyo maana kila mtu anakimbilia UK, wabunge, mawaziri, nk.
Badaya ya kuwashauri hao diaspora wapeleke hela zao nyumbani kuwasadia familia zao na nchi yao mnachangisha hela kwa ajili ya politix.....
NADHANI NI JAMBO JEMA KUCHANGIA JAMBO JEMA NA LILILO NA MASLAHI, LAKINI HILI NALIANGALIA KWA MTIZAMO MPANA ZAIDI. NINAVYOJUA MIMI, WATANZANIA WAISHIO NJE HUUNGANISHWA NA UMOJA WAO AMBAO HAUONGOZWI NA MITIZAMO YA KISIASA, KIKABILA, KIDINI, RANGI AU UWEZO. WANAONGOZWA NA UTANZANIA WAO. KILA MMOJA AKIACHWA AAMINI ANACHOPENDA KWA NAFASI YAKE NA WALA SIYO ORGANIZED KWA KIASI HIKI. SASA HIVI KUMEANZA KUJITOKEZA KUANZA KUJIORGANIZE KIVYAMA, BAHATI MBAYA SANA NAONA NI CCM ZAIDI. SIJUI KWANINI! NA BALOZI ZETU NADHANI ZINARIDHIA HILO. LAKINI WASIWASI WANGU, HALI HII HAITAISHIA KWA CCM TU. ITAKWENDA KWA VYAMA VINGINE, UDINI NA HATA UKABILA AU FAMILIA WANAZOTOKA. HAPO KUTAKUWA HAKUNA UMOJA TENA, KITU KINACHOWEZA KUSABABISHA MISUGUANO, KUSUSIANA, KUJITENGA, NA HATA KUONYESHANA UBABE.
ReplyDeleteSISI TUNAUMOJA WETU HAPA, TULIWEKA WAZI KABISA KWAMBA SIASA, UKABILA NA UDINI HAURUHUSIWI. ISIPOKUWA MWENZETU KAMA ANATAKA KUFANYA SIASA, IWE KWA CHAMA CHOCHOTE HATUMTENGI. TUTAMUUNGA MKONO KWA DHATI. NA TUNAO WENGI WAMEFANYA HIVYO NA NI FURAHA MUDA WOTE.
NADHANI IKO HAJA YA KU DISCOURAGE HALI HII KUKINGALI MAPEMA. ITAWASAMBARATISHA WATANZANIA MLIOKO NJE.
Wafadhili wamekataa kuchangia budget yetu kutokana na kukithiri kwa Rushwa, ufisadi katika awamu hii ya nne...sasa, why should I contribute, my hard-earned money to the party that has failed miserably in circumventing Tanzanians' problems. It's only a fool who will throw his/her money into the sewer.
ReplyDeletewabongo wamechoka kufikiri. sasa wanaona siasa ndio deal! hata wakipata exposure bado wanafikiri siasa ndio kimbilio lao. duh! aibuuu? yaani hawa wanaojifanya CCM-UK wamepoteza kabisa ramani ya wanakotaka kwenda.
ReplyDeleteKwa maoni yote hapo juu, CCM imekalia kuti kavu, kama wangeruhusu uchaguzi wa huru na haki. WaTZ yaelekea wanataka "change"tatizo ni namna ya kuipata. Mie nitawachangia CHADEMA nao watuoneshe njia. Ni mtazamo wangu!
ReplyDeleteMdau Leeds.
Watanzania, hivi utakuwa ni uchaguzi mkuu wa CCM au uchaguzi mkuu wa kuchagua madiwani, wabunge na rais (Serikali)? Kwani hata kama kampeni watakayopiga CCM ni lazima tuwachague wao? Nanyi wasomi wazima eti uchaguzi mkuu wa CCM!! Ndivyo mlivyoambiwa au mnavyoambiwa na viongozi wa CCM wakija huko Ukerewe kuwa ni uchaguzi mkuu wa CCM? Au ndo nanyi katika kupigia upatu CCM?
ReplyDeleteVyama vyote vitasimamisha wagombea, siyo CCM tu.
Sasa nawafundisha, semeni UCHAGUZI MKUU WA KITAIFA WA SERIKALI 2010. Siyo CCM tuu, mnasikia?
Wote wanasikilizia dili. Mnapoteza muda bure hakuna mtu atakayewapeni vyeo eti kwa sababu mnaongoza tawi uk. Huko bongo kwenyewe vumbi linatimka. Wakati wa watu kutoka nje kwenda kuzoa vyeo umepita, ndio maana unaona hata watoto wao wanabaki bongo ili wajichukulie vyao mapema. Fanyeni kazi kwa juhudi wandugu
ReplyDeleteKujiunga na Chama ama kukuchangia vyite ni hiari. Asiyetaka kuchanga halazimishwi: sasa hayo maneno mengine yote yasiyo ya msingi yanini? Wanaoinga mkono CCM wana uhuru kabisa wakusaidia chama chao kama walivyo wenye mapenzi na vyama vingine vile. Hima wana CCM!Hongera Wanza CCM Uingereza! Nyie mfano wa kuingwa.
ReplyDeleteTANGAZO.
ReplyDeleteEwe mTZ mpenda maendeleo na mabadiliko.Kama mwanachama,nakuomba popote pale ulipo iwe Urusi, China, UK, US, TZ, Kenya etc. Onesha uzalendo wako kwa kukichangia chama chako cha CHADEMA kikutumikie kwa maendeleo ya taifa letu.
Hakuna kulala 'mpaka kieleweke'
Kuelekea uchaguzi mkuu, tutegemee matangazo kama haya.
HII NI LAANA!!!
ReplyDeleteHIVI KWELI BADALA YA KUSEMA TUCHANGIE MAYATIMA NA WALEMAVU NA WATU WENYE SHIDA WANAOISHI KATIKA UMASKINI WA KUTISHA Tanzania, KWELI TUNADHUBUTU KUITANA ETI KUCHANGIA CCM????
HIVI KWELI HAWA WATU WANA AKILI TIMAMU???
WANA ROHO YA UKATILI NA UFISADI NDIO MAANA HAWAONI KAMA HILI JAMBO NI LA AIBU NA KUSIKITISHA.
MUNGU AWAREHEMU!!!!
LLANA KUBWA HII INATAKAKUANGUKIA TANZANIA...WEEE TANZANIA WEE NAKUPENDA KWA MOYO WOTE..IEPUSHIE NA HILI BALAA LA HAWA WAUZA UNGA WA UK...
ReplyDeleteSASA NATAKA KUAMINI LILE WAZO LA YULE MTANI WETU WA JADI KUTOKA MOMBASA KUWA WATZ WALIO UK NI WAUZA UNGA..YAANI VICHWA VYAO HAVINA AKILI KAPSAAA KAPSAAAA!!!..
MWALIMU ALITUASA NA TUKASIFIWA TUKIWA NJE YA INJI SIE WOTE NI WATANZANIA..MBONA MNATUTIA AIBU? HUKO MLIKO HATA TV HAMUNA? UMEONA WAPI MWINGEREZA AU MMAREKANI AKAPEPERUSHA BENDERA YA CHAMA UGHAIBUNI??? MMECHANGANYIKIWA OOH MY GOOOOddd!!
SASA NAWAPA USHAURI, HEBU TAFUTENI AKAUNTI YA MSELA MWENZENU CHENGE, ALILIIBIA TAIFA HELA ZA RADA BRITISH AEROSCOPE ZAKE AKAZIWEKA HUKO HUKO MLIKO. MUANDIKE BARUA BENKI MZIDROO HALAFU MUMTUMIE MAKAMBA.
NADHANI KUNA HAJA YA KUWASCRUTINISE VIZURI. INAWEZEKANA MNATUMIA DIPLOMAT PASSPORTS KUPITISHA UNGA MAANA NASIKIA MMEIFANYA TANZANIA KUWA HUB YA UNGA EAST AND CENTRAL AFRICA.CHANGIENI SHULE, MAHOSPITALI BARABARA NA MFUKO WA ELIMU YA JUU MAALUNI WAKUBWA NYIE!
nilitaka kumsihi michuzi awabane maana mnabana nafasi kwenye blogu yetu ya jamii lakini nadhani ni vema awaachie muendelee kuleta mapicha yenu ili tuwaingize kwenye sensa ya wapumbavu..hivi wangapi mmeoa? mna familia? mnamajukumu kweli? na hao maafisa wa ubalozi waliogeuza ofisi za ubalozi kuwa za chama JIREKEBISHENIIIIII!!! SIO AKILI MNACHOFANYA!! FAHARI MAMA WA UJINGA!!
ACHENI KUDANGANYANA HUKO KWENYE VIKAO VENU MNAVOKAA NA KULA BROILA NA JUICI ZA UNGA, NJOONI NYUMBANI MJENGE TAIFA, SIKU HIZI MADINI KILA SEHEMU TUNACHIMBA, MIRADI KILA KUKICHA...KAMA WAJANJA SI MTUMIE HIZO HELA MLIZOIBA KUWEKEZA KWENYE MAKAMPUNI YA WAJENZI MNAACHIA WACHINA KILA SEHEMU WAMETANDA!KELBU WAKUBWA NYIE!
European Union must be interested in this, tafadhali wapelekeeni bakuli....
ReplyDeletesafari hii uchawi umevuka bahari mmelogwa nyinyi si bure he!
ReplyDeleteNdugu zangu wa hapo london,mimi ni mdau naishi hapa uk Bradford hivi jamani kwanini msianzishe mchango kusaidia mashule,hospital au vituo vya kulelea yatima ?,hiyo ccm inapewa sh bilioni tatu kila mwezi na serikali kwa sababu vyama vyote vyenye usajili wa kudumu na kina wabunge hulipwa pesa kila mwezi,inategemea na idadi ya wabunge uliyonayo,sasa tuwape mchango wa nini jamani??
ReplyDeletetuacheni "UNAFIKI NA KUJIPENDEKEZA KUSIKOKUWA NA MAANA"
NI MIMI MDAU UK BRADFORD WESTYORKSHIRE
Kama nina $$ za sadaka bora nikawape watoto yatima kulipa kuwapa hawa wa 'vijisenti'.
ReplyDelete(US Blogger)
pOLE NA KAZI BWANA MICHUZI, NAOMBA KUWAJUA HAWA JAMAA, HUKO UK WALIKO WANAFANYA SHUGHULI GANI?
ReplyDeleteCHAMA CHA MAPINDUZI HAKIHITAJI KUCHANGIWA, KINA VYANZO VYA MAPATO VINGI SANA, KWA MFANO WIWANJA VYOTE VYA MIKOA NI VYAKE, VIINGILIO VYA MECHI ZOTE TANGU MWAKA 2005-2010 VIMEENDA WAPI, hUO NI MFANO MMOJA TU IPO MINGI,
SINA HAKIKA KAMA WANA NIA YA DHATI YA KUKICHANGIA CHAMA ILA KUNA KITU MNAKITAFUTA HAPO BAADAYE, HASA UONGOZI.
HATA MSIPOCHANGA, CHAMA KIKO SAFI, MNAJIHANGAISHA BURE, KWANZA KINA WABUNGE WENGI, NA BAADA TU YA BUNGE HILI WATAVUNA MAFAO YAO, HAO TU WAKICHANGA NI PESA NYINGI.
KAMA MKO MASOMONI, SOMENI KWANZA ILI MPATE MAARIFA YA KUTOSHA, MJE MSIMAMIE SHUGHULI ZA UJENZI WA TAIFA NCHI IPATE KUINUKA, KUWAZA SIASA MKIWA MASOMONI MNATIA SHAKA, KAMA KWELI MNA DHAMIRA YA KWELI YA KUKOMBOA TAIFA LETU.
POLENI SANA, HAKUNA BIASHARA NGUMU KAMA YA SIASA, KUWENI WATAALAM, MTAVUNA.
Haya mambo yanawezekana UK.Hata mama Mwanaidi tumeshampelea ujumbe wetu kuwa karibu sana DC mama lakini matawi yako ya ccm yabaki huko huko London.Wabongo hapa US hatuna vyama vya siasa isipokuwa tuna vyama vya kusaidiana.Tukipata misiba tunasafirisha kwenda kuzika nyumbani kwa heshima zoote.
ReplyDeleteOyaaa, mnapigwa changa la macho. Dakika hii hii zinachotwa kutoka sehemu halafu mtadhania ni michango, this is just a silent magic once again, msidanganyike! TAKUKURU, tuna nyinyi!
ReplyDeleteVYAMA UPEWA RUZUKU KWA AJILI YA UCHAGUZI NA SERIKALI AMBAZO NI TAYARI PESA ZILIZOCHANGWA NA WANANCHI KUPITIA KODI, HIZO ZINATOSHA SANA, SI SAHIHI KAMA CHAMA KUOMBA MICHANGO, KINACHOFANYIKA WATU WENYEWE WENYE MAPENZI NA CHAMA WATACHANGIA BILA YA KUOMBWA. KWANI KIKWETE NI TAYARI MGOMBEA WA CHAMA KWA HIYO NI JUKUMU LA CHAMA KUTUMIA PESA YA RUZUKU ITOLEWAYO NA SERIKALI KUMNADI MGOMBEA WAO. WATU WANA HALI MBAYA KI-UCHUMI KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU CHA RECESSION, JUZI TU ULISEMA HUTATUONGEZA MSHARA KWA VILE SERIKALI HAINA PESA. SASA SISITUTAZIPATA WAPI KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU?
ReplyDeleteAnony wa 08:13:00 PM umeniacha hoi kwa kauli yako kuwa "safari hii uchawi umevuka bahari".Kaazi kwelikweli.
ReplyDeletemimi mtanzania lakini sio ccm.na ninaishi reading.kimoja HAMNA MCHANGO.
ReplyDeleteNdugu wenzangu, jamani walioombwa kuchangia ni wanachama wa CCM, WAPENZI WA CHAMA, MASHABIKI,MARAFIKI NA WOTE WANAOTAMBUA umuhimu wa CCM kuendelea kuongoza Taifa. Sasa kama wewe si mmoja wao, lisikukere hilo, kwani, tangazo hili halikuhusu my friend!
ReplyDeletewanaosema kutukuwe za EPA mmesahau, Serikali ya CCM ndiyo imewapeleka mahakamani?
Nawaliosema tuwaombe Matajiri wachache, CCM Imeshaliona hilo sio sahihi ndo maana wanachama wanaombwa kuchangangia chama chao!
Hii inahitaji tu watu wenye uelevu!uelewa mdogo ndo maana mnaandika hayo. POLENI SANA.
CCM JUU! KAMA KUWAOMBA WANACHAMA WETU KUCHANGIA CHAMA CHAO IMEKUWA NOMA, BASI NAIWE NOMA!
Wewe anonSat Jun 12, 03:06:00 PM, nini maana ya "ndugu wenzangu"??? Pia kwa nini msianzishe mtandao maalumu wa wakereketwa wa chama chenu badala ya kumwaga mchele kwa bata, njiwa na ng'ombe wakati mnawalenga bata peke yao. Hayo mambo yenu ya kutojipanga ndio yanaakisi hata utendaji wenu mbovu wa miaa yote. Nchi haikupata uhuru, bali ukoloni ulahamishiwa kwenu (warithi).
ReplyDeleteVitu vingine ninavyosoma huku sound like jokes. At the same time inaonyesha ni jinsi gani wabongo tulivyo na akili fupi hata kama tumeenda shule. Yaani mtu kaweka kabisa jina lake na personal contacts just kutoonyesha how foolish they are. Michuzi najua utanibania hii lakini honestly hili tangazo linatuabisha sisi Watanzania tulio UK.
ReplyDeleteHell to the NO
ReplyDelete