Habari Ankal,
Ebwana nilikuwa mada moja muhimu kuhusu Universities za Tanzania. Wanafunzi wengi wamekuwa wakicopy ( plagiarism) kutoka kwenye vitabu au article mbalimbali wakati wanapokuwa wakiandaa homework zao, final projects na kadhalika.
Ili kuepukana na tatizo hili vyuo vingi vya ulaya, asia vimekuwa vikitumia software inayoitwa plagiarism detector ili kuwanasa wanao copy katika vitabu au internet source yeyote. Kama bado system hii haijaanza kutumika Tanzania nilikuwa nashauri wangeianzisha ilikupungua au kuondoka kabisa ma graduate fake.
Gharama ya hii software sio kubwa na vyuo vyote vinaweza kuafford. Kwa wale wanafunzi wenzangu mnao andaa final report zenu mnaweza kucheki report zenu kupitia hii webpage
http://www.dustball.com/cs/plagiarism.checker

NB: Hii site inacheck internet sources tu
kama umecopy kwenye vitabu haiwezi kuona .

Mdau : Othman (Birmingham)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 09, 2010

    Halafu watu wanathubutu kusema eti elimu ya majuu raisi! Thubutu! Labda majuu nyingine, lakini sehemu kama UK, aisee ni akili mukichwa, watu wana-disco kwa ajili ya plagiarism, hiyo software iki-detect tu plagiarism, yaani ume-copy from somewhere bila ku-acknowledge source, ujue kuwa unarudishiwa paper lako UNMARKED!

    No kudesa here, that is why we miss home sweet home so much.

    Mazoea yana tabu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 09, 2010

    hiyo imeanza mda mrefu sana kaka, kwa hapa chuo kwangu wana software yao ambayo inaonesha %ge ya uliyo hamisha hlf wanakupa unachostahili

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 10, 2010

    Hey sidhani kama kuna mtu wa sasa hivi aliyekuwa na materials yake binafsi ndo maana watu tunaenda shule unafundishwa kutoka sources mbalimbali kama text books na materials mengine toka kwenye internet. Inategemea unasoma nini kama ni business na information technology sources nyingi zinatoka kwenye mtandao na vitabu. Cha msingi ndugu ni unapo-copy kazi ya mtu unatakiwa kueleza kwamba source ni wapi kama ni kwenye kitabu lazima uonyeshe ukurasa na mwandishi ni nani. Hiki sio kitu kigeni na kilikuwapo miaka mingi iliyopita na ukizingatia sasa hivi information zote zipo kwenye mtandao hauhitaji hata kutumia hiyo plagiarism checker google a line na you will get the entire story don't be to excited with this issue na kulipuka ovyo ndo upo mwaka wa kwanza chuoni nini? Inaelekea mdau yamekukuta wewe wamekukurupua wewe umehamisha ideas za watu na kuweka kwenye paper yako ya final. Next time take the idea and write on your own english.
    MDAU WA DAMU USA

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 10, 2010

    mdau wa Thu Jun 10, 07:39:00 AM mbona unaruka tu kuleta comments bila ya kusoma kwa umakini kilichozungumzwa awali?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 10, 2010

    Sawa plagiarism sio nzuri kweli ila sisi wanfunzi tutunge vitu vyetu akilini,ndio maana tunasoma vitabu na sources zingine,ila katika uandishi wa kitaaluma lazima wewe mwanafunzi uweke marejeo(references).hapo sidhani kama utakuwa umefanya plagiarism,elimu ya huku majuu sio ngumu kama TZ jamani.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 10, 2010

    Labda niweke sawa kidg, ktk elimu zote suala la plagiarism ni tatizo ambalo walimu wote huwa wanakemea sikuzote, bt the issue is how strict are they??nimebahatika kusoma undergraduate Tz na ss nipo UK, tofauti niionayo ni kwamba wenzetu huku wako makini sana na wanafanya vitu kwa vitendo tofauti na elimu yetu ya bongo ambapo mtu suala la kudesser inaonekena ni kawaida kbsa,
    kiukweli ili tuweze kuenda sawa na ulimwengu wa leo ni lazima suala hili lichukuliwe umakini wa hali ya juu
    Mdau-Birmingham

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 10, 2010

    Anon wa kwanza badilika!! Unataka kutumia mbinu zilezile hata kwenye mazingira tofauti? Upo katika 'better teaching and learning environment! Unlimited access to the latest books, papers and technology, highly experienced and motivated lecturers at your disposal, unlimited access to modern laboratories and most resourceful personnel, Absence of Tanesco and Hall 3, bado unamiss mazingira ya shule ya Mlimani kwa sababu ya Madessa? Where is Kamau when I need him?!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 10, 2010

    Nimechecki plagiarism kenye Post yako na nikaambiwa Plagiarism suspected umecopy one-to-one kutoka

    http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-elimu-education-forum/64070-plagiarism-detector.html

    Hatari kwelikweli, wala usijitetee kuwa wewe ndiye OGM, maana huja acknowledge source ya habari yako!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 10, 2010

    Tatizo lako mdau inaonekana kana kwa ulikuwa ni mmoja wa wale waliokuwa wananunua mitihani, mpaka kufika level ya undergraduate ulikuwa unapata mitihani ya final mtaani, na hasa hiyo ndo tabia ya wabongo wengi. Ona sasa hivi serikali imejitahidi kuziba loopholes za uvujishaji wa mitihani na wanafunzi wengi wana fail sana kwenye level za secondary hii inaonyesha wazi kwamba wanafunzi wengi walikuwa wanafaulu pasipokutumia akili zao. Sasa unapofanikiwa kupata nafasi ya kusoma nje ya nchi ndo maana unashangaa kama wewe. Plagiarism ni kosa kubwa sana tena mwenye material yake akiona umeiba pasipo idhini yake anachofanya ni ana sue the college na imeshatokea mara nyingi sana kwenye nchi zilizoendelea. Vyuo vingi vimekuwa sued na kulipa mamilioni ya dolars kwa wanafunzi kutumia sources za watu bila kuwa na copy rights. Hivyo ninachokushauri uwe makini katika paper zako soma materials na use your own english usiwe mvivu kutaka ku-copy and paste kazi za wengine.

    MDAU WA DAMU USA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...