Mama na watoto wake wanaoishi ufukweni
karibu na hospitali ya Ocean Road jijini Dar
Mdau Gladys Kasesela akipozi na mama na watoto
wake baada ya kuwapa zawadi ya miamvuli na nguo leo

Kwa wadau wa watoto wote
Kwa wale wanaopita barabara ya Ocean Rd karibu na Hospitali ya
Aghakhan utaomuona mama mmoja amekalia gogo akiwa na watoto wanne
wamemzunguka, mama huyu amekuwa anaishi eneo hili kwa muda mrefu.
Nasikitika kuwaeleza wapenzi wa watoto kuwa mama huyu amejifungua
mtoto wa 5, ukiangalia picha utaona kama amebeba katoto. Mama huyu na
watoto hawa wamekuwa wanaishi maisha ya hatari sana.

Mama huyu baada ya kuongea naye aliomba wasamaria wema wajitokeze kwa
ajili ya kulea watoto, wasi wasi wangu je sheria inasemaje, maana
sheria mpya watoto naamini ilipitishwa hivi karibuni, na pia juzi tu
tumetoka kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika.
Kuna uwezekano kabisa mama huyu ana matatizo ya kiakili (mimi si mtaalamu kwa hiyo sina uhakika) lakini ana kumbukumbu kwamba baba ya watoto hawa, baba wa kwanza ni mchaga (mtoto anaitwa Haika), mtoto wa pili baba yake
Mkikuyu, mtoto wa tatu wa mgiriki , mtoto wa nne kazaa na Mkongo wa
nne anasema ni Mfaransa.

Leo hii nilipita ikabidi nimpe miamvuli na baadhi ya nguo, utaratibu
ambao nimekuwa nafanya mara kwa mara, pia ameniambia Mh Batilda Burian
amekuwa anamsaidia sana.

Nawaomba wadau mjitokeze kumsaidia mama huyu,
hasa watoto ambao wana kosa elimu na malezi bora.

Ahsante
Mdau Gladys Kasesela

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 37 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 30, 2010

    ankal michuzi kuna siku ukinibania meseji zangu huwa nakutumia meseji za kukutukana naomba nisamehe na pole kwa kukukwaza, hasira nyingine ni za kishetani tuu sitarudia tena huo upuuzi nisamehe,
    nakutakia kazi njema ,
    ni mie mwana mkaidi niliyetambua kuwa
    Mungu anatisha na ni wa baraka tele
    thanks

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 30, 2010

    hii ni huzuni sana dada kasesela na ni vyema umemsaidia na bila shaka wadau wengine watamsaidia sana.Ila mimi nimecheka sana baada ya kusoma maelezo ya mbele ya habari hii. Huyo mtoto mgiriki na mfaransa mbona mweusi.au kafuata damu ya mama?hahaha.
    Good day

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 30, 2010

    HUYU MAMA ANATAKIWA SUSTAINABLE AID/HELP/ASSISTANCE. KUMSAIDIA NGUO NA MWAVULI NA KUMUACHA HAPO HAPO NINA-WASIWASI KUWA HAVITAMSAIDIA KITU. WALE WENYE UWEZO WA KUMSAIDIA KWA NAMNA INGINE WAJARIBU KUFANYA HIVYO. KITU KAMA MAKAZI NA UCHUNGUZI WA AFYA YA MWILI NA AKILI MLA SAMAKI MSAIDIA WAVU AKAVUE, USIMPE SAMAKI, NA MWENYE NJAA MPATIE JEMBE AKILME SI UNGA, THOSE ARE NOT SUSTAINABLE. MASIKINI MPATIE MAARAIFA AJIKOMBOWE, THE SAME NOTION WHY WE WERE GIVEN FREE EDUCATION SOON AFTER UHURU, THE GOVERNMENT EXPECTED THAT AFTERWARDS WE WOULD HAVE DEVELOPED AND BUILT SUSTAINABLE DEVELOPMENT AND THEN WE COULD START PAYING FOR THOSE THINGS SUCH AS EDUCATION AND HEALTH SERVICES. SO WAKUBWA TUNAOPITA HAPO DAY IN DAY OUT TUMUONE HUYU MAMA YETU

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 30, 2010

    HB unaona chukuwa wanao bwana. Mungu atamsaidia atapata msaada.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 01, 2010

    Hivyo inakuwaje anazaa watoto wengi namna hii wakati hana uwezo wa kulea? Solution hapo ni kumchukua huyo mama na kumpeleka hospital akatolewe kizazi ili asizae tena. Akiendelea kuzaa huyu ni kuwabebesha watu mizigo isiyokuwa na maana, maisha magumu jamani kila mtu anaangalia familia yake sasa. Wewe Glady fanya juu chini ukamtoe kizazi huyu mama ili asizae tena.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 01, 2010

    Nyie kwani Hakuna Mgiriki Mweusi au Mfaransa Mweusi? kama walichukuwa Uraia wakamwambia Ni Mie Mgiriki Mie Mfaransa sindio Nyie mtarudi Mie mtu wa USA bwana sindio mnavyojifagilia mie Muengereza. Serikali na wananchi wanaoishi karibu wanasaidia pesa nyingi ni muda wa kumsaidia huyu Mama. watoto wake hawana kosa.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 01, 2010

    Hapo ndio wanaume wanaponitibuaga mpaka basi, kweli kabisa mama wa watu hana akili bado mnajichukulia fursa halafu Mkuu wa nchi anasema mabinti wanaopata mimba wasirudi shule hiyo idadi ya machangudoa huko mjini sijui nani ataipunguza? na wanaowapa mimba kwanini hawachukuliwi hatua imeniudhi sana!!!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 01, 2010

    ninavyoelewa mimi ni kuwa huyu mama amesaidiwa mara kadhaa na wizara ya maendeleo ya wanawake na watoto na pia idara ya ustawi wa jamii. lakini kila akipata misaada ataipokea na baadaye kurudi hapo. pengine wizara au ustawi wa jamii wanaweza kuthibitisha hayo

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 01, 2010

    Nashukuru mdau kwa kumsaidia hili lakni mimi nilikua nataka kusema kama huyo mtu hap juu. Tunajua serikali yetu haina social welfare lakini ni heri wamtoe kizazi tu. Hao watoto wanateseka sana na hawakuomba hii kabisa katika maisha yao...Wamezaliwa kwa kutokupenda. Mimi na believe on cycle of life hapo amewazaa hao watoto na kuwachukulia nafasi ya hao watoto kuzaliwa mahali pengine. Mnakujua jinsi ilivyokua shida sasa hivi watu kupata watoto. The reason behind the baby factory is overworking, Hao watoto wangezaliwa kwenye mahali pengine lakini kwa ajili ya watu wasio na huruma wakaenda kutembea na huyu mama bila kujali akipata mimba itakuaje ndio hivo...

    Serikali iingilie hili kama haiwezi kutunza hao watoto let us all collect our DNA ukikutwa unatembeza spam zako kama mchanga wa pwani basi uchukuliwe sheria..Utazalishaje mtu asiye na akili?

    I feel for those kids masikini

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 01, 2010

    Watu wanachangia CCM wakati kuna sehemu za kutoa misahada na hata Mungu atabariki.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 01, 2010

    Michuzi..naomba usiniweke kapuni
    Nilipata kukaa kijiwe kimoja karibu na Hotel ya Southern Sun zamani Holiday inn, kuna shoe shine mmoja alinipa mkanda mzima wa Mama huyo. Inasemekana mchaga mwenye mtoto wa kwanza ni mfanyabiashara mashuhuri sana K'koo na huwa anamuhudumia mtoto wake. Imani chafu waliokuwa nayo wadau wajinga ni kwamba ukitembea na Mama huyo mambo yanakwenda mswano kwenye kila unachofanya. Kongo pia analea mwanae na huyo Giriki inasemekana ni muarabu wa K'koo. Tatizo la Mama huyo ni kwamba hata akitolewa hapo baada ya muda wadau wanamtafuta kuja kumrekebisha na kuingia mitini

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 01, 2010

    Mimi kinachonishangaza ni hao wanaume wanaompa mimba mama kama huyo,mbona wamekosa huruma,mimi huwa najiuliza hao wanaume wanaowachukua wanawake kama hawa huwa wanakuwa na akili nzuri kweli ama na wao huwa ndiyo walewale?Anyway watanzania tujitokeze kumsaidia huyu mama.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 01, 2010

    Tusijiulize maswali mengi na kumlaumu uyu mama,kwanza anaonekana ana matatizo ya akili na pia uenda anabakwa na wahuni ndio maana anakuwa anapata mimba ovyo,au hamjui kuwa kuna baadhi ya mwanaume wanatabia ya kubaka vichaa,
    mimi Naona tumsaidie,
    na mimi niko tayari kumsaidia,

    Michuzi mimi naomba wewe uwe mweka hazina,
    Toa maelezo tukupate wapi ili tuweze kumchangia uyu mama at least aweze kupata chumba kimoja cha kupanga na tumuwekee housegirl wakuwalea hao watoto,
    Na kupita blog yako utakuwa unatupa update ya uyu mama anaendeleaje wasamaria wema tutazidi kujitokeza kuchangia hali kadhalika kusomesha hawa watoto shule ya bweni .
    Maana kama hako katoto ka kike ka kwanza sasa hivi atakua na yeye kuanza kuingiliwa na wanaume kama sisi wadau hapa hatutashiriki kwa namna moja ama nyingine,na sisi ndio Tutajihukumu bila kutarajia,
    Dada Kasesela ni kama Malaika wao,kupitia yeye katuunganisha nao ili tuweze kuwa wakombozi wao Kupitia kupitia baba yetu aliye mbinguni MUNGU,
    God is watching us wadau LETS DO SOMETHING
    Na turudishe fadhila kwa njia hii,
    MUNGU AKUKUGUSE ANKAL Michuzi na wewe uguswe ulivalie njuga ili jambo hata kulirusha kila Mwenzi kutukumbusha kutoa kwa njia ya kubadilisha maisha ya mwenzio asiye jiweza,
    Na Mwenyezi Mungu atuguse Wadau wa ndani na nje ya Nchi kubadilisha maisha ya hawa watoto wa taifa la kesho.
    Mimi niko Tayari ninahitaji support kwenu

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 01, 2010

    Napenda Kumshukuru Glady kwa kutoa msaada alioweza kuutoa kwa huyo mama na watoto wake,
    Nyie mlaomkebehi Glady kwa msaada alioutoa kumbukeni "kutoa ni moyo usambe si utajiri", kwanini na nyie msiuige mfano wa huyo dada kwa kutoa misaada mingine mbalimbali?

    Kuna mdau anamlaumu huyo mama kwa kuzaa watoto wengi wakati hana cha kuwapa, Kumbuka huyo mama anaweza kuwa alirubuniwa na hayo wanaume wenye roho mbaya kama ya mbwa mwitu kwa pesa kidogo na kwasababu anadhiki na shida akashawishika.

    Maoni yangu ni kwasababu kuna NGO nyingi zinazopata misaada kwa ajili ya kuwasaidia wasiojiweza, ninaziomba zijitokeze hata kama kila moja ikamchukua mtoto mmoja sio mbaya.
    Hayo ndio maoni yangu kwa leo.
    Nawatakia siku njema na kazi njema. MUNGU AWABARIKI.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 01, 2010

    SIJAELEWA IMEKAAJE!! MAANA ALITOKEA WAPI MPK AKAWA HAPO? TUNAWAHAMISHA OMBAOMBA NA WAZURURAJI NA WAMACHINGA, HIVI USTAWI WA JAMII NCHI HII IMEKUFA? NA KAMA IPO KAZI ZAO NI NINI?VIPI WIZARA YA WATOTO AU WAMA WAKO WAPI AU BAJETI ZAO KAZI ZAKE NI KUTOA MATANGAZO KTK TV NA REDIONI KAMA WAFANYAVYO HAKI ELIMU? MAANA HAKI ELIMU HELA YA MATANGAZO INGEWEZA KUJENGA NYUMBA HATA 5 MPAKA SASA!!WANAOHUSIKA WALIFANYIE KAZI HILI AMETOKEA WAPI AMEFIKAJE PALE HANA NDUGU WALA JAMAA?KUTOKANA NA MAELEZO INAONYESHA HAYO NI MATUNDA YA UCD KILA MTOTO NA BB YK MAANA NI HATARI KWELI!!

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 01, 2010

    mhhhh! Kweli wanaume ni viumbe wa ajabu, sidhani kama wanaume waliubwa na roho ya imani, watoto wote hao bado wanaume wanaendelea kumzalisha? hata siamini. Hao wanaume si wachukue watoto wao mbona hawana huruma na watoto wao?
    Hawaoni ni dhambi kubwa kwanza ya uzinzi/uasherati pili ya kutesa watoto?
    Halafu anaomba msaada kwa watoto, jamani mbona madaktari hawamfungi kizazi, hao watoto ni wengi hata kwa mtu mzima mwenye hela?
    Wewe dada unayewasaidi kwanza hongera kwa moyo wako wa imani, hivyo ndivyo wanawake tunatakiwa tuwe na ndivyo tulivyoumbwa lakini tafuta njia nyingine ya kumsaidia ili ainuke kiuchumi ajitegemee au msaidie apelekwe hospitali

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 01, 2010

    Misupu usiweke kapuni, mi nadhani ntaonekana nna roho mbaya,huyu mama watu wamekwisha mpa misaada sana nakumbuka hata Clouds wamewahi kumuhoji na mpaka kuchangiwa nauli ya kurudi kwao na pesa za kujikimu kama kufungua mradi wake ili aweze kujikimu.
    Mimi naona kumchangia kila siku ni kumuendekeza kinachotakiwa arudishwe kwao na baba wa watoo watafutwe hayo mabo ya kusema hana akili ni mabo ya kusadikika na sidhani kama huwa anabakwa yeye kajigundulia sehemu ya kutega pesa basi.
    Watu imefika wakati wadeal na familia zao DSM watu wanasaidia ombaomba lakini nenda vijijini kwao wana ndugu wengi wenye hali za ombaomba wa dar na hawajawasaidia.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 01, 2010

    Ukimwangalia huyu mama kama vile hana ziki yoyote,mimi tatizo linalonikwaza bongo sana ni kuwa watu wamezidi usanii sana na kila mtu anabuni mtindo wake wa kujitafutia kipato kwa hiyo wadau msiwe mnaelezwa kila kitu mkatengeneza huruma tuu lazima muangalie vitu vingi najua michuzi hii comment yangu utaibania manake imekaa mrengo wa kushoto.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 01, 2010

    Ivi wewe Gladys una akili timamu kweli? sasa mwamvuli na nguo ndio umemsaidia nini? huyo mama na watoto wake wanatakiwa watolewe hapo wapate hifadhi ya kuishi; pia Mungu anisamehe ningependa huyu mama achunguzwe vizuri huyu ni msanii, halafu shida zote hizo bado tu anaendekeza libeneke kweli!!!

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 01, 2010

    Mambo Michuzi

    Thanks for this post. Kusema ukweli mama huyo sina uhakika kama ni mgonjwa au msanii, kwani jitihada za kumsaidia hazijaanza leo, Mama huyu alikuwa mwalimu Kigoma, chama cha walimu kilimpa makazi ukonga wakati akiwa na mtoto mmoja alirudi hapo. Isitoshe Clouds walishafanya mahojiano kuhusiana na mama huyu wakati wa kina Fina Mango na Masoud na watu wengine waliieza ni jinsi gani wamejaribu kumsaidia lakini wapi. Ninachoweza kusema mama huyo matunzo anapata watoto wake wanavaa vizuri, muda wote huwa yuko na prepared lunch kila siku kwa ajili ya watoto wake, vichanga anawavalisha pampers, maziwa ya kopo, yuko juu kwa kweli. Mpangilio wake wa maisha uko hivi mchana kutwa anashinda baharini, jioni muda mwingi anakuwa geti la aghakan la kutokea upande wa jolly, usiku analala BP karibu na Move n Peak Hotel. Yuko fit kuna siku nilikuwa napita na rafiki yangu nikamkuta anamuweka binti yake mkubwa relaxer, nadhani there are is a big hidden agenda behind this mama, na ukitizama kwa jicho la tatu utawaza mengi.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 01, 2010

    Nami napendekeza afungwe kizazi, ila pia mjue mama huyo anapiga fegi ile mbaya.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 01, 2010

    This lady will survive with or without the assistance from this forum.

    What is important is sister Gladys has a clear objective of what she wants to do. If the goal of this post just to help her to buy food for the newborn for two months or to raise attention to her needs, then perhaps this forum can help.

    But this situation is much more serious and requires a long-term solution than this forum cannot possibly provide: will these children grow up on the streets, are they being properly cared for, is the lady able to care for her children or herself?

    Perhaps educating all of us on the plight of the homeless and what we can do about it in Tanzania is a more helpful way to help this lady, her kids, and all in similar situation than giving her a few cents here and there and then we all move on...

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 01, 2010

    gladys hongera kwa kutoa msaada achana na walitoa maneno ya kashfa juu yako, sisi, na hasa hao walitoa kashfa uwezo wetu ni comment tu. lakini wewe uwezo wako ni comment na msaada kidogo, kwa hiyo upo juu!!!! kuliko sisi.

    Brain.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 01, 2010

    Huyu mama pia anasaidiwa na Agha Khan Hospital, nadhani hata hicho kichanga amekizalia Agha Khan, kwa ushauri tu ni kuwa ni vema Agha Khan wamfunge kizazi au wamuwekee vipandikizi vya miaka 10 ili kumnusuru, kwa hali ya maisha yuko juu anatuzidi hata sisi waosha vinywa hapa kwenye blog yako! Nadhani cha muhimu ni kuchukua hao watoto na kuwapeleka shule ya msingi Bunge,angalau iko karibu na beach, huyo binti mkubwa ndo anakua hivyo sasa fisi maji wasije anza kumvamia kama walivyomvamia mama yake. Hongera Glady, Something is Better than Nothing

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 01, 2010

    Akikaa hapo ndiyo anapata misaada kama hii ya kina Kasesela. Akiondoka hapo ataishije? Na kwa experience yake, akiwa na mtoto mchnga, misaada ndiyo inaongezeka!

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 01, 2010

    Kwa Comment za humu ndani inadhihirisha kabisa Watanzania hatuna roho ya kusaidiana,ndio maana hii nchi ni maskini sana,
    ingekuwa nchi nyingine za wazungu uyu angesaidiwa zamani,
    ndio maana unakuta Mtanzania mmoja kafanikiwa kusoma mwenyewe kwenye familia kati ya ndugu zake 6 au 10 then yeye hasaidii kusomesha hata mmoja,ili akirudi home azidi kupata sifa,lakini hajui kwamba anazidisha umaskini kwake kwa kuwalisha ndugu ambao hawana kazi katika maisha yake yote,
    kama unasaidia ndugu au mtu mapema kwa kumsomesha au kumpatia kamtaji basi hakika hata kaa kukusumbua maisha maana atakuwa na maisha yake.
    Wabongo tubadilike JAMANI
    Kumbukeni uyo mama kabeba malaika watano hapo,kesho wasiposaidiwa ndio watakuwa vibaka watakao waibia ninyi wenyewe na ninyi mtawachoma moto au changudoa,
    wacha kumlaumu uyo mama,ndio anaweza akawa ana makosa au amechanganyikiwa Je hao watoto Je???
    AMKENI TANZANIA,
    LINI TUTAACHA KUSAIDIWA NA WAZUNGU WANAKUJA KU-ADDOPT WATOTO WETU,KWANI SISI TUNASHINDWA NINI
    HATA KAMA MKITAKA KUNIPONDA UJUMBE UMEWAFIKIA

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 01, 2010

    Huyu mama ni msanii. Hataki kuondoka hapo.Wewe sio mtu wa kwanza kutaka kumsaidia.Waulize madereva wa taksi hapo Aga Khan Hospitali na wadau wengine waliokwisha msaidia au kutaka kumsaidia wakupe kinaga ubaga chake.
    Anawatesa hawa watoto kwa manufaa yake.
    Mimi nilisha saidia, lakini kila mwaka nikija nyumbani namkuta hapo hapo.
    Usiombe kumuuliza kuhusu msaada uliompa, utapata matusi makubwa.

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 01, 2010

    Wandugu,
    Baada ya kusoma comment za wanaomfahamu na wasiomfahamu limenjia wazo zuri la kudumu!
    Huyu mama asaidiwe kwa kutiwa jela huko ukonga. Kisha misaada yote ipelekwe huko. Tabia yake ya kutangatanga na kulala hovyo mitaani iyakoma. Pia hao wanaomgaia mimba watakoma kufanza matendo hayo. Watoto watasoma shule maeneo ya ukonga. Labda wasiwasi wangu ni makamanda wa gereza nao wasije ingia mkondo wa wenzao wa kutafuta utajiri au vyeo kupitia mama huyo( kama alivyosema mdau hapo juu ).
    Haya ni mwazo mazuri kabisa na mafanikio yake (probability) ni zaidi ya asilimia 80.
    Msukule

    ReplyDelete
  29. AnonymousJuly 01, 2010

    HOLD ON WABONGO!!! HATA HUKO UGHAIBUNI AMBAPO KUNA MISAADA KILA KONA, UTAKUTA HOMELESS, DRUGIES, NA WALE WALIODATA NA STREET LIFE, UNAMSAIDIA ANARUDI PALE PALE, MMESHAAMBIWA KASAIDIWA NA MHESHIMIWA NANI SIJUI, AGAKHAN, WATU BINAFSI.... SASA NINI TENA JAMANI? KUNA MDAU KASEMA YEYE ANANAFUU KULIKO SISI HAPA, ABANE MIGUU YAKE HUYO BIBI, MAANA HASHIKWI KWANGUVU WALA NINI. HIVI WAKATI AKIPEWA BOMBA TAMU, WANAWE WANAKUWA WAPI TOBA LAILAHI? HATARI HII JAMA!

    ReplyDelete
  30. AnonymousJuly 01, 2010

    Wifi yangu yangu na jirani yangu wa regent glady (mama monica)

    jamani huyu mama, hako ni katabia kake ameshapewa misaada mbalimbali lakini huwa hata kuondoka hapo.

    Ustawi wa jamii wameshajaribu kuwachukua watoto kwa ajili ya kuwapeleka katika vituo vya watoto lakini mama huyo huwa anagoma katu katu na kurudi katika eneo lake hilo.


    Analijua alifanyalo ndio mana pia kila wakati anayuko na new baby, na hao watoto ukiwaangalia wana hali ya kuridhisha kulinganisha na omba omba wengine.

    Kuna mambo ya kutafakari na kujiuliza kuhusu mwanamke mwenzetu huyu :

    a.kiwanini kila ustawi wa jami wanapojaribu kuwachukua watoto anagoma ?
    b.mi si mtaalamu wa biolojia , lakini hao watoto anaodai kazaa na wagiriki, congo, mfaransa. hawa wa kifaransa na kigiriki hata punje ya halfcast haipo. na mwenzet hawa wababa wa kigeni anaozaa nao huwa anawatoa wapi?pale kwenye gogo?

    kwa ufupi sina imani na ndugu huyu tabia yake haipendezi
    kwa u

    ReplyDelete
  31. AnonymousJuly 01, 2010

    Hutu mama alijifungua mwenyewe karibu na uwanja wa Old Guards hapo Ocean Road. Alipelekwa na msamaria mwema wa Taasisi ya Chakula na Lishe tanzania kwenye hospitali ya Ocean Road baada ya kujifungua, akaelekezwa aende Muhimbili. Alifikishwa Muhimbili na kuhudumiwa (hiyo ni saa nne asubuhi), lakini ilipofika saa nane mchana alirudi na kichanga chake na watoto wengine alionao kwenye maeneo ya karibu na Old Guards, akiendeleza libeneke la kuzurura kama kawa. Ndugu, kama unahitaji kumsaidia msaidie lakini watu wote wanamfahamu na kwamba amesaidiwa sana lakini hiyo ndiyo lifestyle yake. Hapo nguvu za serikali zinatakiwa lakini misaada haisaidii. Believe me or not.

    ReplyDelete
  32. AnonymousJuly 01, 2010

    PRESIDENT MTARAJIWA, JOHN MASHAKA UNASEMAJE KUHUSU HILI SWALA? AT THE MOMENT SERIKALI INABIDI IMSAIDIE

    ReplyDelete
  33. AnonymousJuly 01, 2010

    KILA MTU HAPA ZIRO WANAWAKE WANAWARUKIA WANAUME? INAONESHA POLISI HAWAFANYI KAZI ZAO. MIE KINACHOTAKIWA KUFANYA NI WATOTO WACHUKULIWE WASOMESHWE SHULE ZA WATOTO YATIMA WAEKWE SEHEMU NZURI YA KUKAA NA MAMA ATAFUTIWE SEHEMU AFUNDISHWE USUSI APATIWE KAZI ZITAZOWEZEKANA KILA KITU KINAWEZEKANA WAKIAMUWA WASAIDIZI.

    AU KAMA KUNA MTU HUMU ANATAKA KUSAIDIA MTOTO MMOJA NA MPAKA ANAKUWA MAWASILIANO NA WATU WAKE HAPOTEZI NI VIZURI. XYZ

    ReplyDelete
  34. AnonymousJuly 01, 2010

    Mimi nafikiri yeyote anayemiliki NGO ya watoto mayatima wangemchukuwa huyu mama na watoto wake, watoto wakaanzishwa shule na mama yao akapelekwa hospitali kutolewa kizazi. Baada ya hapo mama akawekewa ulinzi wa hali ya juu ili asitoke tena na huyo atakayekuwa naye afanye uchunguzi ni lazima tu hiyo midume itakwenda kumwangalia na hapo aongee na polisi na watege mtego na kuwakamata ili kuwawajibisha na waulizwe wamemjuaje mama huyo nasi tuko tayari kushirikiana na huyo atakayejitokeza kumchukuwa mama huyo. Tupate taarifa kupitia kwako Michuzi.

    ReplyDelete
  35. Huyu dada anaitwa Saada Kin'gombe mwenyeji wa Kigoma.Alikuwa akifundisha shule ya mzimuni primary kabla ya kuachishwa kazi.Alijaribyu nkufuatilia haki zaki in vain na na mlolongo wa makaratasi yanayoonyesha alivyojaribu kufuatilia issues zake.Anakaa zanzibar hotel apatapo fedha.Akikosa ndiyo analala BP pale karibu na former Red Cross na kushinda ufukweni.Ameishi Mombasa na husema ananyumba yake na vitu.Hufika kipindi akenda Kigoma akakaa na wakati ikifika hururdi tena Dar.Watoto wote inaelekea wa baba mmoja na Saada amesema kamwe hataaha kuzaa mpaka uzazi ukome.She is intelligent but something went wrong somewhwere.Kutokana na mazungumzi yake inaelekea ana ndugu Dar na Kigoma.Lakini kwa miaka kadha maisha yake yamekuwa ndiyo hayo.Jibu juu yake kwa kweli yupo mtu analo na pia mwenyezi mungu.Watoto hawaendi shule but they are bright and well mannered!sOMETHING WENT ASTRAY SOMEWHERE!

    ReplyDelete
  36. AnonymousJuly 02, 2010

    Jamani asanteni sana kwa comments zenu, muhimu tuwasaidie hawa watoto. Muhimu zaidi hapa ni sheria inasemaje unaweza chukua watoto baadae ukapata taabu. Kwa wale walio laumu ningeshauri wangesaidia kwanza kabla ya kutoa lawama. Pia kwa walio tayari kutoa msaada nadhani tuangalie wizara husika itatushauri vipi.

    Kwa kweli watoto watano wakiendelea kuishi maisha ya namna hii inahatarisha taifa.

    Nashukuru sana Kaka Michuzi kwa kulivalia kutoa post hii. Watanzania umefika wakati tuweke pembeni ubinafsi. Tusaidiane kwa mambo endelevu. Walio tayari kusaidia jitokezeni tuunde umoja ili tuone tutasaidiaje watoto hawa. Kumbuka tone moja hutengeneza bahari...
    asanteni

    Wenu
    Gladys Kasesela (Mrs)

    ReplyDelete
  37. AnonymousJuly 07, 2010

    kaka Michuzi naomba utuhabarishe kama kuna utaratibu wowote wa kutoa msaada, mimi siamini kama mtu mzima na akili timamu anaweza kukaa bure tu baharini na watoto watano...anapokuwa mjamzito au kipindi cha kujifungua watoto huwa wanakaa wapi? inawezekana kuna ndugu jamaa au marafiki wanaomfahamu, kama kuna hisia za matatizo ya akili bora apimwe apewe matibabu na sisi wana jamii tujikusanye tusaidie watoto inavyo wezekana,

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...