
Pole na majukumu ya kutuelimisha kupitia kwenye blog yetu.
Nilikuwa safarini mkoani Kilimanjaro nikaona sio mbaya nikawaletea taswira hii na kutaka kufahamu zaidi, Je? Tanroads wanasimamia ipasavyo sheria hii ili kulinda barabara zetu?
Kipande cha Barabara kati ya Korogwe na Mombo ni kibaya hakuna mfano lami yote imeng'oka na panaweza sababisha ajali katika kukwepa mashimo! Nikajiuliza je ni lami mbovu au magari makubwa ya mizigo yanayopita kila kukicha? Naomba kuwasilisha mada.
Mdau Mmbando
Mdau Mmbando
kwa nini faini ni kwa dola?
ReplyDeleteumesahau pia kujiuliza ni kwa nini adhabu ilipwe kwa dola na sio pesa zetu za madafu?
ReplyDeletehio hadhabu ya dollar kali mie naona hela yetu baada kuita shillingi tuite (tz dollar) manake watu wanavyoipenda dollar kiboko.
ReplyDeleteKwenye nchi za wenzetu huwezi kuona wakilipisha kwa pesa za kigeni...yaani hatuthamini kabisa vitu vyetu...huu ni ulimbukeni
ReplyDeleteThis is STUPID...Nani kaandika hapo TANROADS...C'amon...I say this is funny. Unaona kaka michuzi, Kweli sasa tunakuwa kama Somalia...a failed state. Hakuna serikali? Siamini kama hili ni tangazo la serikali..""DOLA"""wacheni masihara jamani
ReplyDeleteHalafu waziri wa fedha anasema tutumie shilingi wakati vyombo vya serikali vinadai adhabu kwa dola. Unafiki mtupu.
ReplyDeleteMi huwa nasikitika sana kuona mambo haya yanatokea. Miongo 2 ( au mi 3) iliyopita tulikuwa na treni za mizigo (hata abiria) zikitokea Dar kupitia tanga mpaka Arusha. Ni treni hizi zilizokuwa zikibeba mizigo mizito ambayo (ninavyodhani) ndio inaharibu Barabara zetu ambazo ujazo (gauge) yake nayo ni ya kusuasua.
ReplyDeleteKwa mtazamo wangu, treni hizi zingeendeelea kutumika kwa usafirishaji wa mizigo mizito kati ya Dar na sehemu kadhaa za nchi. Ila kwa "bahati mbaya", uongozi mbovu, rushwa, "kurogwa" ama sababu nyingine tujizijuazo na tusijozijua,nchi yetu inendeshwa kwa hisani ya "watu wa nje", watu ambao hawatakubali kuona mambo ya msingi na maendeleo kama haya yanatendeka.
Hivi kuna Mtanzania alishawahi jiuliza kwanini misaada yoooote ya miundombinu hijawahi kuelekezwa katika mfumo wetu wa Reli? Sisemi hivi kwa sababu naamini katika maendeleo yatayoletwa na misaada ila kwa kuhoji uhalisia wa hiyo misaada au "hisani" kama wana "Si hasa" wanavoiita.
Mimi huwa nina imani na Tanzaia mpya siku zote. Yote yanayotokea sasa ni chachu ya mabadiliko yajayo, ni sababu (waingereza wansema JUSTIFICATION) ya mapinduzi yajayo. Haya nimapinduzi yatayotokea pale kila Mtanzania atakapo dhihirisha hakuna cha kupigania zaidi ya maisha yake, wewe na mimi tunajua kuwa kiumbe chochote chenye pumzi (uhai) kitapigania pumzi (uhai)wake mpaka tone la mwisho.
Naelewa Watanzaia wengi kwa sasa wanajitahidi kuenzi sera ya "kisiwa cha amani na upendo" sera ambayo haina uhalisia kwa watanzania walio wengi kwa sasa.Kuna upendo gani baina yetu wakati kuna maelfu ya watanzania wanafariki kila kukicha kwasababu tu ya kukosa "vijisenti" kadhaa vya kugharimia "operation" upasuaji mdogo,wakati kuna watu kadhaa wana fedha nyingi mpaka hawana matumizi nazo, hawawezi kuziweka benki kwa sababu wanajua watanzania tutahoji uihalali wake hivyo wanaishia kuagiza fedha hizo katika biashara zisizo na kichwa wala miguu, ila hali tu zinawawezasha kuhifadhi fedha (utajiri) ambazo hawawezi kuthibitisha uhalali wake.
Ni suala la wakati tu. Siijui siku wala saa, ila kama utaratibu wa kuiendesha nchi uliopo sasa hautabadilishwa kwa manufaa ya wengi na nchi yetu kwa ujumla. "Kisiwa cha amani na upendo kitazama wakati wowote".