BWANA MICHUZI, HABARI ZA LEO KAKANGU? TAFADAHALI SANA NDUGU YANGU NAOMBA UNITUNDIKIE HILI SWALI KWA WADAU WA BLOG YETU YA JAMII WANISAIDIE. NATANGULIZA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWA WEMA NA UTUMISHHI WAKO ULIOTUKUKA KATIKA KUELIMISHA JAMII.

-----------------------------------------------------------------------

Wakuu heshima zenu,
Wandugu kuna rafiki yangu mmoja ameachishwa kazi kinyume cha sheria, naomba msaada wenu wa kisheria jinsi anavyoweza kupata haki zake.

Huyu bwana alikuwa akifanya kazi kwenye kiwanda kimoja cha kutengeneza nondo jijini Dar. Kwa bahati mbaya, akiwa kazini, alikatwa kiganja cha mkono wake wa kulia na mashine za kiwandani. Juhudi za madaktari kuurudishia mkono wake ziligonga ukuta. Alitibiwa jeraha la mkono uliopatwa na ajali na baada ya kupona alirejea kazini. Kwa kuwa hakuweza kufanya kazi zake kwa ufanisi kama ilivyokuwa mwanzo, mabosi wake walimhamishia kwenye kitengo kingine ndani ya kiwanda kwa muda. Lakini cha ajabu ni kwamba alipewa muda wa miezi mitatu kuomba kazi nyingine ndani ya kiwanda(endapo zitatangazwa) au nje ya kiwanda na endapo asingeweza kupata kazi yoyote basi angekuwa terminated from employment.

Baada ya kuisha miezi mitatu hakuna kazi yoyote aliyoipata ndani au nje ya kiwanda. Ikabidi atimuliwe bila huruma na bila kulipwa chochote zaidi ya kugharamiwa mkatibabu ya mkono wake.

Je, hii ni halali kisheria? Je, ni utaratibu gani wa kisheria ambao ulikiukwa hapa? Sheria za nchi zinasemaje kuhusu mtu aliyepata ulemavu kazini kama huyu ndugu yetu? Wadau naomba msaada wa kisheria katika hili na jinsi tunavyoweza kumsaidia huyu jamaa apate haki zake za kimsingi na kisheria.

Asante sana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 33 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 03, 2010

    Nampa pole sana ndugu yako. Jambo la kwanza je hapo kiwandani hakuwa mwanachama wa Chama cha Wafanyakazi? Ikiwa hakuwa mwanachama, nashauri aende Chuo Kikuu Kitivo cha sheria aonane na wanasheria wa kujitolea kwa suala kama hilo ili haki itendeke.

    ReplyDelete
  2. Awaone wanaohusika na haki za wafanyakazi katika ofisi za shirikisho la wafanyakazi tucta pale mnazi mmoja. Pia anaweza kuwaona wanasheria katika AZISE mbali mbali zinazoshoghulikia haki za binadamu.

    ReplyDelete
  3. Mume Wangu, safarini CanadaJune 03, 2010

    POLENI KWA MATATIZO YALIYOMPATA HUYO RAFIKI YETU.
    JE, HILO TATIZO LIMETOKEA NCHI GANI??
    kama ni kule marekani, anaweza kulipwa pesa nzuri za kuweza kununua meli mbili kama zile za Bakhressa na chenji itabaki.
    Kama ni huko nyumbani kwetu TZ, basi amshukuru Mola wetu Mtukufu kwani hatalipwa chochote kwa sababu hakuna sheria zinazofuatwa.
    Kuna baadhi ya mabosi wa hicho kiwanda watamdai RUSHWA ili wamsaidie kununua haki yake.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 03, 2010

    Pole sana. Ukweli ni kwamba sheria za kazi zinasema kwamba mwajiri ana haki ya kukufukuza kazi kama unashindwa kwa namna moja ama nyingine kutimiza kile ulicho ajiriwa kufanya. Ukizingatia kwamba alipewa matibabu pamoja na miezi mitatu ya kutafuta ajira ingine, mwajiri amefanya vyote kwenye uwezo wake, zaidi ya hapo kampuni itaingia hasara. Swala la kisheria ni: (1) Je mwajiri ana bima ya wafanyakazi wake kwa ajali kama hizi? Usije kuta yeye mwajiri kesha lipwa zaidi hata ya gharama aliyo tumia kumtibu mfanyakazi wake.(2) Kampuni ni ya kigeni au ya wazawa? Sheria za kazi zinaweza pishana kidogo. Kama ni ya kigeni itafaa kuangalia sheria za nchi husika zinasemaje.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 03, 2010

    Pole sana muhusika wa tukio hili,lakini kimsingi nawaachia majabali wa kisheria kutoa ufafanuzi,kisheria!!!
    La msingi hapa sheria ya usalama kazini na viwandani itatumika,sasa ni jukumu la wanasheria kuangalia utekelezaji wa wajibu wa mwajiri na mwajiriwa katika sheria,inawezekana mwajiri alitimiza kila linalowezeka na kuhakikisha kaondoa hali hatarishi katika eneo la kazi,ikiwamo kuwapa wafanyakazi vifaa kinga vinavyo stahili,kwa sehemu husika ya kazi,na yawezekana aliwapa pia mafunzo ya usalama,hatujaelezwa hili kwenye lalamiko,ila kama mwajiri hakuyafanya hayo juu nloyataja,na ikathibitika hali hatarishi maeneo ya kiwanda ipo,na matukio yanatokea kwa uzembe wa mwajiri,namshauri muhusika atembelee ofisi za kazi,balaza la usurushishi wamusaidie wapi pa kuanzia kutafuta haki yake!!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 03, 2010

    mwambie aende kwa mwanasheria, hawa wahindi wamezidi kunyanyasa watu

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 03, 2010

    Machozi yamenitoka.....Silewi sheria za kazi Tanzania lakini kwa kukatika mkono hivyo ni lazima wangetakiwa wamsaidie sana tu. How much is degree of disability? Sheria ziko tofauti hata huku tuliko ni state by state...Na kama alishasign makaratasi ya kukubali kulipiwa tu hela za matibabu ndio imetoka hiyo..

    Angekua nchi hizi huyo angekua na ahueni... Kiwanda lazima kina workers comp insurance sasa ni za nini kama hazisaidii watu?

    Na kupata kazi ya mkono mmoja Tanzania ni wapi atapata?

    My poor lovely country.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 03, 2010

    Pole sana mdau lakini usikubali haki yako ipotee wasiliana na vituo vifuatavyo kwa ushauri na msaada wa kisheria:

    Legal Human Right Centre
    P.O.Box 75234, Dar es Salaam
    Telephone:+255 22 2113177
    Fax:+255 22 2118353
    Email: lhrctz@raha.com
    More Information

    Action for Relief and Development Assistance (AFREDA)
    P.O.Box 10014 , Dar es Salaam
    Telephone:+255 22 2863320
    Cell:255 744 342466
    Fax:+255 22 2112752
    Email: afreda@faru.or.tz / afreda@twiga.com
    More Information

    Triumph Handicapped and Needy Foundation (Tanzania)
    Telephone:+ 255-26-270-2109
    Fax:+ 255-26- 270-2486
    More Information

    WLAC - Womens Legal Aid Center (Tanzania)
    P.O Box 79122, Dar es Salaam
    Telephone:+ 255-22-218-3769 255-22- 218-0005
    Fax:+ 255-22- 218-3028
    Email: wlac@intafrica.com
    More Information

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 03, 2010

    huyu mdau ilituweze kumpa maoni yetu angetueleza huyo ndugu yake alifanya kazi kwa miaka mingapi katika hicho kiwanda na alikuwa na mkataba wa aina gani na kama kunachama cha wafanyakazi hapo kiwandani.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 03, 2010

    Nampa pole sana aliyefikwa na ulemavu huo. Ipo sheria ya ku compasate kwa mfanyakazi aliyeumia akiwa kazini na kupoteza kiungo.Kwa kuanzia nashauri aende kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi TUICO, kule ataelekezwa kila kitu. Vyama vya wafanyakazi kazi zake ni pamoja na hiyo. Pole sana asijali atafidiwa tu.
    Upendo

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 03, 2010

    Tatizo letu mtu unapoomba kazi huwa tunaangalia mshahara tu kwamba utalipwa ngapi. Makampuni mengi ya kigeni hata ya hapa nchini huwa ama wanakuajiri kwa mkataba wa maandishi (renewable)au kama kibarua usiyekuwa na mkataba unalipwa juu kwa juu. Sasa huyu jamaa aliyefukuzwa kazi inategemea yuko katika kategory ipi ya ajira kati ya hizo mbili hapo juu. Na kama una mkataba, huo mkataba ulishaisha muda wake ukau-renew? na unasema chochote juu ya hayo yaliyotokea? Kwa kifupi hapa mkataba wake ndio unaweza kujibu baadhi ya maswali yake kama ana haki gani. Kama haukuwa na mkataba kwaheri huna chochote utakachoambulia

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 03, 2010

    Hilo suala unatakiwa ukawaone wanasheria au nenda labour union (sheria za kazi) ndio utaapata jibu kamili, hapa sio mahala pake utapata majibu yasiyo na majibu

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 03, 2010

    nduguyetu huyo haki anazo tena sana wala asife moyo.
    kwani dunia nzima mfanyakazi akiumia katika kazi lazima hakizake alipwe.
    ameumia wakati akilihudumia hilo shirika nisawa nawanajeshi nae pia
    ni mwanajeshi katika hicho kiwanda.
    lazima ende vyombo nya sheria vipo na atasaidika tu tanzania ya leo sio ya jana kaka msimamie mwenzio mungu atawasaidia.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 03, 2010

    Pole sana mdau.Ninakushauri kama uta-post email address yako ama simu namba ili watu waweze kukusaidia vizuri zaidi, maana kuna vipengere vingi vinahitajika kabla ya kukupatia ushauri ulio na manufaa kwa kesi yako.

    Lakini kwa ufupi ni kuwa unaweza kwenda na rafiki yako huyo mpaka ofisi za CMA pale NPF Ofisi (siku hizi wanaita Mahakama ya Kazi na kuomba CMA Form 1 ili kuweza kuomba majadiliano ya kuachishwa kazi kiuonevu (Unfair terminaation ) kwa mujibu wa kifungu 37 (2) (c )na kifungu kidogo -subsection- (3) (ii) cha Employment and Labour Relations Act. No. 6 of 2004. na pia Employmentand Labour Relations (Code of Good Practice ) kupitia GN. No 42 ya mwaka 2007 Rule 19 INATOA MAELEKEZO YANAYOHUSIANA NA ILL-HEALTH OR INJURY.

    pole sana na jitahidi kutoa namba na email tuweze kukusaidia.

    Ghett B.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 03, 2010

    Kwanza wasiliana na kituo cha haki za binaadam - kijitonyama, wanatoa msaada wa kisheria katika hali hiyo. Pili cheki na OSHA - occupational Safety and Health Agency - wanapaswa kudili na swala lako maana wanahusika na usalama wa mfanyakazi, ikiwa ni pamoja na kuwaadhibu waajiri wanaotumikisha bila kuwa na vifaa vya usalama kazini. Tatu cheki na chama cha wafanyakazi wa viwanda (cheki na TUCTA watakupa jina lao au nenda ILO pale jamaa watakusaidia ushauri wa kupata msaada wa kisheria?. Tatu wewe mwenyewe tafuta na soma sheria mpya ya ajira ya mwaka 2004 (utaipata ATE -association of Tanzania Employers, TUCTA au ILO, itakupa mwanga wa msaada gani unataka. ZINGATIA KAMA ULIKUA NA MKATABA PIA, NA WA AINA GANI? KILA LA KHERI NDUGU!

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 03, 2010

    Ebwana kwanza pole kwa huyo jamaa kwa hayo yaliyomkuta. Nijuavyo mimi kisheria mtu hawezi kuachishwa kazi kwa sababu kapata ajali tena kazini. Hapa kuna namna mbili za kushughulikia swala lake. Kwanza anatakiwa akatoe taarifa katika Kamisheni ya Usuluhisho na Upatanishi ya Wilaya/ Mkoa. Kuna muda maalumu wa kufanya hivyo, nafikiri ni ndani ya siku 30 toka alipoachishwa kazi (hata hivyo anaweza kujaza fomu ya kuomba kupeleka malalamiko yake nje ya muda. Hapo watashughulikia swala lake na akishinda ataweza kupewa mishahara ya hadi miezi 12. Hata hivyo kwa kuwa wameumia kazini anaweza kulalamika kwenye baraza liloundwa na sheria ya mwaka 2007/08 lakini sina uhakika kama limeanza kazi.
    Ni hayo tu.
    Mwananchi kutoka Coventry-Ukerewe

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 03, 2010

    Kwanza pole sana kwa kupata ulemavu usiotegemea. Napenda kukushauri kwamba sheria ipo mradi uwe na documents zote za hospitali zinazoonyesha kweli ulipata ajali kazini na ukakatwa mkono. Nenda Wizara ya kazi utapata mwongozo wote.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 03, 2010

    huo ni unyama aliofanyiwa kwa kweli....apeleke hayo madai ktk vyombo vya sheria...Atalipwa

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 03, 2010

    Well, kwa kweli hiyo hali inasikitisha....
    1-Hakuwa mwanachama wa kikundi chochote cha wafanyakazi kama TUCTA??
    2-Kama ndio basi,aanze huko kupeleka malalamiko yake ili waeze kumsaidia kulipwa fidia
    3-Kama hapana then anaweza kwendaa ofisi za wanasheria wa serikali kuomba msaada kwa sababu hili suala lazima lishuhulikiwa na labour concilliation board kama kuna madai yake alipwe coz hiyo ajali imeokea kazini na lazima mwajiri atimize wajibu wake iwapo hakutoa vifaa vya usalama!

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 03, 2010

    Pole ndugu, kwa niaba ya mhanga.

    Kuna Mahakama ya Kazi, Nadhani ndiyo inahusika na ussues za uonevu kazini. Tafuta mwanasheria akusadie, hiyo itakuwa ni 'more practical' kwa sababu huyo ataongea na muhusika moja kwa noja na kuona barua na vyeti vya Daktari, hivyo kukushauri kitaalamu zaidi. Pale chuo kikuu DSM, idara/kitivi/College ya sheria, walikuwa na utaratibu wa kutoa msaada wa kisheria bure, sijui kama bado upo. Jaribu pale pia, ikiwa fedha za kumlipa wakili zitakuwa shida.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 03, 2010

    Ni kinyume cha sheria kumfukuza kazi mfanyakazi kutokana na disability. Mwajiri anatakiwa adhibitishe kuwa ni halali kumfukuza kazi huwa mfanyakazi.

    Kwa kifupi huyu mfanyakazi akafungue kesi haraka.

    Kwa maelezo zaidi some EMPLOYMENT AND LABOUR RELATIONS ACT, 2004- Kifungu 37.3.b

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 03, 2010

    poleni sana, kisheria anapaswa kulipwa kwa kuwa aliumia akiwa kazini ila inategemeana na kama aliumia kwa uzembe, bahati mbaya au makusudi. Kuna watu TAZARA workshop walikuwa wanakata vidole ili walipwe fidia, nendeni OSHA pale Mwananyamala mahakama ya Kinondoni utapata msaada wa kuhusu sheria za kazi na OSHA Act 2003

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 03, 2010

    Ndugu yangu kuna sheria za kazi,kama mtu akipata ugonjwa au ajali na ikadhibitishwa na madaktari kuwa hawezi tena kufanya kazi,basi mwajiri wake ana budi kumlipa mafao yake kama mkataba unavyoelekeza,kukuongezea kama huyo mtu anakuwa ni mwanachama wa moja ya hifadhi ya jamii atalipwa mafao yake pia,Mfano Mzuri kwa PPF Kama ameshachangia kwa miaka kumi basi mfuko wa ppf unafao la Ugonjwa,huyo mtu angelipwa mkupuo then mwezi ufuatao angeendelea kulipwa kila mwezi kwakutumia fomula mpaka mwisho wa maisha yake.
    NDO MAANA SERIKALI INASISITIZA KILA MFANYAKAZI KUJIUNGA NA MOJA YA MFUKO WA HIFADHI YA JAMII.
    KARIBUNI PPF KWA UHAKIKA WA MAISHA YA BAADAE.
    Tc.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 03, 2010

    pole sana mdau uliyepatwa na matatizo hayo,mimi sizijui sheria zinasemaje ilaninachoweza kukushauri nikwamba,mtafute mwanasheria mueleze matatizo yaliyokupata nanini uamuzi wako juu ya suala hili,kwakuwa yeye nimtaalam washeria atakusaidia tu,pia unawezakwenda kufungua kesi,kutokana nakwamba umeumia kazini basi unastaili malipo nakuendelea nakazi pia.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 03, 2010

    Kwa kweli si haki kabisa. kampuni inapashwa ipelekwe mahakamani. Huyo mfanyakazi anahitaji kupewa compensation amekuwa disabled while working at the company. First of all it is not humane kabisa. Yaani lazma wawe sued wampe haki yake au wampe kazi inayoendana na disability yake. Nampa pole sana kaka lakini hii issue siyo ya kulaza damu. Wakati umepita haki ya mtu lazima apewe. Kila la heri kaka.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 03, 2010

    Aende serikalini idara ya kazi watamsaidia kupatiwa haki yake kisheria na shirika la bima ili kiwanda kimplipe kupoteza kiongo cha mwili wake

    ReplyDelete
  27. Employers have a duty to make ‘reasonable adjustments’ to cater for any employee considered ‘disabled’ under the law. This is where a person has a physical or mental impairment which has a substantial and long-term (likely to be more than a year) impact on their ability to carry out normal day-to-day activities.

    The employer should have considerred alternative employment more suited to the employee’s health constraints. Dismissal should always be the very last resort.

    He need to seek legal advice on the available option. Most ground is likely to be discrimination due to his disability. He needs to act very quickly as there is a limitation of time to bring a case at an employement tribunal for compensation, etc.

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 03, 2010

    thats unfair dismissal mate,consult the legal advisers and i reckon you will be compansated untill you get new job.

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 03, 2010

    HIYO KESI NI RAHISI SANA NA ANAWEZA KUSHINDA KIRAHISI SANA; KWANZA SWALA LA USALAMA KAZINI, HATA KAMA KAMPUNI ILIWEKA VILINZI, I MEAN GUARD ZA KUZUWIA AJALI KAMA HIZO ZISITOKEE, BASI HIVYO VILINZI VYAO SI SAHIHI NA HAVIFANYI KAZI IPASAVYO NA KAMA VINGIKUWA VINAFANYA KAZI ASINGEPOTEZA MKONO WAKE; NA KAMA WANATOWA MAFUNZO PIA HAYATOSHELEZI NDIYO MAANA AKAPOTEZA MKONO WAPI; HUYO BWANA UNDER ANY SCENARIO ANAPASHWA KULIPWA FIDIA YA MKONO WAKE, NA WALA HAKUSTAHILI KUFUKUZWA KAZI, KAMA ATAPATA WATETEZI WAZURI ANATAKIWA KULIPWA MSHAHARA WA MUDA WOTE HADI SIKU ZILIZOBAKI YEYE KUSTAAFU KWA VILE AMEUMIZWA NA MASINE ZA KAZINI KWAKE NA SIYO NYUMBANI KWAKE NA HATA KAMA KAMPUNI HAINA BIMA ZA WAFANYAKAZI WAKE HILO PIA NI MAKOSA KATIKA KIWANDA CHENYE HALI KAMA HIYO KINAPASWA KIWE NA BIMA KWA AJILI YA AJALI ZA WAFANYAKAZI WAKE, PIA ANATAKIWA AREJEE KWENYE MKATABA WAKE WA KAZI KWANI UNASEMA UKIUMIA UTAACHISHWA KAZI? SI DHANI KAMA UNASEMA HIVYO! NA KAMA UNASEMA HIVYO NA WATU WANAOMBA KAZI HAPO NA KU-USAINI BASI HIYO NI CRAZY NA KWANZA UTAKUWA HAUSTAHILI KUPITISHWA NA WIZARA YA KAZI. MIMI NINGEELEWA KAMA HUYO JAMAA ALIUMIWA NJE YA KAZI NYUMBANI KWAKE NA AMERUDI KAZINI NA AMESHINDWA KUFANYA KAZI SAWA, LAKINI AMEUMIA NDANI YA UTEKELEZAJI WA KILE ALICHOAJILIWA KUKIFANYA, HUO NI UONEZI WA HALI YA JUU NA NI MAPUNGUFU MAKUBWA WA HAKI NA SHERIA ZETU ZA NCHI, NA PENGINE NI UDHAIFU WA SERIKALI YETU KATIKA IDARA HUSIKA, WANASHERIA MPOO NA MESIKIA HALI YA HUYU JAMAA YETU HUU NI WAKATI WA KUMSAIDIA MWANANCHI MWENZETU, THIS IS A WINNABLE CASE

    ReplyDelete
  30. AnonymousJune 04, 2010

    Hakuna mwajirianayeruhusiwa kumchisha mtu kazi endapo kama ameumia. Huyu mtu ana haki zote za kulipwa. Hata kama ikipita miaka mingapi. Ushahidi unao tosha, hakuna cha rushwa wala nini. Wamekupa address fatilia kwa nguvuzote.

    ReplyDelete
  31. AnonymousJune 04, 2010

    jamani legal rights za kiTZ.Nilishawahi kutafuta legal right kuna kitengo ukikisikia jina utatetemeka pale karibu na sayansi jamani jamani machozi yalinitoka kandanda ni ile ile ya kibongo.ilinifanya kuichukia jamii yangu.watanzania tunadhalilisha ujuzi.MUNGU IBARIKI TZ

    ReplyDelete
  32. AnonymousJune 04, 2010

    Ushauri mwingine Huyo ndugu alieumia achunguze pia kama mwajiri wake alikuwa na bima alitakiwa kudai bima ya kuumia kazini" Kuna waajiri hata hawawaelekezi watu kitu cha kufanya.

    ReplyDelete
  33. AnonymousJune 04, 2010

    Kituo cha sheria na haki ya binadamu.....???? Haki za binadamu gani wanazoshughulikia? Binadamu sisi au?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...