Ndugu wanakijiji,

Tunasikitika kutangaza kifo cha baba wa dada yetu Majoy, Mzee Mathias Mahilla, kilichotokea usiku wa kuamkia leo huko Morogoro. Mzee Mahilla amekutana na mauti yake kutokana na ajali ya pikipiki aliyokutana nayo Jumatatu ya juma hili.

Nikiongea na Majoy kwa njia ya simu leo asubuhi, aliniambia kwamba mzee alipelekwa hospitalini siku hiyo na kuruhusiwa, madaktari wakiihakikishia familia kwamba hakuwa na tatizo lolote la kutisha.

Siku ya Jumanne mzee akawa akishindwa kabisa kula na ilipofika siku ya Jumatano mzee akakat kauli, akawa hawezi kabisa kuzungungumza. Akarejeshwa hospitali na kuwepo huko hadi mauti yalipomkuta.

Shughuli za mazishi zinafanyika nyumbani kwa mzee huko Morogoro, eneo linalofahamika kama Magadu Mzinga, kambi ya jeshi ya Mzinga.

Kuwasiliana na Majoyo na kumpatia salamu za faraja usisite kumpigia kwenye namba 0713 298 373. Mwenyezi Mungu amemjalia nguvu na anaweza kuzungumza nawe bila matatizo.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mzee wetu, Mathias Mahila. Amefariki akiwa na umri wa miaka 58. Mwenyezi Mungu ametoa, Mwenyezi Mungu ametwaa, utukufu uwe nae. Amin

Babukadja Sankofa,
Mwenyekiti wa kijiji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 20, 2010

    madaktari wetu wanajua nini? au vifaa hamna.
    Kuna mtu alienda hospitali kubwa Tanzania, wakamwambia anauvimbe kwenye tumbo ambao unaitaji operation haraka iwezekanavyo...kwenda kucheck india wakamwambia hana uvimbe and alikuwa ana tatizo dogo tu ambalo walimpa dawa and now anadunda na mzima wa afya. akacheck tena UK wakamwambia hana tatizo lolote so dawa za india zimefanya kazi and hospital ya bongo ilizusha au sio ndo wanafanya majaribio kwenye mili ya watu au kuna wezi wa spea za mwilini?
    mdau,
    USA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...