Hujambo Ankal na pole kwa
majukumu yako ya libeneke.

Leo hii asubuhi nimemkabidhi Mwanafunzi wa Dodoma, Chipegwa Masima,
baiskeli ya miguu mitatu ya walemavu na vyoo (viti) viwili. Vifaa hivi
vyote nilikabidhiwa na Mdau Richard wa Dar. Namshukuru sana ndugu Richard na wadau wote walionipigia simu na kutuma email. Sasa Chipega anafurahia na amenituma niwape shukurani zake.

Katika hafla fupi ya kumkabidhi vitu hivyo katika shule anayo soma Chipegwa, walikuwa Afisa Elimu Wilaya ya Chamwino, dada Scholah Kapinga, mratibu wa elimu kata bwana Halifa Iddi, Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Benjaminn Mkapa, bwana Hamid Wahay, mama ya Chipegwa Face Chidole, walimu na wanafunzi.

Nilipoongea na mama yake alisema Chipegwa ana dada yake ambaye naye
anaupungufu wa akili, ana mdogo wake wa kiume ambaye ni mlemavu wa macho (kipofu). Bado misaada inahitajika zaidi kwa familia hii ambayo haina baba kwani alifariki mwaka 2007.

Mungu awabariki woote.
Mdau Godfrey George Kyoko
0787771414, 0715771414
email: info@parenttz.org

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 11, 2010

    Safi sana mkuu! Ila isije ikawa kuna harakati za kutafuta ubunge ndani yake! Maana kipindi chenyewe hiki, kila zawadi inatiliwa mashaka.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 11, 2010

    inatia moyo kuona watu tunaweza kusaidiana kiasi hiki. Mungu awajalie na wengine kidogo kidogo tutajaza kibaba.
    Dada Schola ni wewe tulikuwa wote zoo(iringa)??

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 11, 2010

    wadau ni vizuri tulivyoshirikiana ila huyu mdogo wetu mbona yuko kwenye gari la miguu minne si mitatu au unamaananisha umenunua baiskeli 2 halafu cha pili vizuri dada yetu huyu afungwe kizazi manake ikiwa watoto wote ni wana matatizo inaweza kuwa ana matatizo ambayo ni genetic ndio maana yanawapata watoto. si rahisi kwa sie waafrica kukubaliana na hali ila kama inawezekana hata hospitali wamsaidie kurekebisha mambo.

    Goodjob michuzi, kaka uliyeleta hii stori na kufanya kweli, high five toka massachussets

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 11, 2010

    Ubarikiwe mkuu!! huo ni mfano wa kuigwa na hujaogopoa kupost habari yako na jina na nmba zako za simu...kwani najua wewe ni mdau wa globu hii ya jamii na unawajua waosha vinywa na hilo halijakutisha kwani unataka ujumbe ufike kwa jamii kwamba kuna watu wanahitaji msaada na msaada unatakiwa utoke kwa jamii hii hii!!!! ubarikiwe na washindwe kwa jina la Yesu wote watakao-post comments zao za kukukebehi!!-Michuzi, zibane comments hizo!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 11, 2010

    Loh, mdau acha hizo, siasa wala sizipendi. Na wewe badala ya kutilia mashaka toa msaada kwa ndugu hawa wenzio ambao wanauhitaji. Nimepiga picha nyingi sana na kama unataka niandikie email nikutumie uone maisha wanayo ishi familia hii. Kweli inasikitisha. ungeona nyumba wanayo ishi hata usingesema hayo. Ubarikiwe. Godfrey

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 11, 2010

    hiyo baskeli inaitwa wheelchair ,tafuta maaana yake nzuri

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 12, 2010

    Imeandikwa..."tenda wema uende zako, usingoje shukurani, na baraka itatokana na kuzingatia hilo." Hii ni show game, hamna utu wowote hapo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...