Afisa tabibu katika hospitali ya Machame wilayani Hai,mkoani Kilimanjaro Beatus Sumni muda mfupi baada ya kukutwa akitaka kuiba dawa za usingizi (Pethedine) alizokuwa akizitumia kama dawa za kulevya. Chini akiwa anaonesha jinsi alivyoingua wodini akiwa kavaa kininja
Mkaazi mmoja wa jirani na hospitali ya Machame wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro, Beatus Sumni(29) anadaiwa kuchukua dawa za usingizi(Pethedine),wanazotakiwa kutumia wagonjwa na kujichoma mwilini kama sehemu ya dawa za kulevya.

Hali hiyo ilibainika hivi karibuni ikiwa ni baada ya mtu huyo aliyekuwa mtumishi katika hospitali hiyo inayomilikiwa na kanisa la KKKT dayosisi ya kaskazini,kukamatwa akiingia katika wodi ya kujifungulia wanawake na kutaka kuiba funguo za kabati lilikokuwa likiifadhia dawa hizo.Tukio hilo lililoleta tafrani hospitalini hapo na kusababisha baadhi ya wagonjwa kutoka wodini,lilitokea wakati wa madaktari na wauguzi,wakihudhuria sherehe za mahali ya 39 ya chuo cha Uganga hospitalini hapo.

Sumni anadaiwa aliingia katika wodi hiyo huku akiwa amejifunika usoni kama Ninja alitaka kuchukua funguo za kabati iliyokuwa imehifadhi dawa hizo,ingawa jaribio lake lilikwama baada ya mmoja wa wagonjwa kupiga kelele za kuomba msaada.Mmoja wa wagonjwa aliyelazwa wodini hapo,Lucy Salema alisema alishtushwa na mavazi ya afisa huyo ambaye alichukua ghafla funguo za kabati na kuziweka katika mifuko ya suruali yake.

Kwa upande wake muuguzi mkuu wa hospitali hiyo,Edward Mushi, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa afisa huyO alikuwa mtumishi wa hospitali hiyo lakini alifuzwa kazi Februari mwaka huu kwa madai ya kutumia vibaya taaluma yake.

Alisema kwa mujibu wa uchunguzi uliOfanyika kati ya Januari 12 na Februari 20 mwaka huu walibaini mtumishi huyo aliwaandikia wagonjwa 24 dawa ya Pethedine yenye ujazo wa Miligramu 3200 lakini dawa hiyo alijichoma mwilini mwake kwa nyakati tofauti.

Mushi alisema baada ya mahojiano mtumishi huyo alikiri kujichoma dawa hizo mwilini kwake kwa barua yake ya Februari 12 mwaka huu huku pia akitaka kupewa msamaha kwa kosa lililokuwa likimkabili.

Akizungumzia tukio hilo,Sumni, alikiri kuingia katika wodi hiyo hiyo lakini akafafanua kuwa alikuwa na lengo la kumuona mpenzi wake aliyemtaja kuwa ni Josephine Kabululu ingawa taarifa hizo zilikanushwa na wauguzi kwamba hapakuwa na mgonjwa mwenye jina hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 22, 2010

    Huyo fiksi kaenda kumwona mpenzi na pete ya ndoa kidoleni kaazi kweli kweli

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 22, 2010

    Sishangai maana manurse wengi wanatumia nusu kaputi (wanawake)sembuse mwanamume.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 22, 2010

    pedhedine sio dawa ya usingizi ni dawa ya kuondoa maumivu makali na iko kwenye group la DDA(dangerous drug act)na inatakiwa kupewa wagonjwa waliotoka kupasuliwaau wagonjwa wenye metastatic diseases kwenye mifupa,inashauliwa isitumiwe kwa muda mrefu kwa vile ni rahisi kuwa addicted nayo,na wanapewa wagonjwa ambao wako allegic na morphine.ni hayo tu .

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 22, 2010

    Jamaa anaonekana anatumia mkorogo, pia anaoenekana shoga na ni mtumiaji wa madawa ya kulevya....asaidiwe ana matatizo !! si mwizi, ameshaathirika na hiyo dawa na yuko radhi afanye lolote...mimi nilishawahi kuwa mtumiaji wa Valium dawa ya usingizi, ilikuwa siwezi kulala bila valium na ilikuwa nahitaji kulala siku nzima,kulikuwa na issue imenivuruga akili...ilikuwa nahitaji Valium kwa gharama yeyote, kuna wakati nilikuwa natumia cheti cha dr kilichoandikwa two years ago kuwarubuni watu wa pharmacies waniuzie Valium....it was dangerous!!Nilikuwa nimefeli mtihani wa chuo kikuu na nikapigwa disco!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 22, 2010

    Masikini Mkaka wa watu! Atakuwa na Social Issues. Wataalam wa Counseling wamsaidie jamani.

    Basi wabongo navyowajua watamfungulia mashitaka na kumpeleka lupango! Badala ya kumpeleka Rehabilitation Centre kwa msaada wa kitibabu zaidi.

    Haiwezekani mtu ambaye hana matatizo yoyote ya kijamii au kiuchumi, ajikite kwenye masuala kama hayo ya kutumia hizo vitu za kumpunguzia mawazo. Kwa sababu yeye baada ya kutumia hivyo vitu anajihisi yuko 'high', hivyo kwa muda huo ambao yuko 'high', anasahau matatizo yake 'temporarily'.

    Afanyiwe Counseling tu huyo kwa kweli, then Rehab.

    Vinginevyo akipelekwa lupango yatakuwa ndio yaleyele ya ... ''Mama did not raise no quitters!''. Maana akitoka lupango tu, then, kama kawa! Tena atahamia hospitali kubwa zaidi ili kuongeza dozi - KCMC.

    ReplyDelete
  6. Huyo ni drug addict. Ni ugonjwa, anahitaji tiba! Pole zake.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 22, 2010

    Hii inaonyesha jinsi gani bado tuko nyuma kwenye masuala ya control drugs,huyu bahati kashikwa inaonyesha ni muda mrefu kafanya hayo lakini kungekua na strict regulations za utoaji wa dawa hizo ingepunguza au kuondoa kabisa tatizo hili.Wenzetu huku wana system ya double checks(dawa haitolewi mpaka muhudumu mwingine ahakikishe na funguo ina kabidhiwa mtu maalum mpaka akimaliza shift ana mkabidhi mwingine)kwa njia hii imewezesha watu kua makini na utoaji wa dawa hizi.Ukitoa dawa una hesabu umetoa ngapi na umebakisha ngapi na mwenzio ana hakikisha kiasi ulichotoa ndio kilicho andikwa na daktari kwa mgonjwa muhusika,kama kuna upungufu utajulikana hapo ili uchunguzi ufanyike nani alikua kwenye shift iliopita.Sasa huyu druggie aliupata vipi ufunguo kama alikua kashafukuzwa kazi?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 22, 2010

    Watu wengine bwana,so unrealistic "rehabilitation centre,social issues,counceling blah blah blah"Mawazo ni mazuri lakini huyu kaka yuko Bongo ambako mambo hayaendi kama huko Ughaibuni,tukumbuke hayo.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 22, 2010

    Mambo ya Propofol hayo...Mnamwiga Michael Jackson shauri yenu...

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 23, 2010

    jamani mbona hata huku america watu wanaiba madawa ya wagonjwa. huku hata madaktari wengine wamekamatwa wakiiba madawa ya wagonjwa wao. huyu ni drugie na anahitaji matibabu. huyo kaka hatumii dawa za kujishubua yeye ni mweupe. familia yao wengi ni weupe. wewe uliyesema anajishubua nafikiri ni mkavirondo ambako kwenu watu ni weusi kama kima au makaa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...