
MAREHEMU AMMY TUNU
SHEM (MAMA SHEM)
Familia ya Mama Shem (AMMY TUNU SHEM ) wa Kinondoni Dar Es Salaam aliyetutoka tarehe 02/05/2010 Tunapenda kutoa shurkani zetu za dhati kwa ndugu jamaa Majirani na marafiki wote walioshiriki kwa njia moja ama nyingine kwa hali na mali katika kufanikisha kumsindikiza mama yetu kipenzi, mpendwa wetu nguzo yetu Dira yetu (NANI MWINGINE KAMA SI WEWE MAMA – ASANTE SANA MAMA - Raha ya Milele umpe ebwana na mwanga wa milele umuangazie apumzike kwa amani – Amen) katika safari yake ya mwisho hapa Duniani kuelekea kwenye nyumba yake ya milele na kuupumzisha mwili wake tarehe 05/06/2010 katika makaburi ya Kinondoni Dar Es Salaam.
MISA YA AROBAINI YA MAREHEMU AMMY TUNU SHEM ITAKUWA TAREHE 16/07/2010 SAA 10 JIONI NYUMBANI KWAKE KINONDONI – MNAKARIBISHWA SANA
(IMEKUWA NGUMU SANA KUAMINI KWETU ILA KWA MAPENZI YA BWANA YATIMIE)
Mungu awabiriki ndugu , jamaa , marafiki na majirani wote waliosafiri toka sehemu mbali mbali kuhudhuria mazishi ya mama yetu kipenzi.Watu wa Kihurio same Asanteni sana kweli mlimpenda mama yetu, Watu wa Tanga wakiongozwa na mzee kimbute asanteni sana, Ndugu wa Dar Es Salaam wakiongozwa na Mh. Balozi F.B.Mndolwa, Prof Nkindiwe, Mzee Chrisopher Shemaheze, Asanteni sana , Wafanyakazi wa O.A.U , NEDCO, THB, na UNDP na international Organization nyinginezo, chama cha wastaafu wa UN (UNAPATA) Tunashukuru sana.
Mungu awabiriki ndugu zetu , jamaa , marafiki zetu na majirani zetu wote wa mama shem pale Kinondoni, na sehemu nyingineko kwa ushirikiano wanu mliotupa wa hali na mali, Asanteni sana .
Mungu awabiriki ndugu , jamaa , marafiki na majirani wote wa Rashid (Ramsey) Shem (mdogo wa marehemu) pale Kinondoni Shamba kwa ushiriano wenu
Mungu awabiriki ndugu , jamaa , marafiki na majirani wote wa Mama Mathew (Mrs Magongo) (Mtoto wa Marehemu) pale Mwenge.asanteni sana
Mungu awabiriki ndugu , jamaa , marafiki na majirani wote wa Ezekiel Sekuba (Mtoto wa Marehemu) pale Kibamba asanteni sana
Mungu awabiriki ndugu , jamaa , marafiki na majirani wote wa Angelah Kiyao Sekuba (Mtoto wa Marehemu) pale Mbezi Luisi asanteni sana
Mungu awabariki sana ndugu , jamaa na marafiki na watanzania wote waishio Uingereza kwa upendo wao hekima na faraja walizowapatia Richard Shem Sekuba (Mtoto wa Marehemu) Hellen Mammy Elisaeli Swai (Mkwe wa Marehemu) , Eric W. Masanja (Mtoto wa Marehemu) Odilia Tarimo (Mrs Eric) (Mkwe wa Marehemu) katika wakati huu mgumu
Mungu awabariki sana Waumini wote wa kanisa la Roman Cathoric Mt. Martin De Pores Mwananyamala , kwaya ya VIWAWA Mwananyamala, Madaktari Bingwa (DR Neema) na wenzake pamoja na Manesi na Wauguzi wote wa Hospitali ya Tumaini – Upanga Dar Es Salaam
NI VIGUMU KUMSHUKURU KILA MTU ALIYESHIRIKI KWA HALI NA MALI KWA KUTAJA MAJINA ,BALI TUNAOMBA MZIPOKEE SHURKANI ZETU ZA DHATI KWA PAMOJA , SISI FAMILIA YA MAREHEMU MAMA SHEM TUNASEMA ASANTENI SANA MMETUFARIJI SANA KWA UWEPO WENU HATUNA CHA KUWALIPA NA ILA MUNGU AWABARIKI SANA MUENDELEZE MOYO WENU HUU MLIOTUONYESHA KWA YOYOTE YULE. KARIBUNI TUSALI PAMOJA TAREHE 16/07/2010 KWENYE MISA YA AROBAINI YA MAMA YETUMPENDWA PALE NYUMBANI KINONDONI – KARIBUNI SANA
ASANTENI SANA NA MUNGU AWABARIKI SANA
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LITUKUZWE AMEN
1. RASHID (RAMSO) SHEM – ---- +255765653670 (MDOGO WA MAREHEMU)
2. MRS ELIZABETH MAGONGO -+255713660417 (MTOTO WA MAREHEMU)
3..EZEKIEL SEKUBA--------------- – +255715289134 (MTOTO WA MAREHEMU)
4.Julius Magongo -------------------- +255717100276 (Mkwe wa Marehemu)
5.ROSE SHEM ----------------------- +255713691715 (Wifi wa Marehemu)
R.I.P mama!!
ReplyDeletepole sana jirani yangu mama mathew kwa msiba huo mzito, Mungu aiweke roho ya Marehemu mahala pema peponi, Amen
ReplyDelete