Meneja wa TBL,Fimbo Butallah akifafanua jambo mbele ya waandishi wa Habari (hawapo pichani) katika mkutano uliofanyika leo katika ukumbu wa Idara ya Habari-Maelezo.kushoto ni Mratibu wa Tamasha hilo la Mtemi Mirambo,Amos Mkonga.Meneja wa TBL,Fimbo Butallah pamoja na Mratibu wa Tamasha hilo,Amos Mkonga wakionyesha vipepetushi vinavyoelezea Tamasha hilo kwa waandishi wa habari waliofika katika mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Idara ya Habari-Maelezo

TAMASHA LA MTEMI MIRAMBO TABORA

Chief Promotions imeandaa Tamasha la Ngoma za utamaduni liitwalo MTEMI MIRAMBO,lenye lengo la kukuza sanaa na kuvitangaza vikundi vya ngoma vilivyopo katika mkoa wa Tabora.

Tamasha hilo litaanza kufanyika katika viwanja vya chipukizi Tabora kuanzia Tarehe 16 - 18 Julai,2010 kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 12 jioni.

Siku hiyo shughuli mbali mbali zitafanyika kama vile maonyesho ya ngoma za asili,Sarakasi,Ngonjera na Nyakula vya asili.mgeni rasmi katika Tamasha hilo anatarajiwa kuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Mh.Moshi Mussa Chang'a.

Tamasha hili linakuja kwa udhamini mkubwa toka kwa kampuni ya TBL kupitia kinywaji chake cha Balimi,Bodi ya Utalii (TTB),Zain Tanzania na Merina Investment.

Chief Promotions imesajiliwa mwaka 2003 na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na Baadae Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto,na imefanya kazi na Mashirika mengi tu yakiwemo ya Umoja wa Matiaifa (UNAIDS,WHO,UNDP) na pia imefanya kazi na TBL,NSSF,TACAIDS na mengine mengi.

kwa mawasiliano
Amos Mkonga,
Mkurugenzi Mtendaji,
0755 638004/0655 638004

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. ...Inapendeza, Tuendeleze, Tuzipende, Tuziheshimu na kudumisha mila zetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...