Kutokana na taarifa zilizotolewa na gazeti la HabariLeo la tarehe 19 Juni ukurasa wa 4, na kurudiwa kwenye tahariri ya gazeti hilo la tarehe 20 Juni ukurasa wa 6, HakiElimu inapenda kutoa ufafanuzi kwa umma kuhusu maana, malengo na ukweli wa takwimu za ujenzi wa nyumba za walimu zilizotumika kwenye tangazo letu kwa wananchi.
Tangazo limebeba maneno yafuatayo:-
..“.Mwaka 2008, Serikali ilipanga kujenga takriban nyumba za walimu 22,000, lakini zilizojengwa ni kama nyumba 300; yaani asilimia moja tu. Kutokana na upungufu wa nyumba za walimu, walimu wachache waliopo shuleni wanalazimika kufundisha kwa muda mrefu na hata kufundisha masomo wasiyoyasomea. Hali hii inadumaza elimu. Kuna upungufu mkubwa wa nyumba za walimu. Japo hazitoshi, ni muhimu sasa Serikali itekeleze ahadi ya kujenga nyumba 22,000 za walimu, kama mpango wa MMEM unavyosema, kwa mwaka 2010/ 2011”.
Tunapenda wananchi wafahamu ukweli ufuatao:-
1. Chanzo cha takwimu zilizotumiwa kwenye tangazo hilo ni Ripoti ya Serikali ya Utekelezaji wa MMEM II kwa mwaka 2007/2008 yenye jina la “Primary Education Development Programme II (2007-2011): Annual Performance Report FY- 2007/2008) iliyotolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na TAMISEMI mwezi Agosti, 2008. Katika ukurasa wa 11, kipengele 2.1.2 kinachohusu “Miundombinu ya shule” (School infrastructure), aya ya kwanza. Serikali inatamka wazi kuhusu idadi ya nyumba ilizojenga kulinganisha na malengo yake. Tunanukuu:
“…The target for 2007/8 under this component was to construct 5, 732 pre-primary classrooms, 10,753 primary classrooms and 21,936 teachers’ houses in rural and remote areas. Providing teachers with houses is a positive incentive and motivation for retaining them in their working areas. In the year under review a total of 1, 263 classrooms, 277 teachers’ houses...were constructed..”
Ikimaanisha kwamba (kwa tafsiri yetu):
“…shabaha ya serikali kwa mwaka 2007/2008 ilikuwa ni kujenga madarasa 5,732 ya elimu ya awali. Madarasa 10,753 kwa shule za msingi na nyumba za walimu 21,936 katika maeneo ya vijijini na yaliyo pembezoni zaidi. Kuwapatia nyumba za walimu ni kichocheo chanya na motisha muhimu ya kuwabakiza walimu katika maeneo yao. Kwa mwaka wa mapitio (2007/8), jumla ya madarasa 1, 263 na nyumba za walimu 277 zilijengwa….”
2. HakiElimu katika tangazo lake haikuongelea ujenzi wa nyumba za walimu kwa kipindi cha uongozi wa serikali ya awamu ya nne, isipokuwa imezungumzia utekelezaji wa MEMM II (2007-2011), tena kwa kipindi cha mwaka 2008 tu.
3. Katika tangazo hilo, HakiElimu haijasema kwamba kuna uhaba wa nyumba 22,000 kama mwandishi wa gazeti hilo alivyobainisha. Bali imesema, Serikali ilipanga kujenga idadi ya nyumba hizo, kama nyaraka zake, MMEM II na ripoti ya Serikali ya utekelezaji wake kwa mwaka 2007/2008 (Primary Education Development Programme II (2007-2011): Annual Performance Report FY- 2007/2008) zinavyobainisha.
4. Vilevile, tangazo la HakiElimu halijasema Serikali ya awamu ya nne kwa kipindi chote cha utawala wake imemudu kujenga idadi ya nyumba za walimu zipatazo 300 tu, bali imesema serikali imejenga kiasi hiki cha nyumba za walimu kwa kipindi cha mwaka 2008 tu. Ripoti tajwa inathibitisha hilo.
5. HakiElimu siku zote inazingatia ukweli na ushahidi wa kitakwimu kutoka kwenye nyaraka za Serikali yenyewe, tafiti zake na za wadau mbalimbali. Pia kwa kutembelea na kuona hali halisi kabla ya kutoa ujumbe wowote.
6. Lengo la tangazo la HakiElimu ni kuonesha madhara yanayotokana na upungufu wa nyumba za walimu; ambayo ni pamoja na kuchangia walimu kadhaa kuacha kazi na kusita kwenda kufundisha hasa maeneo ya vijijini na yale ya pembezoni. Hii ni kutokana na kutokuwa na uhakika wa mahali pa kuishi. Ripoti ya serikali pia imebainisha hili. Katika tangazo hili, HakiElimu inaiomba Serikali kutenga pesa kwenye bajeti ya 2010/11 kwa ajili ya kujenga nyumba nyingine 22,000 za walimu kama ilivyopangwa kwenye MMEM II (kwa mwaka wa fedha 2010/11).
7. HakiElimu inatambua mchango wa mashirika mbalimbali katika ujenzi wa nyumba za walimu nchini na elimu kwa ujumla, lakini inaamini kuwa mchango huo hauzuii mipango na bajeti iliyotengwa na serikali kutekelezwa.
8. Dhima ya asasi za kiraia kamwe sio kupongeza serikali wala kulumbana nayo; na wala sio kupotosha umma. Ni kukuza na kupanua wigo wa demokrasia na ushiriki wa wananchi katika kuleta maendeleo. Wananchi siku zote wanafahamu na wanapaswa kuendelea kufahamu kwamba; moja ya kazi muhimu za asasi za kiraia ni kufuatilia utendaji wa serikali katika masuala yote yanayohusu maendeleo na ustawi wa wananchi.

hatuna hela ya kujenga nyumba za walimu lakini tuna hela za kuwapa brazili kuja kutufunga kwetu. kweli maisha bora kwa kila mtanzania
ReplyDeleteMimi nafikiri hili swala la waalimu kutegemea nyumba za serikali lingeisha. Hizo hela zingewekwa kwenye kampuni ya Mortgage kwa ajili ya nyumba na shirika maalum la ujenzi wa nyumba nzuri za kudumu kwa ajili ya waalimu. Waalimu wanaofundisha vijijini wanongezewe house allowance au mkopo nafuu. Waalimu wachukue mikopo wajenge karibu na kijiji au katika mji wanaoishi au karibu na shule, na siyo wajenge wao. Shirika maalum la nyumba lijenge. Namna hii wanapolipa mortgage(Mkopo) pesa inafanya mzunguko na kuendelea kujenga nyumba zingine za waalimu. Mwalimu anapoacha kazi basi alipe deni lote au shirika la mortgage linachukua hiyo nyumba na kuuzia Mwalimu mwingine. Bila kufanya mzunguko wa pesa serikali haitaweza kujengea waalimu wote nyumba. Na hata hizo nyumba ambazo zitajengwa na Serikali zitakuwa siyo za standard nzuri na Waalimu hawatazijali kuzitunza. Lakini, ukimwambia Mwalimu hii nyumba ni yako na wame sign mkataba wa mortgage watazintunza vizuri mpaka watakapomaliza madeni yao. Ndivyo nchi zilizoendelea zinavyofanya na hata miji na vijiji vyao vinakuwa kwa ajili ya credit system. Tanzania has a long way to go! Sorry kwa kuchanganya kiswahili na kiingereza.
ReplyDeleteMdau
Canada
JK na serikali yako..muache kutumia vyombo vya habari vya serikali kutangaza tu mazuri yenu..mkubali kukoselewa..mbona serikali ya Obama inakosoloew na inakubali imekosea..ndiyo uongozi ulivyo
ReplyDeletewewe hapa pakali mwaka wa uchaguzi huuu....mpaka kieleweke....
ReplyDeleteUnavyosema walimu wajengewe nyumba kwa motgage ndugu yangu hapo juu ...hivi unajua hela ya mwalimu anayopata? Kitajenga choo tu na atalipa mpaka afe na vijukuu vyake kama vinaamua kuingia uwalimu nayo vitalipa kweli...Inasikitisha lakini ukweli ndio huo. Bado tunahitaji jinsi ya kuwalipa mishahara mizuri walimu na kuwapa insentives...
Kuwa mwalimu Tanzania ni kama wito wakati nchi za wenzetu ni kazi ya kukuwezesha kuishi...kama huna moyo wa kutumikia ualimu huuwezi kabisa Tanzania..
Ndio maana walimu wetu wanamiradi mingi tu la sivyo hawawezi kuishi na pia kuwa na miradi hiyo kunawafanya wasiweze kujituma au kuwa na muda wakufundisha vizuri. na kwa kutojituma au kuwa makini katika kufundisha wanafunzi wanakua hawafundishwi vizuri. wanafunzi haoa wanatoka wanakua walimu nao wanakwenda kufundisha wakati walikua hajafundishwa vizuri na maisha magumu nao wnatumia muda mwingi nje ya madarasa, then wanafunzi wanakua hawafundishiwi viuri na walimu wanakua hawajui wafundishacho ... mwisho wa yote elimu yetu inakua mbaya mbovu ya low standard Aliyeulizaga kwanini wanafunzi wetu hawafanyi vizuri international nadhani jibu umelipata hapa.....
Sio kila hoja au issue lazima aitolee majibu.Hivi sasa Rais wetu anakurupuka na kusikiliza ushauri wa watu wanaompotosha.Mimi ninaamini HakiElimu ni shirika makini na ndio maana matangazo yao yanatumia takwimu.Hata ishu ya ujenzi wa Udom alikurupuka kujibu hoja ya Zito kwa kuwaita wanafunzi na kuwahutubia ili kujibu hoja.Tunamuomba Rais wetu atulie huu ni muda nyeti wa yeye kupoteza umaarufu kwa kujibu kila hoja.Mbona Mzee wetu Ben alikuwa anakula kabunyau tu hata kama dude ni zito.Yeye yuko safi wanaomuangusha ni watendaji na washauri wake na ndio maana wanamdanganya na kumshauri madudu kila kukicha.Kikwete ukipata nafasi tena fukuza hao watendaji na washauri wajinga wajinga.
ReplyDeleteanony wa 01:30 nimeks=usoma vizuri. Ni ajabu na kweli kwamba Kikwete na wenzake wanataka kutuaminisha kwamba waoni malaika hawakosei kitu ambaco si kweli jamani. Yakiwepo mazuri mmefanya its ok ndio kazi tuliyowapa sasa kama hamtaki kukosolewa then hiyo ni serious kwa kweli.
ReplyDeleteKwani nini kimetokea tena HakiElimu? Duu, This country bwanaaaaaaaa????????????!!!!!!!!!! Wameshapigwa kibano tena nini, mbona taarifa ziko wazi tu. Kura yako mtanzania mwezi wa kumi uitumie kikamilifu kuchagua waukweli.
ReplyDeleteMchangiaji bw. Ally, mawazo yako hayatekelezeki kwa sababu walimu wanahamishwa. Chukua mfano kwamba mwalimu ambaye kwao ni Ukerewe mwanza anapangiwa kazi Nkasi Rukwa na anakopeshwa nyumba, akihamishwa inakuwaje? utaratibu huo unawezekana mijini tu ambapo hata ukihama unaweza kupangisha nyumba.
ReplyDeleteHAKI ELIMU HAMNA HAJA YA KUJIELEZA HAPA, WANANCHI WA NCHI HII TUNAWAKUBALI SAANA NINYI NA TAMWA NDO WATETEZI HASA WA WANYONGE NA SAUTI ZA WASO NA SAUTI
ReplyDeleteKEEP IT UP GUSY
...Ukiona hivyo ujue "Ujumbe wa Haki Elimu Umefika".
ReplyDeleteMr. Ally,
ReplyDeleteOpinion zako ni nzuri, lakini walipe morgage kwa mshahara gani? Dar es salaam yenyewe credit system imeshindikana. Huko vijijini ndio itawezekana?
Haki elimu wasitafute kujikosha ni kweli wamekosa kwani mtu anaesikiliza tangazo hilo leo atapata picha gani? Takwimu za 2007/2008 unatolea tangazo leo 2010/11 ni jeuri na dharau kwa serikali yetu, Serikali inalijuwa hilo tatizo na wanajitahidi kadri ya uwezo na mpaka sasa nyumba zaidi ya elfu 7 tayari hivi kweli unaendelea na mfano wako wa nyumba 300? Wanabidi wakiri na waache kuwavunja watu moyo!!
ReplyDeletehaki elimu kazi nzuri, endeleeni kuwafafanulia hao waandishi inapobidi, lakini kutoelewa kwao kusiwakatishe tamaa, haya ndio matokeo ya kukosa mazingira mazuri ya kufundishia kwa mwalimu, ndio maana tuna waandishi wengi (sio wote) mambumbumbu.
ReplyDeleteWaandishi wa habari Tanzania wengi, sio wote, wana upeo mdogo sana. Huwa wanarukia tu mambo na kuyaandika bila kufanya utafiti hata mdogo wa kuhoji wahusika wawili-watatu. Na pia kuna tatizo sana la vyombo vya habari kuwa vipaza sauti vya propaganda za wamiliki. Vinatetea wamiliki wao bila kufuata ukweli, hata pale walipokosea wanataka kuwapamba. HakiElimu imefanya utafiti na kutumia nyaraka za serikali yenyewe. Kama mwandishi wa HabariLeo anapingana na ukweli juu ya tangazo la HakiElimu na aseme sasa. Ametumia takwimu zipi kazipata wapi? Amefanya utafiti gani? Anajipendekeza kwa JK ili apate nafasi serikalini kama akina Seth Kamuhanda, Salva Rweyemamu na waandishi wengine waliokwaa mavyeo serikalini?
ReplyDeleteHaki Elimu hongereni kwa kupevuka na Advocacy skills (unajenga hoja kwa utafiti na kwa kutumia taarifa sahihi)
ReplyDeleteMwalimu: Alikua anaitwa anaitwa..... KINJEKITILE NGWALE.
ReplyDeleteMwanafunzi: Kwenyekitabu wameandika CHABULUMA.
Mwalimu: Eeh huyo huyo.
Msg sent! big up HakiElimu mkoo juu sasa. Toeni ka - analysis ka ahadi za kiwete vs utekelezaji ili tujui utekelezaji ni asilimia ngapi
ReplyDeleteKWA KWELI HAKI ELIMU MIMI BINAFSI NAWAKUBALI SANA TOKEA ZAMANI MATANGAZO YENU YOTE YANAKIDHI MAISHA HALISI TUNAYOYAONA SISI WANANCHI WA KIPATO CHA CHINI maadamu mnatumia data za ukweli endeleeni kuchapa kazi sisi tunawaombea M/Mungu azidi kuwalinda
ReplyDeletewe anonymous wa fri jun 25, 09:36:oo hebu waambie hao wavivu (serikali) watoe takwimu nyingine haki elimu watazitumia kwenye matangazo kwa faida yako, ingawa faida hiyo huioni kwa sababu ya hali ya mwalimu aliyekufundisha.
ReplyDeletewewe mchangiaji wa Friday june 25 09:36 unashangaza kweli, unaonekana huelewi mambo ya ufuatiliaji, nakushangaa unashangaa hakielimu kutolea tangazo bajeti ya mwaka 2007/2008 ulitaka watoe tangazo hilo lini? katika masuala ya utekelezaji wa miradi ni lazima ujipe muda na huu ndio muda muafaka wa serikali kuulizwa kilichotokea kwa bajeti yake ya 2007/2008 kipidni hicho kilichopita kinafaa kabisa kuwa kipimo cha utekelezaji wa kilichotokea. au ulitaka tangazo litoke 2009, hii ingekuwa mapema sana, embu jifunze habari ya Monitoring and evaluation kidogo ndio ulete hoja hapa. serikali inapaswa kuulizwa, kwa staili ya aaina yeyote hata ingepita miaka 10 kama serikali ilitoa ahadi ambazo haikuzitekeleza sasa unatakaje? Nashangaa unaishambulia Hakielimu, imethubutu na imetumia nafasi yake ya uwatch dog vizuri, laiati NGO zote zingekuwa hivi mambo yangeshabadilika kitambo! na mind you, that is a very sensitive part, we unaona serikali imeonewa, leo nenda shule ya msingi Sakasaka B iliyopo wilaya ya Meatu mkoani shinyanga halafu ukirudi uone kama utaona kama hakielimu wamefanya kosa kuikumbusha serikali.
ReplyDeleteKwenye mamba hata kenge wapo, wewe anonymous unayesema takwimu za 2007/2008 linatolewa takwimu mwaka 2010/2011 hivi umewasikia wanasema lengo la tangazo lao nini au unakurupuka tu au wewe ndio wale mnaotaka mpewe sifa na serikali. Kwa taarifa yako mwaka 2010/2011 bado haujaanza hadi July 1 wanachofanya HakiELimu ni kuwaambia serikali watimize lengo lao kwani sasa ni kipindi cha bajeti na mipango ya 2010/2011. Taarifa za utendaji wa 2009/2010 sisi watendaji serikalini ndio tunaziandaa sasa watazipata wapi? Hivyo HakiElimu kwa mara nyingine mko juu na mko current na poleni sana kwa kuitwa waongo ,wanafki na msio na utafiti ,UKWELI UKO WAZI. Ebwana tunasubiria vitu vingine nina uhakika mmejiandaa ,jamani HakiElimu hawajafungiwa watakuwa wanajisafisha kutokana na kauli za Mheshimiwa kuwaita waongo ,wanafki na wasiofanya utafiti halafu Mhariri mmoja sijui katoka wapi na yeye akaaandika tahariri ya kuwashtutumu nashangaaa kwanini hawatoi kazi hiyo kwa watu makini kama Ankal Michuzi, yaani tunazidi kukereka na tabia hizi za wahariri wabovu hivi ANKAL bado upo daily news? umfikishie mhariri wa habari hiyo
ReplyDeleteWhat a big shame kumbe hata sifa zote juu ya ujenzi wa shule za kata ukifanya analysis hazijatimia malengo embu someni tena ripoti ya utekelezaji uone walipanga kujenga madarasa mangapi na wakajenga mangapi tena kwa kukategorize pre-primary and primary kisha wakati wa kureport ikatajwa kwa jumla yani ni chini sana, me naona serikali wakae kimya unapochokoza watu kama hawa watafichua na waliyomeza! Siamini kila siku wanamdanganya mheshimiwa kwani hana radio na TV ya kusikikiliza walichosema jamaa mbona kiko wazi kabisa wamsiwatishie HakiElimu tisheni watendaji
ReplyDeletehuwa lazima nifatilie matangazo ya HakiElimu kwa ukaribu sana maana wanatoa taarifa zenye akili sana kwa sie wenye akili zetu!!
ReplyDeleteyani hata msipojieleza umu,wanainchi wenye akili uwa tunawaelewa sana na TUNAWAPONGEZA
sio matangazo ya kuchangia chama eti na wewe je?aagggrrrrr
Hata kama takwimu zimepitwa na wakati, lakini zipo VALID kwa nyakati zinazotajwa ktk tangazo. Haki elimu wanafichua vitu ambavyo mwananch wa kawaida havijui au hawezi kuvi-figure out; Big up, I love u guys ingawa wala sijui nani mwanzilishi nani mfanyakazi. Kazi nzuri... Mkimuona Kayumba mwammieni nimemmiss kumuona ktk TV
ReplyDelete