Katibu mkuu wa TFF FREDRICK MWAKALEBELA
na FLORIAN KAIJAGE Afisa Habari wa TFF

Shirikisho la soka nchini TFF limetangaza viingilio
vya mchezo wa kirafiki kati ya TANZANIA na BRAZIL utaopigwa neshno June 7, 2010

VIP A: laki mbili.
VIP B: laki moja na nusu.
VIP: C laki moja
Rangi ya chungwa mkabala na VIP elfu themanini.
Rangi ya chungwa nyuma ya magoli elfu hamsini.
Rangi ya bluu na kijani mzunguko elfu thelathini.
Lakini TIKETI za laki mbili zimeisha

Chanzo cha habari

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 01, 2010

    Hii ni biashara kichaa. Mchezo wa mpira unatazamwa na watu wengi lakini wengi wao ni watu wenye kipato kidogo hivyo hakuna watu wakutosha kununua hizo tickets. Uwanja utakuwa mtupu kabisa.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 01, 2010

    siyo siri TFF wameonyesha tamaaa sana kwenye viingilio vya hii mechi,katika viingilio vyao wamejaribu kuwabagua watu wa chini,wenye kipato chini laki tatu na nusu....Na hii yaonyesha wanaopenda burudani ni wenye kipato kikubwa which is not true,ukijaribu kufuatilia record za nyuma kwenye mechi za simba na yanga wanao ingia/kuchangia kipato kikubwa ni wasio na kipato kikubwa na tena wao ndo wanaotoa motisha kuchangia timu mojawapo kushinda,sasa swli linakuja hao watakao toa laki mbili(wavaa suti) wataweza ku-shout na kuwawezesha Taifa Star ika-shine hapo 07/06...?Au TFF wame target kukusanya viingilio vya nchi jirani tu...actualy this is un fair..!na pamoja na viingilio kuwa juu hili lakini mwisho wa siku utasikia wamekusanya mapato kidogo na wakati mpaka sasa tumeambiwa tiketi za laki mbili zimeisha...Ushauri wangu Viongozi wajitahidi kufatilia MAHESABU ya tiketi kwa kina moja after another...Hayo ndo maombi yetu walala hoi tusio kuwa na laki mbili za kuona burudani wakati tunaipenda...
    Its me Mpenda Kabumbu

    ReplyDelete
  3. MliakuvanaJune 01, 2010

    Since I am entitled to my own opinion, I, personally think the prices are ridiculous! If they were Simba vs Yanga prices + 10,000 Tshs more than I could have considered attending. But as it is right now - manyage, ndimugayesida nene!

    I am stayinghome and watching the game on TV!!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 01, 2010

    Ikiwa bei za tickets ndio kwanza zinatangazwa itakuwaje papo hapo tuambiwe za laki mbili zimeshakwisha? zilikwishaje kwishaje kabla ya kutangazwa bei yake? hizi tickets zimeuzwaje? au ndio zimeshatengwa ili kugaiwa wakubwa na vigogo wengine ambao wengi wao hawajawahi hata mara moja katika maisha yao kuja kuona mechi za taifa stars?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 01, 2010

    HAYA NDIO MUONE FAIDA YA KUWA NA VIWANJA VIZURI SASA MTAONA MAFANIKIO YAKE

    MIHELA HIYO ITAKAYOINGIA SASA ONGEZENI KUJENGA VIWANJA VINGINE VIPYA NA VYA KISASA ZAIDI

    NA JITAHIDINI KATIKA SUALA LA HUDUMA BORA HAPO UWANJANI NA SIO KUANGALIA MIHELA TU

    HUDUMA BORA ULINZI,USAFI,NIDHAMU,NK

    INGEKUWA TOKEA MIAKA YA NYERERE TUNA MIVIWANJA MIKUBWA NA YA KISASA KAMA HUO WA SASAHIVI BASI TUNGEKUWA MBALI SANA

    TATIZO VIONGOZI WOTE MACHO YAO KWENYE RUZUKU TU

    MAMBO MUHIMU YA KUINGIZA MIHELA KWA NJIA RAHISI KAMA HIZO HAWAANGALII NA KUITANGAZA NCHI VYEMA

    SASA TUSIKUMBUKE YALIYOPITA TUGANGE YAJAYO WAKATI NDIO HUU WA KUINUA NCHI YETU

    NA UHAKIKA BAADA MIAKA FULANI MASHINDANO MAKUBWA YATAWEZA KUFANYIKIA NCHINI KWETU KAMA VILE AFRICA CUP

    MUNGU IBARIKI NCHI YANGU
    MUNGU WABARIKI WATANZANIA WOTE KWA UJUMLA

    MUNGU DUMISHA AMANI YA NCHI YANGU TANZANIA

    MUNGU WAANGAMIZE WALE WOTE WANAOLETA UCHOCHEZI WA KUHARIBU AMANI

    MUNGU WAANGAMIZE WALE WOTE VIONGOZI MAFISADI WALIO WABINAFSI KATIKA MALI YA UMA

    MY HEART IS ON MY HOME COUNTY TANZANIA.

    mdau wa mahakama kuu ya dunia nawakilisha.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 01, 2010

    Viingilio vikubwa sana hasa kwa wafanyakazi na wafanyabiashara wa kawaida, lakini kwa wakazi wengi wa dar es salaam sidhani kama hiyo 30 alfu ni kubwa saana ukitaka kudhibitisha hilo tembelea kuanzia majira ya jioni njia kuu za kutoka mjini hadi maeneo ya mbagala,bunju,kibamba,gongolamboto,tabata kigogo nk uone jinsi baa zilivyojaa watu.Wapenzi wa mpira nadhani watachagua soka kuliko bia kwa siku hiyo.All in all TFF viingilio mmeua!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 01, 2010

    ktk familia ya watu wa5 itabidi baba awakilishe familia

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 01, 2010

    LAKI MBILI NI KARIBU NA POUND 100, HAPA UK HATA WAKIJA BRAZIL NA ENGLAND KIINGILIO SI £100, HUO NI WIZI, PENGINE WANAWEZA KUSEMA WANAFANYA MAHESABU YA KUWA WATAINGIA WACHACHE KWA VILE WATANZANIA WENGI PESA NI HABA SO WAMEWEKA KIWANGO KIKUBWA KUZIBA HILO PENGO WAKA HUKU UK WATU WENGI UINGIA KWA BEI NDOGO HIVYO GHARAMA INAWEZA KURUDI, LAKINI HATA NA HIVYO, NAHISI PESA ZILIZOWALETA BRAZILI NI ZA SERIKALI NI ZA WALIPA KODI WANGELIFIKILIA HILO NA KUWEKA KIWANGO CHA CHINI ILI WAINGIE WENGI WASIFIKIRIE KURUDISHA PESA KWA VILE NINA UHAKIKA SI ZA KUKOPA NA WALA TFF HATAKIWI KUZIRUDISHA. VITU KAMA HIVI NDIVYO VINALETA MATABAKA NA KUTANUWA MWANYA WA WALIONACHO NA WASIONANCHO NA KUKUZA CHUKI NDANI YA JAMII ZINAZOWEZA KUPELEKEA VITENDO KAMA VILE VYA WIZI UJAMBAZI NA UDOKOZIU MAKAZINI ILI KUTAFUTA KUFANANA

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 01, 2010

    Tiketi ya season nzima kwa uwanja wa nyumbani kwa west ham ni pound mia tatu na nusu sawa na laki saba.
    Manchester na Chelsea kiingilio sio pound mia ambayo ni sawa na laki mbili.ni pounds therathini hadi arobaini sawa na elfu themanini.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 02, 2010

    Mimi naona hivyo viingilio ni fair kabisa ukilinganisha na hela waliyolipa na timu inayokuja. It could nbe more. Mbona ticket ya US open tennis zina uzwa mpaka $3000 na watu wanaingia wenye hela zao? Hao hapo ni watu wa biashara. hella zao walizowekeza ni laxzima zirudi.

    Sioni sababu ya kukasirika na sina uhakika na hili lakini hiyo TFF sio public sector na hawalipwi na taz za watu hivyo wanaweza kufanya vyovyote watakavyo.

    Na 30,000 mbona ndogo kabisa hiyo

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 02, 2010

    Bongo tambarare mkiletewa reality check watu mnahaha...Ndio maisha haya kama mnauza kiwanja hatua 20 kwa million 5 na kinauzika bila masihara lazima muwe na hela za kuingia kwenye huu mpira...Msituangushe bwana mtu wakilishe kwenye huu mpira isije uwanja ukajaa wakwe zetu na mashemeji zetu tu.

    ReplyDelete
  12. Mume Wangu, Mikanjuni TangaJune 02, 2010

    LAZIMA HAYA MAFUTA YA KWENYE GARI YA BOSI WANGU NIYANYONYE ILI NAMI NIPATE KUONA HII MECHI

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 02, 2010

    KUPANGA NI KUCHAGUA,
    SASA WATANZANIA NDIYO TUTAJUA KUWA MPIRA NI GHARAMA,
    TUONDOE MAWAZO YA KUFIKIRIA KUWA BRAZIL WATACHEZA NA SISI KATIKA MPANGILIO WA 'MSAADA' KAMA AMBAVYO TUMEZOEA. MPIRA NI GHARAMA NA UKITAKA KUONA A WORLD CLASS SQUAD NI LAZIMA TULIPIE SISI WAPENZI WA MPIRA, HAKUNA SHORT CUT.
    SASA HIVI HAPA UGHAIBUNI VIPINDI VYA MICHEZO VYOTE PAMOJA NA MAMBO MENGINE VINAZUNGUMZIA MECHI YA BRAZIL NA TANZANIA...HUU NDIYO WAKATI WETU WA KUSIKIKA KAMA TUPO, TUSINGOJE KUZUMZIWA KWA MABAYA TU KILA SIKU.
    KWA TAARIFA TUSIPONUNUA TIKETI WAKENYA, WAGANDA, WARUNDI NA WANYARWANDA WATANUNUA NA KUJAZANA KTK WANJA LETU

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 02, 2010

    There is nothing like paying whoever a price here, hiyo inaitwa "APPEARANCE FEE" Newzealand team ilipokuja tuliwalipa $ 40,000, hii ni timu kubwa kama mnavyojua, lakini ukubwa wake haukupewa, imeutengeneza na sote hata wasiopenda mpira wanafahamu fika kuwa Brazil ni timu kubwa. Mtu yeyote asiyependa mpira ataipenda Brazil au Mchezaji wa Brazil atamfahamu kwa jina kamili.
    Brazil tunawapa heshima yao stahiki wala si kuwalipa. Mnachosahau watu wengi ni kwamba tukichukulia mpira au kazi nyingine yoyote serious inalipa, Mbona watu wanalipwa kuuza maneno yao ya busara? Mbona watu wanalipwa kwa kuandika maandishi yanayoelimisha au kukosoa?
    Kila kitu kina gharama yake, hata timu yetu ikifikia viwango hivyo italipwa tu, sasa tatizo kubwa ni kuwa taasisi binafsi na hata za kiserikali zimekuwa zikifanya siri fedha kama hizi tunazolipa kwa watu wanaotutembelea kutufundisha kwa njia mbadala kwamba tukiwa serious kama wao tutafanikiwa. Hii imewakatisha sana tamaa watu wetu wengi kwasababu hawajui umuhimu wa wanachokifanya, wanaona kama wanapoteza muda tu. Watanzania wenzangu, chohcote unachofanya kitakuwa na maana na thamani kama utakifanya kwa moyo wako wote, utakithamini na kukiamini kuwa kitakutoa. Usipoteze muda wako kufanya unachopenda maishani, fanya unachoweza. Kumbuka kila muda unaopoteza ndio unadetermine maisha yako. Waliotutangulia kiustaarabu walisema, "KITU HUWA NA THAMANI PALE TU THAMANI YAKE ITATHAMINIWA".

    Asanteni,

    DMR

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 02, 2010

    ushenzi mtupu

    1.tickets za laki 2 zilikua ngapi na zimenunuliweje kabla taarifa hazijatoka kwa umma?
    2.nani ametoa pesa kulipa brazil waje na shilling ngapi?source?
    3.nyie mwabwana wawili wa TFF msiuze nyago apo mnatia kinyaa tu
    4.nasubiri matokeo ya iyo mechi kuanzia mahudhurio na mapato yatayopatikana
    5.yani ata kama ndo USIRI wa nini sijui,mnatuona mafala sana sie wanainchi

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 02, 2010

    Watu bwana! Kila mtu anaongelea laki mbili, sio sawa, acheni kungalia kwa juu juu, Shs 200k ni kwa viti 748 kati ya viti 57,800, majority ya viti bei ni 50k kwenda chini. Hivi niulize kama Manji anataka kwenda uwanjani nae alipe 30k, mnajua price descrimination kweli? Pia fikiria kitu kama NMB ambao ni official sponsor wa taifa stars, wakurugenzi wake nao walipe vijihela?! lets be serious, leteni hoja kwa bei ya majority yaani Shs 30k to 50k. mimi nasema ofkoz sio bei chee lakini ni muafaka. Zimbabwe na uchumi mbovu wao majority wanalipa US $ 15, sisi na uchumi wetu mzuri tunalia na US $ 20 to $ 35?.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 02, 2010

    Naoma mwakalebela unatafuta hela ya kampeni ya Ubunge october!

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 02, 2010

    Acheni kuchonga hapa !1 hao wenye first class tickets ndo wanao waleta hao brazil ! nyie wengine ingieni uko kwingine mwarudishie watu pesa zao !1
    Am among waliyo kuwa na ticket first class baba kanipa

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 02, 2010

    Tanzania media reports say the east African country paid up to $2.5 million as a match fee to the Brazilians.
    source bbc

    !! waliyo changa hizo pesa wangekuwa wana moyo kama huo wa kuchanga kwenye matatizo ya jamii tanzania tungekuwa mbali.

    ReplyDelete
  20. AUNT YA KAMAUJune 02, 2010

    SASA NAONA MMEANZA KULIALIA ETI VIINGILIO VIKUBWA KUMBE KISA CHA NINI KUTUKANA WABEBA BOX? MBONA DOLLAR 200 AMA 50 NI PESA NDOGO SANA KWA MBEBA BOXI BASI MTUPIGIE MAGOTI TUWATUMIA ILI MKAONA BRAZIL SISI HUKU BRAZIL WAKIJA HATUWAPI HELA NA VIINGILIO NI DOLLAR 5 MAANA BRZIL WAKIJIFANYA WAJANJA NEW YORK HAWAIONI NA VIZA HAWAPATI, SASA INABIDI WAWE MABWEGE KAMA NYIE MKIJIFANYA WAJANJA BRAZIL HAWASHUKI HAPO DAR MNABAKI KUWAANGALIA KINA MRISHO NGASSA NA NJANSIGWA HAHAHAHAHAHA!

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 03, 2010

    It's been a while since i checked on Michuzi's.I almost forgot how negative people can be up in here.Just go enjoy the game if you can or stay home and turn on your TV.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 03, 2010

    kwanza mshukuru hata kwa hizo TV mtaona kwa bure siye huku kidogo tu unasikia PPV...$70.00 ...ngumi za dakika ishirini ukitaka kuangalia nyumbani. Hiyo hela ndogo sana tu...

    Mnalalamika ticket za $200 zimeishaje wakati hamuwezi kulipa hata $30 kwanza.

    mnasema wanacharge ghali wakati mmesema wametupa hela kuwaleta hao wachezaji. Mnapenda vya deso tu..Mnataka kuiona game lakini hamtaki kulipa...ndio maana lebron analipwa hizo hela...kwa vile watu wanapay kuona game.

    waliosema hapo juu this is reality check hawakukosema. mnawasema wabeba box kumbe hela za matanuzi hamna...Ngoja tuwatumie mkaone japo kidogo najua SA ndio kabisa hapakanyagiki...budget yake hamna kabisa

    Ndio sababu wale wenye movie yao sijui inaitwa nini tena kila siku wanaifungua Uk mnalalamika kwanini unafanya premier huko ..kwanini huifungui hapa....wakale police...mmzezoa kubootleg kila kitu...mshukuru TV itaonyeshwa bure hiyo soccer mataiona la sivyo......

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...