Dunia kigeugeu

Kikosi kazi cha FM Academia
Wazee wa Pamba, Bendi ya FM Academia, ndiyo itakayotumbuiza katika shindano la kumtafuta mrembo wa Redds Miss Ilala 2010 linalotarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar Juni 26, Jumamosi hii.
Mwenyekiti wa kamati ya Miss Ilala Jackson Kalikumtima amesema mambo yote yako sawa juu ya bendi hiyo na pia msanii wa ngoma za asili Wanne Star atakuwepo katika kutoa burudani katika shindano hilo litakalokua la kuvutia kutokana na mikakati iliyowekwa kuhakikisha mambo yanakuwa makubwa.
Ameongeza kuwa kwa sasa warembo wote wako safarini mkoani Tanga ambapo wanafanya ziara ya kimafunzo na tayari jana usiku walihudhuria shindano la Miss Tanga na pia wameshatembelea vivutio mbalimbali vya utalii kama vile mapango ya Amboni na kujionea mambo mbalimbali na leo wanatarajia kuanza safari ya kurejea jijini Dar es salaam.
Ameongeza kwamba kiingilio katika shindano hilo kitakuwa katika sehemu tatu ambazo ni VIP 1 shilingi laki 100.000 VIP2 shilingi elfu 50.000, na kawaida ambapo kiingilio kitakuwa ni shilingi elfu 10.00 kwa kila mtu, amewataka mashabiki wa urembo kujitokeza kwa wingi katika shindano hilo kwani mwaka huu kiuna mambo mengi mapya ambayo watayaona na kuyafurahia.
lakini msije kutudanganya ka mwaka jana wakati lundega alivo tangaza eti Kofie atatumbuiza halafu asitokee na wala asitoe hata taarifa.
ReplyDeletenasubili kuwaona FM wakiwa kwenye jukwaa la miss ilala kwa mara ya kwanza.
wamekwisha hawa. nasikia siku hizi mpaka wapige show na jahazi ndio wapate watu. ukienda kwenye show yao, ankal wanaboa sana. maneno kibao halafu nyimbo hazina hata mpangilio. kazi yao kujisifia tu kama timu ya mpira ya uingereza, pafomannsi sifuri. sie tuko na twanga tu, mpaka wajirekebishe wawe kama walivyoanza. hatuendi pale kuangalia sura au majina, tunafuata burudani.
ReplyDeleteYaani jamani Mi huyu Young Millionaire (Patcho Mwamba!). Yaani wee acha tuuu!
ReplyDeleteUle wimbo wake alioimbia Emanuel's, na wale wadada wamevaa vibukta vya blue, jina la Wimbo kidogo limenitoka, naufagilia si kipolepole.
michu eeh tuwekee live wazee wa ngwasuma wakipafomu mzee tuwekee youtube tuzinyonye.
ReplyDeleteWee Msafir, Khaaa! Hebu tumia tafsida kidogo! Lol.
ReplyDelete