Za saizi mkuu (Shikamoo)
pole na kazi ,
Naomba kupata fursa katika blog yetu ya jamii kuelezea machache kuhusu uvamizi wa mashamba ya watu unaofanywa na viongozi wa serikali ya mtaa wa kimara Mavulunza (Bonyokwa).
Nachukua nafasi hii kuandika malalamiko haya nikiwa kama mmoja wa watu niliovamiwa. Na pili kwa Mhe. Raisi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kufahamu kwamba kuna viwanja ambavyo vilitengwa kwa ajili ya makaburi, lakini viongozi wa serikari ya mtaa kwa kushilikiana na diwani na Mjumbe, wamegawiana na kuchukua viwanja Vya watoto ambao ni yatima na kuvigeuza makaburi.
Nachukua nafasi hii kuandika malalamiko haya nikiwa kama mmoja wa watu niliovamiwa. Na pili kwa Mhe. Raisi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kufahamu kwamba kuna viwanja ambavyo vilitengwa kwa ajili ya makaburi, lakini viongozi wa serikari ya mtaa kwa kushilikiana na diwani na Mjumbe, wamegawiana na kuchukua viwanja Vya watoto ambao ni yatima na kuvigeuza makaburi.
Kiwanja chenyewe kipo mlimani! Hivi ushaona wapi marehemu wakazikwa kwenye mteremko ( bondeni) ambapo mvua kubwa ikija majeneza yanaweza kuonekana na majirani wa eneo hilo wanapinga kitu kama hicho kilichofanyika.
Kisa hiki kimetukumba sisi ambao ni yatima na shamba letu hilo tuliachiwa na wazazi wetu. Na mwaka jana mwezi wa 8 serikari ya mtaa katika kipindi cha maandalizi ya chaguzi za serikari ya mtaa walivamia na kuweka bango shambani hapo linalo sema “ SHAMBA HILI LIMECHUKULIWA NA SERIKARI HAIRUHUSIWI KUFANYA SHUNGULI YOYOTE” nakusema wanataka kujenga Shule, Hospitali na sehemu ya makabuli, Lugha ambayo waliitumia kupiga kampeni kwa wananchi wa eneo hili kuwa watawapatia vitu hivyo.
Cha kushangaza ama kusikitisha hamna cha barua ya serikari wala wizarani na nilipo mfuata mwenyekiti wa serikari ya mtaa ambaye alikuwa ana hamia mtaa mwingine aliniambia hawatutambui lakini anaweza kutusaidia tu kwa kutugawia kiwanja. Wakati zoezi la leseni ya makazi lilipofanyika shamba letu liliandikishwa kwa majina yetu ambao tupo watatu na mpaka kwenye ramani tupo na tukaenda wizarani na wizara kutambua sehemu hiyo kama ya makazi.
Kesi hii tumeifungua ofisi ya kata kimara Baruti chakushangaza mpaka sasa wamekuwa wanairusha rusha pasipo kuisikiliza toka mwaka jana mwezi wa nane mwishoni. Wametupa stop order lakini waliendelea kuzika na wamesha uza viwanja walivyo gawiana,Tumeanzia kata tukijua ndipo mwanzo kwa wao kuweza kuona na kuweza kutoa maamuzi wakiwa kama ni watendaji wao wakuu lakini nao wanaoneka kusita sita katika kutoa maamuzi wakihairisha kesi kila mara ili tukate tamaa.
Nimeelezea haya kwa ufupi hasa baada ya rahisi wetu Mhe Kikwete kutembelea maeneo haya ya kimara na kuwa anajua utendaji mbovu wa watendaji hao pamoja na madiwani ambao ni makada wa CCM. Na hii ni kuonyesha na kukumbusha kuwa wapo katika kutetea wananchi na sio kuwaibia.
Kwa dizaini hii MAISHA BORA NI NDOTO
Mdau Kimara Mavulunza
Pole ndugu yangu, na siku zote cha mnyonge ndicho huliwa na wenye nguvu, hata hivyo hakijaharibika kitu, naona una nguvu kisheria japo mabavu yanatumiak, kama kweli shaamba lenu linatambulika mpaka wizarani na kwenye ramani mmo sioni kama mtapoteza haki yenu ila inaweza ikacheleweshwa sana. nakushauri habari za kata achana nazo nenda kwenye ngazi iliyo juu ya hiyo kata ili kama ni kuwajibishwa iwajibishwe, kama kuna nia mbaya iliyofanywa na hao viongozi ni kwamba huo ni mktandao na kwenye ngazi ya kata watakuwa wanjuana, na pia unapokuwa unachukua hiyo hatua hakikisha una ushahidi uleee wa ramani ya wizara, inuka, fanya hima maana unavyozidi kuchelewa ndivo hivyo hivyo wenye uchu wa ardhi, kaburi lao wenyewe wanapopata mwanya wa kujipanga upya, au kama ukiona wewe mwenyewe huwezi basi fanya mpango uweke hata wakili wa kukusaidia, ndugu inuka kimbia upesi kunako msaada habari ya ofisi ya kata itakudhulumu ukiwa unaona.
ReplyDeleteMuandikie barua Mkuu wa Wilaya Kindondoni Mhe Jordani Rugimbana na nakala peleka kwa Mkuu wa Mkoa na Ofisi ya Waziri Mkuu. Halafu nenda na nakala yake DC umuone na umweleze. Piga simu yake ili uombe miadi naye 0784528358.
ReplyDeleteNamfahamu Diwani wa Kimara Mheshimiwa Mringo siamini kama anahusika. Umeongea nae?