kwa picha zaidi
Home
Unlabelled
alice lushiku anyakua taji la redd's miss kinondoni 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Jamani hivi watoto wetu wa kike hawana kitu kingine cha kufanya kila wiki ni mashindano ya urembo? Vipi mpishi bora au mwanafunzi bora? Oh my god nikiona tena matokeo au matayarisho ya urembo, mifupa yangu itaruka mwilini iache ngozi peke yake. Ni fundisho gani tunawapa watoto wa kike? Yaani kiuwa mrembo ndiyo kitu cha maana.
ReplyDeleteNinapo ona haya mashindano ya U-Miss yasiyokwisha ambayo Wasichana wa Ki-Tanzania wamefanywa kuwa ndio ajira zao siku hizi huwa naona huruma. Husani wakati huu ambapo soko la ajira la jumuiya ya Afrika ya Mashariki limewekwa wazi kwa nchi zote jumuiya.
ReplyDeleteNaamini karibuni tu mtaona Wa-Tanzania wakifanywa Manamba, maboy na Mayaya ndani ya nchi yao wenyewe kwani tumekuwa watu tusio na priority na raia wetu. Kwani kila binti anataka kuwa Miss siku hizi.
Sasa, tuwalaumu hawa mabinti na wadogo zetu au? Jamani, tujiangalie sisi kwanza -- vitu gani vinapewa kipaumbele kwenye jamii yetu? Kwanini makampuni yako mstari wa mbele kufadhili mashindano kama haya? Bila shaka ni kwasababu macho yetu yanapenda hivi vitu.
ReplyDeleteAngalia hata hapa kijiweni, mijadala ya maana inakwepwa. Watu hawataki kubadilishana mawazo yatakayoleta mabadiliko au mapinduzi kwenye nyanja mbalimbali. Unadhani mabadiliko ya maana yatakuja tu hivi hivi?
Angalia vitu ambavyo wenzetu wanafanya (Bondeni):
http://vijana.fm/2010/06/30/taifa-la-wavumbuzi/
Pia, kuhusu hili suala la EA Common Market, watu waanze kujiandaa -- Polish your CVs, piga msasa ngeli, hakikisheni mnakuwa competent kwenye fani zenu. Kwasababu, ule ukweli ni kwamba, huko ndipo dunia inapoelekea (acha Afrika Mashariki kwanza).
Inasikitisha sana kwasababu bado Watanzania wengi hawajui hata EA Common Market inamaanisha nini na itakuwa ina implications gani kwa ujumla.
Tuamke jamani.. Mijadala karibia yote iliyopita ilikuwa ni kama kupinga tu EAC. Sasa imetufikisha wapi? Ingekuwa vizuri kama blogs na vyombo vya habari vyetu vingepeleka nguvu zao kuelimisha umma na kushauri nini wafanye, ili watani zetu wa jadi wakija tuwe tayari. Unadhani watu wanaipenda ardhi tu ya TZ.. Kuna mengine zaidi ya hayo! Mtu mwenye akili ya ujasiriamali anatambua kuwa kuna opportunities nyingi sana Bongo. Sisi tunajua haya?
End of my rant! Na poleni wenzangu kwa kisago "tulichopata" jana.
jamani tumechoka na hawa mamiss watafute ajira nyingine za maana sio za kuuza sura azitasaidia kujenga taifa
ReplyDeleteI don see anything wrong with beauty peagents cema inauzi pale washindani wote unakuta hawana shule and carrier wanataka kufanya ulimbwende ni kazi. Yaani hawana ambitions kabisa. Term ikiisha wanaishia kuwa waigizaji,bongo flavour artist yaani upuuzi mtupu.
ReplyDeleteNchi za watu unakuta dactari anawania umiss. sio bongo high school drop outs ndo wanachangamkia tenda
Siku nyingine ukituweka haya mambo utuwekee na historia za haa washindi...Ni nanai aamesoma wapi na anafanya nini sasa hivi...Kama wana miaka zaidi ya 18 wameshaonja maisha tujue walikopitia sio tuone wanavyokwanya tu meno hapa...
ReplyDeletetusomeshe na tuwezeshe watoto wa kike kama hamtaki wauze sura kiivi!!wazazi/walezi ni jukumu letu ndani ya familia
ReplyDeletemmeelewa?