Na Mwandishi wetu
MABONDIA Joseph Richard na Idd Ramadhani (Kg 54) wa klabu ya ngumi ya Ashanti watashindikiza pambano la ngumi la uzani wa Middle Weight kati ya Bondia Rashid Matumla 'Snake man' na Mada maugo litakalofanyika Julai 18 mwaka huu katika ukumbi wa PTA, Sabasaba Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar, Kocha wa Ashanti Rajabu Mhamila 'Super D' alisema katika pambano hilo la Kg 75 mabondia hao kila mmoja atacheza pambano la kirafiki kusindikiza pambano hilo.
Alisema bondia Joseph Richard atacheza na bondia Kijepa Omari katika pambano la kilogramu 54 raundi 4 wakati bondia Iddi Ramadhani atacheza na Antony Matias katika mapambano hayo ya utangulizi ambayo yanatarajiwa kuwa na upinzani mkali tunataka kuwahakikishia kuwa vijana wa jiji Ashanti tumeiva kila idara.
"Mabondia wangu wawili ambao wanakuja juu katika mchezo wa ngumi hivi sasa watasindikiza pambano la Matumla na Maugo, hii ni nafasi pekee ambayo klabu yetu inajivunia nafasi hii," alisema Super D.
Kocha huyo alisema mabondia ameanza kuwanoa kwa ajili ya pambano hilo ambalo kubwa na kuongeza kuwa ana imani wataibuka na ushindi katika michezo watakayocheza katika wakati huu wanapojiandaa kuwa mabondia tishio.
Mbali na hilo kocha huyo alisema ili kuhakikisha viwango vya mabondia wake vinakua kila kukicha ameanzisha programu maalumu ya kujipima kila mwezi ili kuwaandalia mazingira ya kujiamini katika michuano mbalimbali watakaopata kushiriki katika michuano yao ya ndondi.

KUNA MPAMBANO WA MCHEZO WA NGUMI WA KIRAFIKI? WAKATI WATU WANATOKA NA MANUNDU
ReplyDelete