Watanzania wameshauriwa kuzichangamkia hisa za shirika la ndege la Precision Air zitakapoingia soko la hisa baadaye mwala huu ili waweze kulimiki shirika hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Michael Shirima alisema hivi karibuni kuwa kampuni yake ina nia ya kuwamilikisha Watanzania shirika hilo na kwamba taratibu zitakapokamilika hisa za shirika hilo zitauzwa kwenye soko la hisa la Dar es Salaam.
“Bodi na wenye hisa wa Precision Air wameamua kukuza mtaji wa kampuni kwa kuwapa nafasi Watanzania wengi kumiliki kampuni hii la ndege” alisema .
Alisema kwa sasa kampuni yake iko kwenye mchakato wa kuuza hisa hizo na kwamba lengo ni kuhakikisha kwamba ifikapo mwishoni mwa mwaka huu hisa hizo zianze kuuzwa.
“Tunauhakika wa kufanikiwa na kwamba umiliki wa hisa za Watanzania utakuwa kwa asilimia 51 hadi asilimia 66, hisa zilizobaki zitamilikiwa na shirika la Kenya Airways” alisema.
Kwa upande wangu nimefurahiswa sana na maendeleo haya ingawa najua umiliki wangu utayeyuka lakini naamini kwamba kampuni itakua na kuongoza katika usafiri wa anga kwa ukanda wetu huu.
Kwa sasa Mwenyekiti huyo ana miliki asilimia 51 ya shirika na Shirika la ndege la Kenya Airways lina miliki asilimia 49.
Kwa mika 16 iliyopita shirika hilo limekuwa likipata faida na hatimaye kukua hadi lilipoingia ubia na shirika la ndege la Kenya miaka saba iliyopita.
Kwa sasa shirika hilo linafanya safari zake katika mikoa mbalimbali ya Tanzania pamoja na nchi jirani za Kenya naUganda.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...